Dawa gani itamsaidia mtoto mchanga kupata choo?

mataka

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
286
61
Wadau nina mtoto mchanga wa siku kumi, anasumbuliwa sana na kukosa choo ana siku ya 4 hajakipata tumempa glucose siku 2 bado hajapata, kama kuna mwenye ufahamu chanzo ni nini tafadhali tujuzane na ipi tiba nzuri kwake. Nitashukuru
 
mpe maji ya uvuguvugu mara kwa mara ila kiasi kidogo sana (kama nusu ya kijiko kidogo cha chai),itamsaidia mara nyingi kila anapomaliza kunyonya maziwa ya mama .
 
tafuta mafuta ya samaki, yanauzwa madukani kisha mpe kidogo sana lakini kabla hujampa soma maelekezo kwanza maana huyo ni mtoto wa umri wa chini mno na pia mwulize muuzaji!
 
Mkuu mwache tu atajisaidia mwambie mama yake akazane sana kumyonyesha na ashibe sana ,hii nidawa nzuzi zaidi au tafuta mafuta ya samaki
 
Pole, mkuu ..una maanisha alipata choo kisha ikaacha?
- Ananyonya kiasi cha kutosha?
- Tofauti nakukosa choo mtoto, tumbo la mtoto likoje, anacheua sana /kutapika?..tumbo limeongezeka ukubwa?
-Vipi katika haja ndogo, anapata?
-Ana homa?..
Mkuu kwanini usifike HOSPITALI mapema?
 
Pole, mkuu ..una maanisha alipata choo kisha ikaacha?
- Ananyonya kiasi cha kutosha?
- Tofauti nakukosa choo mtoto, tumbo la mtoto likoje, anacheua sana /kutapika?..tumbo limeongezeka ukubwa?
-Vipi katika haja ndogo, anapata?
-Ana homa?..
Mkuu kwanini usifike HOSPITALI mapema?

ndio alipata afu ikaacha, homa hana, kucheua anacheua akishanyonya, tumbo lake la kawaida, haja ndogo anapata
 
Pole sana,huyo mtoto ni mdogo sana kumpa vitu bila ushauri wa daktari unaweza kuta unaliongeza tatizo badala ya kutibu na hata kumdhuru.Mpeleke hosptal au Furaha clinic iliyopo pale Morocco
 
Wadau nina mtoto mchanga wa siku kumi, anasumbuliwa sana na kukosa choo ana siku ya 4 hajakipata tumempa glucose siku 2 bado hajapata, kama kuna mwenye ufahamu chanzo ni nini tafadhali tujuzane na ipi tiba nzuri kwake. Nitashukuru

Ni kawaida kabisa,anagain weight,usimpe chochote,maziwa ya mama yake ni dawa tosha,kama ulimpa kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama ni mbaya sana,maana bado ni mdogo,na hayo ndio yanayochangia complications za matumbo ya watoto wachanga,system yake bado haijaweza kudigest chochote zaidi ya maziwa ya mama.Ukianza kumpa other things ndio utapata nae shida,mwache anyonye tu,choo akikosa hata 4days haina neno,nenda hata hospital ataambiwa the same ninachokuambia,labda kama ulimpa kitu kingine zaidi ya maziwa ya mama.Nakuambia choo atapata tu,tena kitakuwa kingi mpaka utashangaa.
 
Mkuu usimpe mtoto wa siku 10 kitu chochote( ninashangaa wengine wanasema hadi ukwaju!!!).....kama ananyonya, anapata usingizi wa kutosha, amechangamka...anakojoa..kama hana shida yoyote katika vitu hivyo mwache hivyo hivyo....ndio anakua hivyo, mtoto akipata choo kila saa sio nzuri pia, ipo siku atapata choo zaidi ya mara tatu kwa siku tena kingi.....na ikitokea hivyo usiogope pia ni kawaida!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom