David Silinde ana mpango wa kuendelea na ubunge?

ouagadougou

Member
Sep 12, 2012
5
1
Nimesoma na David Ernest Silinde mbunge wa mbozi magharibi na mdogo wangu ki-umri

Hivi majuzi nimezungumza na mwananchi mmoja na akanieleza yafuatayo kuhusu Silinde.

1. Hahudhurii vikao vingi vya halmashauri ya wilaya
2. hahudhurii/amehudhuria kikao kimoja tu cha baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma (kwa mujibu wa
maelezo ya mdau huyu Tunduma ni mji wa muhimu sana katika siasa za jimbo la Mbozi Magharibi na alipata
kura nyingi sana zilizomwezesha kushinda jimbo hilo.
3. Aliahidi kuwa na makazi yake Tunduma, jambo ambalo haliko hivyo mpaka sasa na haonyeshi mpango wowote.
4. Si mwepesi wa kurudi jimboni kama alivyo mwepesi wa kwenda nje ya nchi hivi sasa.
5. Hajaanza kuchimba visima vya maji kama alivyoahidi.

na mengineyo mengi ambayo nisingependa kukuchosha kusoma.

kwa haya na mengine kadhaa najiuliza Je mdogo wangu huyu ana mpango wa kuendelea na ubunge katika siku zijazo? Je CHADEMA wanalitambua hili?
 
Nikitu kizuri kuwakumbusha wabunge kutimiza ahadi, kutetea wabunge wasiotimiza wajibu ni kuhujumu CDM
 
Kuwakumbusha muhimu sana,ili wasionekane kuwa na ahadi hewa kama wale wengine
 
Silinde uje tunduma dogo m4c tunaitaka ije huku tuyasemehe haya. Maji ni tatizo huku wajameni.
 
Wewe una uhakika gani na taarifa za kupewa na mdau usiyekuwa na uhakika naye? Fanya utafiti wa kina hata ikiwezekana mshirikishe Mheshimiwa David Silinde mweleze shutuma zote zinazomkabili.Si umesema ni mdogo wako umesoma naye? Au ndio mambo ya kulitaka jimbo yameanza?

Mheshimiwa David Silinde,chonde chonde mara upatapo habari hii tujuze wanajamii ukweli wa mambo.Jamaa tayari wameishaanza kulitolea macho jimbo lako.Siasa mchezo hatari sana!
 
Kama mlisoma pamoja na mdogo kiumri, ni jambo jema kama ukampigia simu na kuongea masuala haya. Jambo unalolifanya ni zuri, lakini njia unayotumia sio sahihi na haumtendei haki mdogo wako. Please mpigie simu
 
Embu mwacheni Silinde wa watu kabisa, hayo yote ni majungu tu, mimi nimekushusha ulivosema haendi jimboni? Muongo mkubwa! huyu kaka kwake dsm napajua na ni nadra kumkuta nyumbani coz anaishi zaidi Tunduma na Mbozi huko, Ukimuona ni 3 days anageuka shamba, sasa mtu afanyaje????

Visima achimbe na nini wkt sirikali haijatoa fungu? Atumie posho yake?
 
Mbona hizo zilikuwa characteristics za LAU MASHA? Umemuona BUNGENI tena? WATU WA MWANZA hawana Mchezo; alikuwa

akienda Mwanza Anakaa kwenye NYUMBA ya BABA YAKE Mzee Fortunatus Masha Mzee Masha ni UDP... LAU akagoma kujenga

MWANZA na WAKAMTUPA
 
Ni kweli Silinde anaweza kujenga hoja na ni mzungumzaji mzuri sana lakini kiutendaji kuna malalamiko mengi. Tunduma watu wanaipenda sana CDM ila Silinde tunaomba utendaji, aliyeleta thread hii ameileta kwa lengo zuri tunapopata jimbo haitakiwi lirudi ccm.
 
Hata kama ni kweli, kwani si bado ana muda?? Hii judgement inakuwa na mashiko zaidi ifikapo Septemba 2015. Mpeni Davie muda apige kazi.
 
Ni mbunge wangu huyu,ila kinachomsaidia ni kwamba wanatunduma ni maadui wakubwa wa ccm,hivyo wapo tayari kukitetea chadema kwa gharama yoyote bila kujali mapungufu ya mbunge wao.!
 
Haya anayo lalamikiwa mbona ni ya kawaida na yanarekebishika pasipo gharama yoyote.kubwa ni hili la visima ambalo nadhani kuwa yeye kama yeye haliwezi bila kusaidiwa.Ajitahidi kujirekebisha.
 
Nafikiri lengo la mleta ni zuri,zaidi waliopo karibu na Mh huyu wamjulishe tuu nafikiri ni kijana makini ataelewa zaidi
 
Haya anayo lalamikiwa mbona ni ya kawaida na yanarekebishika pasipo gharama yoyote.kubwa ni hili la visima ambalo nadhani kuwa yeye kama yeye haliwezi bila kusaidiwa.Ajitahidi kujirekebisha.

Wahenga walisema, "mdharau mwiba, mguu huota tende". Nilipotia nyekundu, panajieleza. Ukidharau dogo, basi litajenga kubwa na mwishowe unajua. Lakini kubwa zaidi, tunataka viongozi na wabunge wa CDM waonakane wakitenda yale wanayoyasimamia. Malengo ya CDM ni kuongoza kwa mfano, ili waTanzania waweze kuwaamini na kuwakabishi nchi. Hivyo, tunaomba Silinde na CDM wayafanyie kazi haya kama sio majungu!
 
Wewe kwa kuwa umesoma naye, nadhani una nafasi nzuri zaidi ya kumshauri kuliko wana JF asiowajua wala wasiomjua kwa karibu!
 
wabunge wote waliahidi sana
ila tumezoa ahadi za CCM kutotekelezwa tunatazamia kuona mabadiliko makubwa kutoka CHADEMA kwamba japo kwa yale madogo yaliyo ndani ya uwezo wao basi tuone utofauti na watangulizi wao ccm

ngoja tuchunguze Mbeya Mjini kwa Sugu kukoji ila na haraka haraka naona ahadi computer 1000 haijatekelezwa
 
Wewe una uhakika gani na taarifa za kupewa na mdau usiyekuwa na uhakika naye? Fanya utafiti wa kina hata ikiwezekana mshirikishe Mheshimiwa David Silinde mweleze shutuma zote zinazomkabili.Si umesema ni mdogo wako umesoma naye? Au ndio mambo ya kulitaka jimbo yameanza?

Mheshimiwa David Silinde,chonde chonde mara upatapo habari hii tujuze wanajamii ukweli wa mambo.Jamaa tayari wameishaanza kulitolea macho jimbo lako.Siasa mchezo hatari sana!
Hii post ina faida kwa mheshimiwa Silinde,ushikwapo shikamana kaka,Tunduma siyo mbali,waone wananchi uwape mipango,
 
Back
Top Bottom