David Nkuba a.k.a Mac D hatunaye tena.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Kwa wale wanaomfahu David Nkuba amefariki leo kwa ajali ya gari ndogo maeneo ya Shinyanga.

David alisoma Azania Secondary, Usagara High School, alipita pia UDSM kidogo na baadae akamalizia masomo yake Chuo Kikuu cha Mysore, India alikosemea Shahada ya Uhandisi na kubobea katika Ectronics na Communications.

David ni Mwanataaluma mzuri wa ICT amefanya kazi makampuni mbali mabli na mpaka mauti inamkuta mwajiri wake ni Chuo Kikuu cha DSM, kitivo cha Informatics and Virtual Eduaction.

Ameacha Mke na mtoto mmoja Melisa. Msiba upo nyumbani kwake Chuo Kikuu, unaingilia gate la Maji kama unatokea Ubungo, unaenda kushoto. Tujitokeze kwa wingi kumfariji mjane na mtoto na kutoa msaada wowote utakaohitajika

Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
POLENI SANA WAFIWA! HUYU ALIKUWAWANAMUZIKI MIAKA IPI, MAANA KUNA MAC DEE MWINGINE ALIKUWA MWANAMZIKI WA BONGO FLAVA KWENYE EARLY 2000s NA ANAISHI MAENEO YA KARAKATA, AIRPORT NA HUYU HANA SIFA HIZO ZA ELIMU KAMA ULIVYOELEZA
 
RIP brother. ww umetangulia na sisi tupo nyuma yako,
 
Tukumbushie mwimbo wake hata mmoja aliowahi kuimba maana hayo ndo madhara ya kujiita a.k.a kwa wasanii wate wa bongo.Anyway poleni wote jaman
 
Ujumbe huu hapa chini ni kutoka kwa mdogo wake.

Nimepokea kwa masiitiko makubwa kifo cha kaka yangu David Nkuba ambae aliondoka asubuhi ya leo akiwa na mjomba wetu Moses Nkuba kuelekea Shinyanga na walipofika Dodoma walimpitia mjomba wetu Maj .Emmanuel Nkuba ,walipofika Singida walipata ajari na yy kaka yangu pamoja na mjomba Maj Emmanuel Nkuba wamefariki kwenye ajari hiyo.

Mr Joseph Nkuba ndio anashughulikia mipango ya mazishi ambayo yatafanyika Shinyanga Maswa kwa mawasiliano zaidi ,no za simu za kaka joseph Nkuba ni 0784 3052 72 | 0763 163211

Pumzikeni kwa amani David Nkuba na Emmanuel Nkuba

Ndimi mdogo wake
Fortunatus Nkuba
0787230056
 
Kwa mara nyingine tena ajali imemchukua mmoja wetu! Apumzishwe mahali pema, amina
 
Back
Top Bottom