Dawa ya babu kweli inatibu;wachunguzi muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya babu kweli inatibu;wachunguzi muhimbili

Discussion in 'JF Doctor' started by Pdidy, Apr 30, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi wa NIMRI,MUHAS
  Naye Leon Bahati anaripoti kuwa,Uchunguzi wa awali uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Muhimbili (MUHAS) umebaini kwamba dawa ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila ina uwezo wa kutibu magonja sugu zaidi ya sita.

  Katika ripoti yao wamependekeza kufanyika kwa utafiti zaidi juu ya uwezo wa dawa hiyo katika tiba, usalama, kiwango cha dozi anachopaswa kutumia mgonjwa na muda wa matumizi.

  Wataalamu waliochunguza dawa hiyo iliyosisimua na kuvuta watu wengi ndani na nje ya nchi kwenda katika Kijiji cha Samunge, Wilaya ya Loliondo, Arusha kwenda kupata dawa hiyo wamesema imewastaajabisha kwa namna ilivyo na kemikali nyingi zenye uwezo wa kuimarisha afya ya binadamu.

  Wataalamu hao, Profesa Hamisi Malebo na Profesa Zakaria Mbwambo wamesema utafiti huo wa awali umeonyesha kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kudhibiti ugonjwa wa kisukari, moyo, saratani, ini, malaria, Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababisha uvimbe mwilini, vidonda pamoja na athari za bakteria mwilini.

  Magonjwa mengine yanatajwa kuwa ni ya mfumo wa chakula, athari za mfumo wa akili na moyo kushindwa kufanya kazi sawasawa.

  “Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapaswa kuendesha majaribio ya utafiti ili kujibu maswali muhimu kama vile usalama wa dawa hiyo katika mwili wa binadamu, dozi yake pamoja na muda wa matumizi kulingana na aina ya ugonjwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo yenye kurasa 25.

  Jambo jingine ambalo wataalamu hao kutoka katika vitengo vya tafiti za dawa za asili wa NIMR na MUHAS, wanalisisitiza katika utafiti huo ni uwiano wa kemikali kwenye dawa ya mti huo walioupa jina kuwa ni wa maajabu.

  Ripoti hiyo ambayo Mwananchi ilifanikiwa kuiona, ina sehemu saba ambazo zinajumuisha shukurani kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kugharimia utafiti huo, maelezo kuhusu mti huo wa ajabu, muoanisho wa mti huo kibaiolojia, njia walizotumia kutafiti na matokeo yake, maelezo ya majumuisho na mapendekezo.

  Uchunguzi wa kimaabara
  Ripoti hiyo inaeleza kwamba katika kuchunguza sumu iliyopo katika mti huo, walitumia panya na kubaini kwamba ni salama pale ambako haitumiki mizizi hiyo moja kwa moja.

  Wataalamu hao wanaeleza njia anayotumia Mchungaji Mwasapila ya kuichemsha na kutoa dozi ya milimita 200 kwa mgonjwa ni salama na haiwezi kumuathiri binadamu kiafya.

  Wanasema kemikali zilizopo kwenye mti huo zimeonekana kuwa na uwezo wa kudhibiti magonjwa kama ambavyo Mchungaji Mwasapila amekuwa akieleza.Wanasema walipompa panya dawa hiyo, iliweza kuweka uwiano mzuri wa sukari kwenye mfumo wa damu hivyo kuashiria kwamba ina uwezo wa kutibu kisukari.

  Hali hiyo inaelezwa kuwa inatokana na mti huo kuwa na mfumo unaoweza kusababisha muanisho wa utoaji wa insulini ambayo kwenye mwili wa binadamu ni muhimu katika kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

  Kuhusu ugonjwa wa moyo, wataalamu hao wanasema dawa ya Babu ina uwezo wa kushusha mapigo ya moyo ambayo yako juu hivyo kuweza kudhibiti maradhi hayo.

  Mti huo pia umeonekana kuwa na uwezo wa kurekebisha ini ambalo halifanyi kazi zake inavyotakiwa hivyo kutibu aina zote za magonjwa zinazotokana na athari za kushindwa kwake kufanya kazi.

  Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu, moja ya kazi za ini ni kuondoa sumu mwilini na iwapo halifanyi kazi zake sawasawa, sumu hizo husababisha madhara mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.

  Wameuelezea uwezo huo kuwa unasaidia kupambana na ugonjwa sugu wa saratani.Utafiti huo pia umeonyesha kuwa mti huo wa maajabu una uwezo wa kudhibiti virusi wa aina mbalimbali kama vile vya Ukimwi na polio. Wataalamu hao walieleza kwamba walipojaribu kulinganisha panya walioambukiza virusi, aliyetibiwa kwa mti huo aliongeza uwezo wa kuendelea kuishi kwa kati ya asilimia 28 hadi 35 ukilinganisha na yule ambaye hakutibiwa.

  Ilionekana pia kuwa panya walioathiriwa na virusi waliotibiwa na dawa hiyo waliepushwa na uwezekano wa vitoto vyao vilivyozaliwa kufa mapema kwa asilimia 70 hadi 90.

  Kwa sababu hiyo, wanasayansi hao wakahitimisha kwamba maelezo ya Mchungaji Mwasapila kuhusu tiba ya Ukimwi ina ukweli ndani yake.

  Kemikali za mti wa maajabu

  Baada ya kuchunguza mti huo wa maajabu kimaabara, wataalamu hao walibaini kwamba una kemikali nane muhimu.Kemikali hizo zinajulikana kwa majina ya kitaalamu; steroids, terpenes, benzenoids, phenylpropanoid, lignans, coumarins tannins, flavonoids na cardiac glycosides.


  Sesquiterpenes (trpenes) ni kemikali ambayo kitaalamu inajulikana kuwa ina uwezo wa kukabili bakteria, malaria, saratani na visababishio vya uvimbe mwilini.Triterpenes inajulikana kitaalamu kuwa inatibu athari mbalimbali za mifumo ya mwili kama vile njia ya mkojo na uvimbe mwilini.

  Kemikali nyingine pia zinasaidia kuweka usawa lehemu (cholesterol) kwenye mfumo wa damu na nyingine kama vile ‘ursolic acid’ hupunguza nguvu ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kuzaliana kwenye mwili wa binadamu.

  Kemikali nyingine phenylpropanoids na phenylethanoids zipo kwenye kundi la pili la kemikali zinazopatikana kwenye mimea ambazo kazi yake kubwa ni kutibu vidonda, athari za hewa chafu na mazingira ya hewa yenye athari za mwili.

  Coumarins husaidia mambo mbalimbali mwilini athari za moyo hasa zinazosababisha kupungua uwezo wa kusukuma damu na kutibu athari za mfumo wa chakula pamoja na wa akili.

  Historia ya mti wa maajabu

  Mambo yasiyo ya kawaida kuhusu mti huo wa ajabu yanaelezwa kwamba yalijitokeza kwa kasi katika Kijiji cha Samunge Agosti, 2010.

  “Watu wengi walifurika katika Kijiji cha Samunge kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kupata tiba ya magonjwa sugu,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

  Wametaja magonjwa hayo sugu kuwa ni kisukari, Ukimwi, pumu, saratani na kupooza ambayo wanaeleza kuwa Mchungaji Mwasapila alikiri anayatibu baada ya kuoteshwa tangu mwaka 1991.

  Katika uchunguzi wao, wataalamu hao walisema mti huo una majina mbalimbali kutokana na makabila tofauti mkoani Arusha.Wanasema Mchungaji Mwasupila aliwaambia mti huo unaitwa “mugariga” wakati Wamasai wanauita “engamuriaki” au “olmuriaki” na kabila la Wasonjo linauita “engamuriaga.”

  Kulingana na maelezo waliyoyapata kutoka kwa mchungaji huyo, wakati wa maandalizi ya dawa hiyo, huchemsha mizizi yake kwa saa moja na baadaye huachwa ipoe kabla ya matumizi.

