Dawa gani nzuri ya kutibu Fungus?

Dawa gani nzuri ya kutibu Fungus?

Safi sana mkuu,, upo vzr....

Vp kuhusu hii dawa chini inafaa kwaajili ya fungus ? Na je kama inafaa, ubora wake dhidi ya Terbinafine cream upoje ?
View attachment 1959811
Hii haitibu inapoza tu. Tena Usijaribu kuitumia ndio itakuwa mazima hautakuja kuiacha, ukistop siku Tatu tu unawashwa hadi unajichuna ngozi,(wahindi nuksi sana) ukipaka unapoa na kung'aa kama mzungu.
Madem huwa wanaitumia kupaka maeneo yenye Sugu kwenye mwili Hasa mapajani.
 
Basi haikuwa fungus hiyo...vi vitu watu wengi wanachanya.,mtu anawezakwambia ana fungus lakini ukiangalia unaona ni ugonjwa wa zinaa.
Du hatar bas... kwa mwanaume inawezekana gonjwa la znaa ukaish nalo zaid ya Miaka miaka5 na likawa lina act kama fungus tu miwasho kdogo..ukltbu halitok..
 
Muathirika Ni KE au ME?

Watu mnatoa ushauri hata hamjui Ni sehemu za Siri zenye utamu au Ni za kiume.
Kujua jinsia na umri wa mgonjwa Ni prerequisite ya kutoa tiba.
 
Pole sana mkuu,hiyo dawa uliyoweka kwenye picha ni steroid haitibu fungus, actually hua haishauriwi kutumia steroid kama una fungus.Kama una uhakika ni fungus kanunue Terbinafine cream upake asubuh na jioni baada ya kuoga.Hakikisha unavaa nguo za ndani safi wakati wote,hakikisha taulo lako ni safi,hakikisha unavaa nguo za ndani zilizokauka vizuri na taulo yako uwe unaanika mara baada ya kutumia...ukitumia hiyo dawa ukipata nafuu usiache ghafla,ongeza angalau siku nne mbele za kupaka hata kama utaona tatizo halipo.
Hii kwakweli hata mimi ndio iliniondolea kabisa tatizo la fungus. Japo siku ya kwanza kupaka fungus watafumka balaa na maumivu kidogo
 
Dettol sio dawa ya fungus tafadhali.

Shule zenu zinawaponza mnajua tuu "how" lakin "why" hamjui ingekuwa Bora sana Kama ungeanza kuchunguza hyo Dettol ya maji inavitu gani ndan na he hvyo vitu vikikutana na bacteria au fungus inakuwaje?

Dettol ya maji ndo sululisho la huyu jamaa anapaka Leo asubuh kesho asubuh anakuwa ameshasahau kuingiza mkono na kujikunakuna.

Mie n Shahid wa hili na wapo wengi nimewapa ushauri na wakapona kwanza matokeo yake n ya muda mfupi shughuli imeisha.
 
Wakuu mnisaidie dawa ya fungus za miguuni . Zinanitesa Sana. Natanguliza shukrani wakuu
 
WanaJf naombeni ushauri je ni dawa hani Nzuri ya kutibu Fangas sehemu za Siri ? Nimeshatumia dawa lakin naona mambo hayakai sawa ... Naombeni ushauri View attachment 1959652
Tumia SONADERM-GM paka usiku baada ya kuoga na mwili kukauka kabisa na asubuhi fanya hivyo, pia hakikisha sefu unaibadirisha kila siku na ifuliwe kwa dawa ya madoa iwe safi iliyopigwa pasi.
Kama usipoona dalili za mafanikio kwa siku nne, nenda kwa dakitari.
 
Wakuu mnisaidie dawa ya fungus za miguuni . Zinanitesa Sana. Natanguliza shukrani wakuu
Anza na usafi wa miguu hakikisha hauchezi kwenye maji au tope (hiyokazi waachie bata), soksi badilisha kila siku na ziwe safi na vaa viatu vinavyopitisha hewa ya kutosha ili miguu iwe mikavu pia safisha miguu kwa vanila (ile ya maji inayotumika kusafishia mboga na matunda pia kulainishia nyama) kisha paka SONADERM-GM
 
Tumia Apple Cider Vinegar kwa kuipaka na pamba kwenye maeneo zinazosumbua.
 
Anza na usafi wa miguu hakikisha hauchezi kwenye maji au tope (hiyokazi waachie bata), soksi badilisha kila siku na ziwe safi na vaa viatu vinavyopitisha hewa ya kutosha ili miguu iwe mikavu pia safisha miguu kwa vanila (ile ya maji inayotumika kusafishia mboga na matunda pia kulainishia nyama) kisha paka SONADERM-GM
Akisha fanya yote hayo, aachane na wanawake cheap na vile vyumba vya short time kwenye Gest za uswazi. Bora ulipie chumba 25k or above na ujiandikishe kwenye register lkn kisafi na hakitumiwi ovyo kuliko vile vya 15k special for short time ambavyo huhitaji kujisajili na hupewi risiti. Shuka huwa hazibadilishwi na uwezekano wa kupata fungus, kunguni, chawa na magonjwa ya ngozi Ni mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom