David Kafulila: Ni njia ngumu lakini ndio njia pekee!

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Taifa linajengwa na watu wakiwa na tamaduni zao ndani ya nchi yenye mipaka inayotambulika kimataifa. Nchi ni ileile lakn Taifa linaishi na kukua! Watu hawa wanaounda Taifa wanajiwekea taratibu zao za kujiendesha ambazo huziita Katiba na Sheria kwa ajili ya kukua na zaidi UHAI wa Taifa lao.

Katiba na Sheria ndio Mkataba kati ya wanaopewa dhamana kutawala na wale wanaotawaliwa. Inakuwa hivi ili kila binadamu wa Taifa hilo awe na HAKIKA ya maisha yake mwenyewe na Taifa lake.

...Nchi ni mali ya Taifa husika sio mali ya Kiongozi. Majaaliwa ya watu na Taifa lao yanapaswa kubaki ndani ya Katiba na Sheria na sio kuhamia kwenye mkono wala kichwa cha Kiongozi. Ukuu wa Katiba unapaswa kuwa juu ya kila kitu na kila mtu. Ni hatari sana kuwa na kiongozi mwenye matendo yanayokuwa juu ya UKUU WA KATIBA.

Ndio kusema Rais ni mtumishi wa Umma. na kwasababu hiyo ni mlinzi wa Nchi na Taifa lake.Na anafanya kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba. ambao ni Katiba na Sheria. Ndio sababu Rais kabla hajaanza kazi anaapishwa Kuilinda na Kuitetea Katiba.

Kwa kauli zake Rais wetu nikama hakuelewa mkataba aliosaini kwamba ni yeye kuwa mlinzi wa nchi sio mmiliki wa nchi. Angejua kuwa sisi ndio wenye nchi na yeye ni mlinzi angetamani kutusikiliza.lakn kwakuwa alielewa tofauti au anakusudi la kuvunja mkataba haoni sababu ya kutusikiliza kwani anahisi nchi ni mali yake wakati ni mali yetu.

Lakn tunamkumbushaje huyu mtu tuliyempa kazi ya ulinzi sasa amejigeuza mmiliki wa mali? Tunafanya nini kama wenye nchi dhidi ya huyu mlinzi wa nchi inapoamua kuvunja mkataba kibabe na kwa mabavu na jeuri?

Hatua za kuchukua zinategemea kiwango chetu cha ufahamu kuhusu dhana ya wananchi kama wenye nchi na Rais kama mlinzi wa Nchi. Tunaweza kubaki kulalamika na kulia kama mateka kwasababu mlinzi ana silaha na vyombo vya ulinzi. Tunaweza kukataa kuwa mateka na kuikomboa nchi yetu kwasababu silaha alizonazo ni mali yetu tulimkabidhi kama mlinzi wetu. KUPANGA NI KUCHAGUA. Kuna njia nyingi za kukataa kuwa Mateka, Wananchi wote wakatae utawala huu unaokanyaga Katiba na sheria, Wasomi watujengee uwezo wa kukataa utawala usio heshimu Katiba, Viongozi wa dini Wahubiri injiri ya kukataa Utawala unaovunja Katiba, Wanahabari wazidi kukataa , Bunge kama Muhimili uiwajibishe Serikali hii iaioheshimu Katiba na Mahakama Isimamie kuhakikisha sheria hazinajisiwi na mtawala yeyote. Kila mmoja wetu kwa nafasi yake akisimama na kutimiza wajibu wake, Mlinzi wetu ama atatambua nafasi yake kuwa ni mlinzi na sio mwenye mali au Atatoroka tuweke mlinzi mwenye adabu na Katiba, na kutoka hapo uwe mwanzo mpya wa kudai upya Katiba sahihi kwani tuliyonayo inampa mamlaka mlinzi kiasi cha kutupuuza wenye nchi.
 
Nasubiri wale wasomi waliochaguana kule arusha wanaoaminika kuijua katiba kuliko sisi wengine wataisaidiaje "tanganyika" yao.

Ni kweli tunataka huyu mlinzi atupishe maana hajitambui. Tena nadhani hata hajitambui kuwa kuwa yeye ni wa jinsia gani.

Eti "sipangiwi cha kufanya"
 
Nasubiri wale wasomi waliochaguana kule arusha wanaoaminika kuijua katiba kuliko sisi wengine wataisaidiaje "tanganyika" yao.

Ni kweli tunataka huyu mlinzi atupishe maana hajitambui. Tena nadhani hata hajitambui kuwa kuwa yeye ni wa jinsia gani.

Eti "sipangiwi cha kufanya"
Well said tuendelee kusubiri
 
Nasubiri wale wasomi waliochaguana kule arusha wanaoaminika kuijua katiba kuliko sisi wengine wataisaidiaje "tanganyika" yao.

Ni kweli tunataka huyu mlinzi atupishe maana hajitambui. Tena nadhani hata hajitambui kuwa kuwa yeye ni wa jinsia gani.

Eti "sipangiwi cha kufanya"
munajichosha mno hawpishi ngo na 2020 anapita tu kama hutaki nenda kenya
 
Tunataka Mchakato wa Katiba Mpya uendelee na yawekwe masuala yote wananchi waliyoyapendekeza na isiwe Katiba yenye maslahi kwa watawala. Mchakato mpya ukianza tunataka wahumbe wa Katiba Mpya wachaguliwe kwa usawa na sio kujaza wajumbe wa Chama kimoja tu cha siasa, hii itakuwa ni KIINI MACHO!
 
Back
Top Bottom