Dawa Mseto zatoweka nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa Mseto zatoweka nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Dawa Mseto zatoweka nchini


  na Hellen Ngoromera


  [​IMG] DAWA Mseto za kutibu ugonjwa wa malaria [Artemether and Lumefantrine (ALu)] zinadaiwa kutaifishwa nje ya nchi na baadhi ya vigogo hivyo kusababisha kupotea kabisa hapa nchini. Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini dawa hizo ambazo ziliingizwa nchini na serikali na kupatikana katika hospitali/zahanati za serikali pekee zinadaiwa kupotea tangu kipindi cha mchakato wa uchaguzi uliofanyika mwaka jana.
  Kutokana na kutaifishwa kwa dawa hizo nchini tayari zilishaanza kuonekana katika nchi za Zambia, Kongo na Zimbabwe.
  Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Tanzania Daima ilikuwa ikifanya uchunguzi katika hospitali mbalimbali za serikali hasa za jijini Dar es Salaam na kubaini kwamba dawa hizo hazipo.
  Ili kutafuta ukweli wa hilo mwandishi wa habari hizi alikwenda kujitibu malaria katika hospitali ya Mnazi Mmoja na Temeke na kuomba aandikiwe dawa hizo mseto, lakini alielezwa kwamba hazipo.
  Hata hivyo, hakukata tamaa bali aliamua kutafuta mbinu na kuweza kuandikiwa dawa hizo katika cheti ambacho alizunguka nacho katika hospitali mbalimbali za serikali bila mafanikio.
  Akiwa katika moja ya hospitali hizo mwandishi alizungumza na baadhi ya wagonjwa ambao walimweleza kuwa nao walikuwa wakiumwa malaria lakini kwa kuwa walikuwa wanatumia dawa mseto waliomba waandikiwe dawa hizo lakini walielezwa kuwa hakuna.
  “Sikufichi nilishazizoea dawa hizi, baada ya kuelezwa kwamba hakuna;
  nilihangaika ikiwemo kumpigia simu daktari wangu mmoja wa serikalini ambaye siku iliyofuata aliweza kunisaidia.
  Aliniletea dozi ambayo haikutimia na alipofika ofisini aliongezea vidonge vilivyosalia ambavyo alilazimika kuviomba kwa watunza dawa na alibahatika kuvipata kutokana na kuachwa na wagonjwa waliokuwa wakivitapika walipopewa hivyo kuharibu dozi,” alisema Leila Jabir.
  “Dawa hizi zilipotea tangu kipindi cha siku nyingi lakini hasa wakati wa kipindi cha uchaguzi, wakubwa walizichakachua kwa kuziuza nje ya nchi ili kupata faida zaidi.
  “Hivi unafikiri mtu akiuza dozi moja kwa sh 5,000 au zaidi ana hasara gani isitoshe yeye kanunua kwa bei ya kutupa, nchi hii acha kabisa ndugu yangu,” alisema mmoja wa madakatari wa hospitali ya serikali ambaye jina lake tumelihifadhi.
  Chanzo hicho cha habari kilieleza kwamba kwa kuwa dozi ya dawa hiyo huuzwa kwa sh 500 katika hospitali za serikali baadhi ya vigogo wa serikali waliamua kuzifanyia mradi na kuzitaifisha nje ya nchi ili kupata fedha nyingi ambazo zingewasaidia kwenye kampeni.
  Inaelezwa dawa hizo zilitumika kama mtaji ili kuwawezesha baadhi ya vigogo hao hasa waliokuwa wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa kampeni kupata pesa za kuendeshea kampeni.
  Kwamba vigogo hao walizinunua kwa wingi na kwa bei inayoouzwa katika hospitali za serikali kisha kwenda kuzilangua katika nchi za mbali.
  Pamoja na dawa hizo kupatikana kwa bei nafuu katika hospitali za serikali, katika maduka ya dawa mseto zinauzwa kwa bei ghali ya kati ya sh 10,000 hadi 18,000 kwa kutegemeana na nchi iliyotoka au iliyotengenezwa.
  “Mimi nina jamaa yangu yuko Zimbabwe, kuna siku kanipigia simu na kuniambia kwamba anaziona dawa zetu za mseto tena zenye nembo ya Tanzania nchini humo, hali hii inatisha dadangu,” kilisema chanzo hicho.
  Kutokana na kuadimika kwa dawa hizo, wagonjwa wanaokwenda kwenye hospitali hizo hupewa dawa mbadala ya SP kutibu malaria.
  Hata matangazo yake ya kuhamasisha matumizi yake hayatangazwi tena kwenye vyombo vya habari hasa redio na televisheni.
  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, hakukanusha wala kukubali kuhusu suala hilo.
  Badala yake alisema hawezi kulizungumzia zaidi kwa njia ya simu ikizingatiwa kwamba linadaiwa kuwahusisha wakubwa (vigogo) na linavuta hisia kubwa kwa jamii hivyo aliahidi kulitolea ufafanuzi leo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,308
  Likes Received: 418,592
  Trophy Points: 280
  Waganga wa kienyeji nao huzinunua na kutengeneza mkorogo na kuwauuzia waathirika............nchi hii sasa ni nyang'anyang'a kabisa.................
   
 3. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ebwaanae! ndo maana shida kuziPata. tanzania tanzania nchi yangu tanzania.
   
Loading...