Eddo mkweli
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 475
- 37
Habari zilizotufikia hivi punde.
Aliyekuwa katibu wa wizara ya nishati na madini na baadae kufukuzwa kwa tuhuma za Ufisadi na kuhalamisha mchakato wa upitishaji wa Bajeti ya wizara ya Nishati na Madini Ndugu David Kitundu Jairo anashikiliwa na TAKUKURU wilayani Iramba kwa tuhuma za kugawa Fedha wakati huu wa mchakato wa kura za Maoni.
Jairo ni mgombea wa Ubunge kati ya watu wa nne waliojitokeza akiwamo Amon,Mwigulu na Kilimba.
Jairo anatuhumiwa kusambaza fedha tsh.30000 kwa kila balozi na makatibu wa Matawi ya CCM katika vijiji mbalimbali akiwamo Ujungu,Mtekente,Mtoa,Msai n.k
Ni takribani masaa 2 sasa anashikiliwa katika ofisi hizo za Takukuru wilayani Iramba,hatua za kumfikisha mahakamani kwa kujibu tuhuma hizo.