ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
MAMILIONI ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ulimwenguni, sasa wanaweza kupata tumaini jipya baada ya wanasaynsi wa nchini Isreali kugundua dawa ambayo inasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu Ukimwi.
Wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Hebrew kilichopo Jerusalem nchini Israeli wamegundua dawa yenye protini ambayo wanadai inaweza kupunguza virusi vya Ukimwi kwenye mwili wa mgonjwa kwa asilimia 97 ndani ya siku saba tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Times la Israel.
Ugunduzi huu mpya sasa unatoa tumaini jipya katika utafutaji wa dawa ya ungonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba ukiwa umeshaua watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka 2015 pekee.
Virusi vya Ukimwi hushambulia chembe chembe nyeupe za damu zinazojulikana kama CD4 ambazo husaidia kupigana na magonjwa yanayoingia mwilini.
Virusi vya Ukimwi huingia ndani ya chembe chembe hai nyeupe na kujizalisha kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa CD4.
CD4 zinapokuwa chini ya 200 kwa kyubiki milimita za ujazo wa damu, mgonjwa anahesabika kuwa tayari ameanza kuugua Ukimwi.
Ugunduzi huo mpya umehusisha majarabio ya dawa hiyo mpya ambayo iliwekwa kwenye damu ya wagonjwa 10 wa Ukimwi iliyokuwa kwenye chupa maalumu kwa ajili ya majaribio.
Sehemu kubwa ya dawa hiyo ambayo ilipewa jina la Gammora na watafiti, ilisababisha uzalishaji wa DNA ya virusi hao ndani ya CD4 iliyoathirika kujizalisha kwa wingi badala ya utaratibu wa kawaida ambao huzalisha moja au mbili.
Hii inasababisha chembe chembe nyeupe zilizojeruhiwa kujiharibu zenyewe na kuzifanya zishindwe kusambaza virusi zaidi.
Majarabia yanahusisha dawa hii mpya ya Gammora yataendelea kukiwa na matumaini makubwa kuwa itaweza kuua asilimia 100 ya seli zilizoathiriwa na Virusi vya Ukimwi.
Abraham Loyter mmoja ya wagunduzi wa dawa hiyo mpya, aliliambia gazeti moja la Israeli kuwa ugunduzi huo mpya unaleta tumaini jipya.
“Tunachokifanya sisi ni kuharibu seli ambazo zimeathirika na kwa hiyo zitakufa moja kwa moja na hazitaweza kusambaza tena virusi,” anasema.
Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Israeli ilitangaza kwa mara ya kwanza kugawa dawa zenye uwezo wa kuzuia maambukizi kwa makundi yenye hatari zaidi ya kupata maambukizi mapya. Dawa hizo zinazojulikana kama prophylactic drugs zinapomezwa mara kwa mara zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia maambukizi.
Kwa sasa, dawa pekee kwa watu wenye virusi vya ukimwi, ni dawa za kupunguza makali ambazo humezwa kila siku ambazo pia hupunguza uwezekano wa maambukizi mapya.
Historia inaonyesha kuwa VVU ilitokea kwa nyani waliopo katika Afrika ya kati katika miaka ya 1900. Kutokana na mwingiliano kati ya tamaduni tofauti na mataifa, vilianza kusambaa duniani.
Ukimwi uligundulika nchini Marekani miaka ya 1980 na ulijulikana kama Ukosefu wa Kinga kwa Mashoga (GRID). Kadiri muda ulivyokwenda, wagonjwa wengine watano waligundulika nchini humo, wote wakiwa ni mashoga mwaka 1981.
Wakati watafiti na wanasayansi wakiendelea kuumiza vichwa kupata majibu ya dawa ya ugonjwa huu unaendelea kugharimu maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kila mwaka, bado tiba au kinga yake ya uhakika imekuwa mtihani mkubwa ambao hadi sasa hakuna aliyeufaulu. Hata hivyo, wugunduzi huu wa wanasayansi wa Israeli unaweza kubadilisha matokeo.
Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini zina asilimia ndogo mno ya maambukizi yanayokadiriwa kuwa 0.1. Hii ni tofauti na nchi za Kiafrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo karibu asilimia tano ya watu wake wanakadiriwa kuwa wameaambukizwa VVU.
Kwa sasa tuna watu 7,500 ambao wanaishi na VVU hapa Israeli,” anasema Dk. Margalit Lorber ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Afya cha Haifa's Rambam kinachoshughulika na magonjwa yanayotokana na upungufu wa kinga ya mwili. Wagonjwa wapya 450 huripotiwa kila mwaka,” anaeleza.
Wakati asilimia ya watu walioathirika na VVU nchini Israel ikiwa ni asilimia 0.1, nchi hiyo ilianza tafiti kuhusiana na ugonjwa huo miaka 1990 wakati kulipokuwa na msukumo mkubwa duniani juu ya utafiti wa VVU na Ukimwi.
Wanasansi walioshiriki katika utafiti wa dawa hiyo mpya wanasema, majaribio ya ufanisi wa dawa hiyo yataanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na wanatarajia kuifanya tiba hiyo kuwa ya gharama nafuu kuliko dawa zozote za ugonjwa huo.
Gammora: The Possible Israeli Cure for AIDS - The Media Line