Hivi kwanini una justify tweet ya davido? Unaamini hawezi kukuponda we mtanzania au?
Hukumbuki p-square walivyokuja bongo wakasema eti hawamjui diamond wala hawajawahi msikia. Wakati Obama "the world's president" alivyokuja bongo alimtaja hasheem thabit ambaye ata NBA hafanyi vizuri, just Because ya ustaarabu na kuthamini mchango wa watanzania.
Mimi sio fun wa diamond, but niko hapa kutetea utanzania, siwezi kusema its ok. Wakati najua mtu anajaribu kutudharau.
Sasa we ndugu yangu kama unajaribu kujustify na kutetea ata kwenye kudharauriwa its you (kisa tz nchi ya amani) huu ni upuuzi.
Davido na wenzake wote walilenga kupondea mshindi wa big brother from TZ. Usijustify ujinga.
Angalia insta na tweet zingine za davido, kijana always ana mdomo mchafu wa kujisikia, hana ata ustaarabu. Sijui wewe unatetea nini.
Wana dharau hao siku Niko na wawest Africa wakawa wana shangaa simu yangu eti na wewe Una simu nzuri tunajua Nyie ni maskini walinikeraje wanatujua kuwa si ni choka mbaya wangejua
Mkuu, mbona suala la Obama & Hasheem, na P Square & Nassib ni vitu viwili tofauti, kiasi kwamba nashangaa kwanini umevitumia kwa pamoja kama vile ni vitu vinavyofanana. Kwa kuwa tupo kwenye jukwaa lenye members kama laki mbili hivi, ngoja nitumie muda mfupi kujaribu kuwekana sawa.
Suala la Obama na Hasheem, ilikuwa rahisi kwa Obama kukiri kumtambua Hasheem, kwanza anaishi kwenye nchi yake na anayoiongoza. Pili, Obama ni shabiki wa NBA na kwa Marekani karibu kila mchezaji wa NBA ni super star, isitoshe Hasheem ni mmoja wa wachezaji wawili wa kikapu aliyefanya vizuri kwenye Draft ya kuingia NBA.
Ni Tanzania tu ndio tunaomchukulia poa Hasheem, lakini kwa Marekani jamaa anapewa heshima kubwa tu, ukipata nafasi ya kuwa Marekani na ukakutana naye kwenye mijumuiko ya watu kama vile Night Clubs au kwenye viwanja vya NBA na sehemu nyingine zinazofanana nazo.
Kuhusu P Square na Nassib, ikumbukwe kwamba wakati P Square wanakuja nchini wimbo wa Number One Remix wa Nassib alioimba na Davido ulikuwa bado haujatoka, na ndio wimbo ambao kwa kiasi kikubwa ulimtangaza Nassib kwa Nigeria na Africa, hivyo wala haishangazi kusema kuwa hakuwa akimjua.
Kama unakumbuka Nassib alipata nafasi ya kuhudhuria kwenye harusi yao wakati akiwa Nigeria kwa ajili ya kurekodi video ya Number One Remix, na kwa wakati huo Nassib alikuwa akijuana zaidi na akina Iyanya na Davido pekee. Sidhani kama mchonga vinyago wa Tanzania anamjua kila mchonga vinyago wa Nigeria.
Kuhusu kufahamiana, hata Luke Shaw wa Man United alipokuwa akizungumzia na Frank Lampard wa Man City aliweka wazi kuwa hamjui Tonny Adams.
Ova
Me pia love u mingimingiiiiii.
Hehehe usipontaja jina nitapita kama sio mimi vile. Ukomavu ni pamoja na kuvumiliana. Hata hapa jukwaani usipopuuza baadhi ya ishu na kuziacha zipite utajikuta unaagombana hadi na vivuli vya jf.
Karibu nyumbani idris, ngoja nikupe yaliyo jiri while ulikuwa uko mjengoni
1. Wema kaachana na chibu, chibu kajiegesha kwa zari "the boss lady".
2. Kuna ugonjwa mpya wa "tezi dume", unatibiwa marekani tu na unawapata sana sana viongozi wakubwa wa nchi
3. Kama una account Mkombozi ukifika kacheki, unaweza kuwa umepata gawio la escrow. Wengine wamepata mara tatu ya ulioshinda
Welcome back home
Kwahiyo we ulidhani amelengwa nani?? Twende taratibu haina haja ya kuhamaki. Kwanini alivyokua anatukanwa hakuweka clear what he meant?? Kwanini bado ameendelea kupost vitu vile vile mpaka leo?? Hiyo picha anamaanisha nini??
hahaaa kweli kabisa usemayo
umekomaa hasa kiakili ni kazi bure kugombana na anonymous
mi napenda una argue kisomi sana be blessed
Je alimtaja diamond kwenye ile twit? Aliitaja Tz? Mbona mnajibu Kama mko old stone age?? Meen hii ni karne ya 21 hatupaswi kuendeshwa na hisia.
Assume alimlenga diamond....so mtu akikufanyia vibaya na wewe unamjibu kwa ubaya ndo mnavyofundiswa?? Diamond anafanya kazi ya fasihi ambayo inatakiwa ielimishe na iburudishe..... Ndo maana wanaitwa vioo vya jamii kwamba waioneshe jamii wapi pa kurekebisha kwa kuonesha njia. Msanii anatakiwa aiishi kazi yake.
Though ni kweli davido ana dharau lakini kwa hili mmejistukia
Alafu davido alishajulikana bongo hata kabla ya collabo. Kumbuka domo aliongea nae kuhusu collabo alipokuja fiesta.
Unapoongea na watu inabidi ujue ni watu wa aina gani! Sifa ya mtu mzima ni kujiongeza, and this is readers response, mtu anaposoma kitu fulani tunategemea akiilewe vyovyote anavyoweza, Kwanini unakazana kusema diamond kakosea kwanini usianze kumkosoa kwanza davido? Unahisi ni kwanini tusiamini hizi ni chuki za wazi kwa Diamond? ??? Mtu mwenye busara angeanza kumkosoa Davido kwanza ndipo aje kwa Diamond! I am safe to say that Mrembo by Nature hampendi ndomo na hii inathibitishwa na comment zako.
All in all,mie siungi mkono matusi lakini nawashangaa watanzania kwa unafiki wenu!Wageni na watu wa mataifa wengine mnawaona bora kuliko nyie!!Davido hakufanya poa,mi sio shabiki wa dai ila dai ni mtz mwenzangu!Hell no we didn't cheat!so to speak alivo retweet dai ni sawa tu!!Matusi ya wanaija mmeyaona!wanavoponda mmeona?tukemee matusi sio kupindisha tweet ya davido!!Ha we can do better pia!!Go! Go! Tz...hata bila Davido Nassib angefanya poa!!Sipendi urafiki wao uishe ila rafiki yako akikuzingua kisa ni rafiki utakaa kimya kama kondoo?no unampa makavu na urafiki unasonga na adabu ndo inakuwepo sasa!
Kwahiyo we ulidhani amelengwa nani?? Twende taratibu haina haja ya kuhamaki. Kwanini alivyokua anatukanwa hakuweka clear what he meant?? Kwanini bado ameendelea kupost vitu vile vile mpaka leo?? Hiyo picha anamaanisha nini??
Barikiwa pia wewe toto ya mjini
ameeeen
waache watukane dalili ya mpumbavu yeyote ni kuruhusu emotions zitwale busara
yeyote anayetukana tukana hovyoo ni mpumbavu