Dawa na njia mbadala za Kupunguza unene/uzito | Weight Loss techniques and advice

Hapo kwny chia seeds nmeijaribu kuitumia labda nianze tena

Loweka for ten minutes
Iweke kwa friji
Kisha tumia kutengenezea juice


Unajua unaweza kufanya diet ya juice na ukapungua huku ukibaki kuwa na afya na kinga ya kutosha?
 
Kupungua uzito kwanza inabid ujijue why umeongezeka uzito ghafla. Kuna watu wengne wana nature ya miili minene, kuna koo za namna hii, yan wao wale san wasile san wakifikisha umri flan wanakuwa mabonge automatically na kuna wengne ni viceversa, hata wafanyeje miili haiongezeki ng'oo.

Km unene wako sio geneticaly inherited basi kutakuwa na other causes ambayo ww binafsi unaijua. Kwa hiyo ukishaijua hiyo cause basi change that habit na utapungua bila wasiwasi.

Nikupe mfano, mm mwshon mwa mwaka jana nilikuw na 74kg. Kufika July mwaka huu zikaongezeka mpk 78kg. Kwa hiyo nikawa najiona mzito san plus kakitambi uchwara. Nikaona hii hali hapana. Lkn nikawa najua kabsa hii imesababishwa nature ya kaz yangu. Nilikuw nakula vzr lkn kile nachokula hakifanyi kaz ipasavyo.

Hivyo nikaamua kupunguza mlo, nikiwa kazin asbh sinywi chai nakula lunch tuu basi. Na nikirudi home sili tena chakula kizito, either nakunywa chai ya maziwa tuu ama naongezea na bites yyte ya kudanganyia tumbo. Ndani ya mwezi nilipunguza kilo 4, na mpk sasa znaendelea kupungua, nina 73kg now.

Kazi kwako.
Na vipi hyo lunch ulikuwa unapiga wanga kama kawaida au ?

Na
 
Ngoja nikwambie kitu ndugu.. hakuna dawa inayoweza kukupunguzia uzito, cha msingi ni kubadilisha vitu unavyokula au kupunguza kiasi unachokula na pia badili life style kama walivyokwambia hapo juu. Mazoezi ni 20% ya kupunguza uzito, 80% ni diet
 
Mazoezi ndo kila kitu nimegain weight sana hiki kipindi Nina week Sasa tangu nianze mazoez ukinuona kama uliniona week nyuma lazima ushangae mana nimeloose weight kiasi kikubwa sana tambi limeanza Isha kabisa lakini ratba yangu ya mazoez ni ngumu mno kama huna moyo mgumu huwezi kabisa ganya
 
Ngoja nikwambie kitu ndugu.. hakuna dawa inayoweza kukupunguzia uzito, cha msingi ni kubadilisha vitu unavyokula au kupunguza kiasi unachokula na pia badili life style kama walivyokwambia hapo juu. Mazoezi ni 20% ya kupunguza uzito, 80% ni diet
Sure mkuu misosi ndo uharibu kila kitu me nimeweza kwa kweli ndani ya week tu nimebadili life style yangu lakini pia nafanya mazoezi makali sana yani nilichokipata ndani ya hii week kuna watu wanaweza kipata hata miezi sita....
NB : ninaandika hii post kutokea viunga vya gym
 
Nadhani ushauri umeshaupata wa kutosha kutoka kwa wadau waliotangulia. Badala ya kurudia point ngoja niongezee kitu.

Ukitaka kuwa na afya bora, jiku kubwa ni mazoezi na diet.

Ila hivi vitu wengi tunachukulia kama ni adhabu na kuwa unafanya wakati flani tu.

Ukweli ni kwamba, badilisha life style. Kama mnywaji sana, punguza, badala yake kunywa maji. Pale mezani bar akikisha kuna chupa ya maji.

Tafuta sehemu yenye kidistance kidogo ya kupaki gari. Kwa hiyo utapaki pale na kutembea kidogo kwenye kazini na kurudi.

Tumia ngazi, kama ni nyingi, panda lifti na ushuke floor isiyo yako, malizia kwa ngazi.

Ni vitu vidogo vidogo lakini vinahitaji consistent. Baada ya muda, hutoona ni mazoezi bali ni life style yako.
 
Ngoja nikwambie kitu ndugu.. hakuna dawa inayoweza kukupunguzia uzito, cha msingi ni kubadilisha vitu unavyokula au kupunguza kiasi unachokula na pia badili life style kama walivyokwambia hapo juu. Mazoezi ni 20% ya kupunguza uzito, 80% ni diet
Kweli kabisa mi nimepungua kwa kupunguza chakula tu nilikuwa na 80 sasa hivi kila nikipima uzito ni Kati ya 70 na 72 na hapo sifanyi mazoezi
 
Sure mkuu misosi ndo uharibu kila kitu me nimeweza kwa kweli ndani ya week tu nimebadili life style yangu lakini pia nafanya mazoezi makali sana yani nilichokipata ndani ya hii week kuna watu wanaweza kipata hata miezi sita....
NB : ninaandika hii post kutokea viunga vya gym


haha hatari sana. keep it up mkuu.
 
Hii inanikumbusha nina Rafiki yangu alikua anataka kupungua Kilo, ah Kazini kwao akapewa HOWO kutoka katika SCANIA aendeshe hahaha acha limtafune Mwili hadi kawa kama alivyotaka, ila waone Wataalamu uenda wakakusaidia
 
Badilisha life style yako. Mazoezi, piga jogging sana, jogging inakata uzito, piga mazoezi ya kukata tumbo kila siku. Badili mlo wako. Mimi nikaamka nakunywa maji ya moto, then ninapiga jogging 8 kms everyday in the morning, baadae nakula matunda na glass moja ya maziwa.

Mchana nakula lunch ya nguvu ila naangalia sana mafuta. Jioni ni kachai tu au matunda tena. Hapo lazima afya yako ishike adabu. Usiwe unakulakula hovyo. kama mazingira yako hakuna sehemu ya kufanyia viongo, piga mazoezi hata chumbani kwako. Kila la kheri
 
UPDATES
sasa hivi nmeanza diet ,
Asubuhi : chai na chapati mbili kama kawaida
Mchana : matunda full
Usiku : mhindi 1 au 2 ya kuchoma
Nahitaji kutumia almost 1200-1400 calories per day,ili niache almost 500calories lakini nahisi itakuwa zaidi ya hapo
Nahitaji kwa wiki npungue 0.5 kg had 1 kg inatosha
Mazoezi;nitaanza na kutembea umbali wa kawaida tu
Maji nahitaji kunywa zaidi ya lita 3.5 kwa siku.
Vp hapo wadau...ushauri wenu wakuu
 
Back
Top Bottom