JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,661
- 6,395
TAARIFA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TABIA MBAYA ZINAZOHATARISHA USALAMA WA MAISHA YA WATANZANIA NA MALI ZAO
Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa, kuwaombeni kwanza; muisaidie Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuwataarifu Watanzania wote na kuwaomba sisi sote tushirikiane kuunga mkono kwa dhati Rais wetu Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kukomesha tabia mbaya zilizozuka katika Taifa letu za kulawiti, kuteka, kunyanyasa na kuua Watanzania wenzetu.
Pili: kupendekeza kwa Watanzania wote, wananchi na viongozi, kukubali kwamba Taifa letu si la wauaji wala la wahuni, ni Taifa la watu wanaoishi kwa kuzingatia Katiba ya nchi yetu na sheria zinazotokana na Katiba hiyo sisi sote tunao wajibu wa kufuata na kutii Katiba yetu na sheria zote zinazotokana Katiba hiyo, na ambazo hazikiuki Katiba. Hakuna nafasi wala ruhusa kwa raia yoyote wa nchi hii kuishi nje ya utaratibu huu. Huu ndio msingi wa amani, umoja, na maendeleo yanayo shirikisha wananchi wote kwa faida yao. Kwa maana hii, sisi Watanzania ni wastaarabu.
Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue. Kwahiyo Taasisi ya Mwalimu Nyerere inaomba tumsaidie Rais kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hao ili achukue hatua stahili. Anavyo vyombo vya dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpa taarifa za uhakika. Nchi yetu imeviwezesha kuwa na uwezo wa kutosha wa utaalamu na