  Jambo ambalo liliwashangaza wataalamu hao ni kwamba mchungaji huyo maarufu kwa jina la Babu, amekuwa akisisitiza kwamba ili dawa hiyo ifanye kazi ni lazima yeye binafsi aimimine kwenye kikombe atakachokunywa mgonjwa. Kikombe chake huwa anakitumia kama kipimo.

  Uchambuzi wa mti kisayansi

  Wataalamu hao walisema baada ya kuuchunguza mti huo walibaini kitaalamu unaitwa carissa spinarum ambao upo katika jamii ya apocynaceae.

  Wanauelezea kuwa ni mti wenye miiba na utomvu kama maziwa, majani yenye kijani cha kukolea kwa juu na chini yake viotea kama nywele laini na mti humea hadi urefu wa mita tano kutoka usawa wa ardhi.

  Katika kuzaa, wanasema mti huo hutoa maua meupe na mchanganyiko wa rangi nyingine kama vile nyekundu, pinki na zambarau.

  “Huzaa matunda ya mviringo yenye kipenyo kinachokadiriwa kuwa sentimita 1.1 na yanapoiva huelekea kuwa na rangi nyeusi… Ukiyala ni matamu na ya kufurahisha. Ndani huwa na mbegu mbili hadi nne,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.

  Nchi ambazo mti huo unaweza kupatikana zinatajwa kuwa ni Australia, Botswana, Cambodia, Cameroon, Eritrea, Ethiopia, Ghana, Guinea, Japan, Kenya, Myanmar, Namibia, Nigeria, Papua, Saudi Arabia, Senegal, Afrika Kusini, Sudan, Thailand, Uganda, Vietnam na Yemen.

  Matumizi ya mti huo kijadi
  Wamasai wanaelezewa kuwa wamekuwa wakiutumia mti huo kama sehemu ya kunogesha chakula. Jamii nyingine za hapa nchini zinazoutumia ni Wasonjo, Wagogo, Wakurya na Wabarbaig.

  Uchunguzi wa pia umebaini kwamba Ghana hutumia matunda ya mti huo pamoja na chakula kama sehemu ya kumfanya mgonjwa kupata hamu ya kula.

  Katika nchi nyingine kama Kenya na Sudani, hukamua mbegu zake ili kupata juisi.

  Katika bara la asia baadhi ya watu wanaelezewa kuwa huitumia mizizi yake kwa ajili ya kuzuia kuharisha.

  Pamoja na maelezo mazuri ya utafiti huo wa awali, wataalamu hao wamesema serikali inapaswa kuweka mkakati wa utafiti wa kina zaidi ili kuwa na mkakakti bora wa kitaalamu kuhusu dawa hiyo.

  Miongoni mwa mapendekezo yao ni kuitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa fedha kwa ajili ya utafiti huo ambao utatoa picha halisi ya tiba za mti huo wa ajabu na hasa kujibu maswali muhimu ya uwezo wake katika tiba, usalama, kiwango cha dozi anachopaswa kutumia mgonjwa na muda wa matumizi.
   
 2. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Pdidy, Asante Kwa taarifa nzuri, Sina jinsi zaidi ya kukubaliana na utafiti huu kwa sababu umefanywa na wataalamu lakini muda waliotumia kufanya utafiti ni mfupi sana.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nashukuru sana kwa ripoti yenye ma2maini ya kutosha ya Mungu na utafiti ya kiutaalam. Na ss nitakuwa njia moja ku2a kw Babu.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wakuu... liverproof & Pdiddy...asante sana ...yahitajika imani, matumaini na tiba bioogically katika dawa hii ... mama yangu amepona sukari na presha ... namshukuru mungu
   
 5. K

  Kivia JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bado tunawasikiliza wataalamu wetu., kwani kuna ku kupunguza makali ya ugonjwa na kupona. Tuliwahi kuona dawa kama KEMRON ambazo zilithibitishwa kutibu lakini leo ziko wapi. Tunaomba zitengwe hosp na uchunguzi ufanyiwe wagonjwa kupata uhakika.
   
Loading...