Dawa na suluhisho la upweke

Dawa na suluhisho la upweke

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
42,561
Reaction score
105,373
Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba upweke ni kuwa wao peke yao. Na hivyo ili kuondokana na upweke wamekuwa wakikazana kuhakikisha wanazungukwa na watu wengi.

Licha ya kuzungukwa na watu hao wengi bado upweke walionao hauishi. Bado wanajiona wapweke licha ya kuwa kwenye kundi kubwa la watu.

Badala ya kutatua tatizo la upweke ambalo watu wanalo, wamekuwa wakitafuta njia za kukimbia tatizo hilo, kulificha lisionekane. Na wamekuwa wakificha tatizo hilo kwa kutaka kuzungukwa na watu wengi na kuepuka kuwa peke yao. Na dunia hii ya sasa ambapo mitandao ya kijamii inatuunganisha na
dunia kwa masaa 24 kwa siku, njia za kukimbia upweke zimekuwa nyingi zaidi.

Kwa uwepo wa mitandao hii hata mtu anapopata nafasi ya kuwa yeye mwenyewe, haraka sana
anaingia kwenye mitandao ili kujua kipi kinaendelea huko. Hii yote inazidi kukuza tatizo hili na inaweza kufika wakati likashindikana kufichika na madhara yakawa makubwa.

Dawa ya upweke, Ni kujikubali wewe mwenyewe kwanza. Kama huwezi kujikubali wewe mwenyewe, kwa vile ulivyo, hata uzungukwe na watu wengi kiasi gani, hata uwe kwenye mitandao gani ya kijamii, bado
utajisikia mpweke. Bado utaona kuna kitu hakijakamilika kwako na utaona maisha yako yana kasoro.
Na ili kujikubali ni lazima ujijue wewe mwenyewe, na utajijua kwa kupata muda tulivu wa kuwa wewe
mwenyewe, kuyatafakari maisha yako na kujua kipi unapendelea na kipi unaweza vizuri.
Pale unapoweza kukaa wewe mwenyewe na usijione mpweke, hapo ndipo unapokuwa umetibu tatizo la upweke. Usikimbilie watu au mitandao ya kijamii, anza na wewe mwenyewe.

Ukweli ni kwamba upweke hautokani na wewe kukosa watu kwenye maisha yako, bali unaanzia ndani yako mwenyewe, kwa kutokujijua vizuri na kujikubali. Dawa ya upweke ni kujijua vizuri na kujikubali kwa vile nilivyo. Usikimbilie tena kuzungukwa na watu au mitandao ya kijamii kuondoa upweke wako, badala yake anza kuondoa upweke ndani yako.

images%20(2).jpg
images.jpeg
 
Loneliness.... noma sana hii kitu

From personal experience mimi niko so introvert kiasi kwamba nilifika stage ya kutotaka hata kukaa na mimi mwenyewe

Nikaanza kutumia other substances(drugs) ili akili ihame nisiweze hata kujua nawaza nini yaani nikawa najikimbia mwenyewe....

But i have learned to face my demons... tatizo liko ndani na wala sio nje...

To ne born again we must firs be willing to die...

Bado niko kwenye process ya kujiua mimi mwenyewe ili nizaliwe upya
 
Pole sana Mkuu.

The same to Me..Nilipangiwa kazi Mkoa ambao Sikuwahi kufika kabla..Upweke uliniandama mno nilidhani kwa kuwa na marafiki wengi itasaidia but haikuwa hivyo.

Katila kukaa na kujifikiria nikaja kugundua upweke ni zaidi ya kuzungukwa na marafiki muda wote, Ili kuukabili upweke kiukamilifu ni lazima ujikubali na uyakubali madhaifu yako.

To be happy, One has to recognise the special gift given by God and feel thankful about it. Comparing oneself with others,or complaining all the time that God has been unfair,will do nothing but bring about unhappiness and discontent.
 
Aiseeeeee.....
 
Lazma wengne tuwe wapweke tu hakuna jinsi

Tena mm ndo mpweke zaid naweza shnda ndan asubuh mpka jion
Mkuu, kwahiyo hata hautoki nje ili ufanye shughuli yeyote...
 
Pole sana Mkuu.

The same to Me..Nilipangiwa kazi Mkoa ambao Sikuwahi kufika kabla..Upweke uliniandama mno nilidhani kwa kuwa na marafiki wengi itasaidia but haikuwa hivyo.

Katila kukaa na kujifikiria nikaja kugundua upweke ni zaidi ya kuzungukwa na marafiki muda wote, Ili kuukabili upweke kiukamilifu ni lazima ujikubali na uyakubali madhaifu yako.

To be happy, One has to recognise the special gift given by God and feel thankful about it. Comparing oneself with others,or complaining all the time that God has been unfair,will do nothing but bring about unhappiness and discontent.
Duhhhh...
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom