David Kafulila; Huu ni mtazamo wake kuhusu sakata la kumvua unaibu katibu CHADEMA Zitto

Sawa ila mwambie Zitto afuate taratibu za chama ktk kugombea uongozi,kupitisha vikaratasi chini kwa chini kabla ya mchakato huo ni dhambi!lazima uelewe kama huna ndoa kufanya tendo lile ni dhambi kubwa,ila kama una ndoa halali unakua unatimiza ibada.Pia jiulize Dr.Kitila mzima hakujiona yeye anafaa kuwa mwenyekiti mpaka anampigia debe Zitto kiasi kile huku zitto anajifanya hautambui waraka hajauona!pia bado wanakataa kumtaja M2, hawa watu kweli wana akili timamu au ni robot wanatumwa tuu?

Hakuna ambaye ajaanza mikakati Si Mbowe wala Zitto... Wote wanamikakati yao... Tofauti iliyopo Mbowe Mwenyekiti wa Chama, Zitto mwanachama wa kawaida. Waraka ulikuwa wa siri umesambazwa na Team Mbowe... Aliyeusambaza kakitia chama kwenye msuguano.
 
mungu iangamize milele chadema, inanuka damu na roho za watz iliowauwa. rest in peace chacha wangwe
 
mods, tafadhali, naona mleta mada amekosea kwenye heading, tafadhali rekebisheni isomeke kafulila sio kafulika

cc.

mods wote - invisible, buchanan, fang, melo
 
David, sikubaliani na wewe hata kidogo. Although in the general sense, una pointi.

Nadhani ZZK ni rafiki yako sana wa hali na mali. Kumtetea ni jambo tunalilitegemea kutoka kwako.

Issue ya kijana Zitto iko kwenye matatizo yake kama kiongozi wa chadema. Vikundi vya siri si afya kwenye demokrasia ya kweli. Wenyewe Chadema wamesema kuwa wana utaratibu wao inapotokea mtu anataka kugombea kutokana na matatizo mengi huko nyuma. Zitto na wengine wote wanatakiwa kufuata taratibu za chama.

Akili ya kawaida kabisa inaonyesha Zitto alijua kuhusu waraka na amedanganya CC kuwa haufahamu. Yeye na Kitila ni marafiki wakubwa na wako close. Haiwezekani aandike maparagraph yote hayo bila rafiki yake kujua.

Ebu tueleze kama huko nccr mtu hafuati kanuni na taratibu za chama, haaminiki na yuko na misimamo inayotia shaka pamoja na maonyo na vikao vya kumrekebisha mngemuacha tu?! Kuna collective responsibility, mnapoamua pamoja mnatekeleza kwa pamoja mambo mbalimbali ya chama, ila huyu zitto pamoja na Shibuda wana mtazamo tofauti, kisingizio... eti demokrasia.

Hata kitendo cha mashabiki wa chama changu CCM kushabikia ishu ya zitto haimsaidii bali inazidi kuthibitisha mashaka ya watu wa chadema dhidi yake. Iweje sie CCM tumtetee mtu wa Chadema kwa nguvu ivyo? Sie kama CCM tunafaidi kwa kuwa tu zitto akiondoka anaacha gap na ni kete ya kisiasa kuwa wale chadema wanasambaratika au wanafukuzana!

Sisi kama CCM tunatakiwa tujikite kwenye philosophy yetu, tuaddress mapungufu yetu na sio kuhangaika na chadema kila uchwao. Tunatumia gharama nyingi kuhangaika na hawa CDM kwa hoja za kipuuzi kabisa. Kuna issues za umeme, umasikini, elimu, healthcare nk tukihangaika nazo na kuziaddress tutazidi kupendwa na wananchi daima.

Mimi Critical KADA

maggid alisema kuwa CCM hawawezi kupenda Upinzani especially chadema ambao wanahatarisha uwepo wao madarakani. Kwahiyo Kama kuna mivutano ndani ya Upinzani lazima CCM watachochea kuni, ukiwa ni pamoja na kumpa support! Hebu jiulize kama Leo Zitto atachukua uenyekiti CDM, CCM watendelea kumpa shavu?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza David Kafulila fahamu kwamba hakuna ugomvi kati ya Mbowe na Zitto.Bali kuna ugomvi kati ya Zitto na Chadema.

Mbowe hana mamlaka kutengua maamuzi ya Kamati kuu.Na Mbowe endapo kama atarudi nyuma katika hili hatutamvumilia....
 
Natambua hayo ni mawazo yake lakini tunapaswa kukataa kabisa hili swala la kuwapatia watu uongozi kwa kigezo cha sehemu wanazotoka ni siasa chafu na mbaya ambazo tukiziruhusu zinaweza kuligawa taifa vipande vipande.Ebu fikiria akitokea kiongozi mzuri wilaya ya Bagamoyo tumkatae kwasababu Rais wa sasa anatokea huko !.


Mkuu Ngongo hayo ni mawazo yake na ni haki yake kama vile wewe ulivyokuwa na haki na kuwaamini hao mabwana wakubwa.
 
Huyu ni mpiga debe wa Zitto hana lolote nilimdharau wakati ule aliposema ndani ya bunge sasa ni zamu ya mkoa wa Kigoma kutoa rais wa Tanzania.

kigoma mna udhaifu, jisahihisheni.
Hata hapa katika bandiko hili la kafulila naona udhaifu ule ule. Ukisoma andiko hili la kafulila hapo mwanzo kabisa kuna ukigoma tu na kwamba yeye anatazama suala la zzk kama ni ugomvi binafsi wa mbowe na zzk hata kama maamuzi ya kumvua zzk uongozi yametokana na cc ya chadema. Hili ni tatizo kubwa linaloweza kupelekea cc isifanye kazi yake barabara kwa sababu kuna watu wanachukulia ni ugomvi binafsi. Hii isipewe nafasi.
 
Kafulila wewe ni sisimizi,mmeondoka kibao CDM lakin ndio inazidi kupaa kumbuka CDM sio mtu ni taasisi,kufukuzwa kwa ZZK ndani ya cdm hakutoathiri chama hata kidogo bali ndio kitazidi kusonga mbele maana muhaini na yuda atakua ameondoka!!
 
Kwanza David Kafulila fahamu kwamba hakuna ugomvi kati ya Mbowe na Zitto.Bali kuna ugomvi kati ya Zitto na Chadema.

Mbowe hana mamlaka kutengua maamuzi ya Kamati kuu.Na Mbowe endapo kama atarudi nyuma katika hili hatutamvumilia....

Mbowe .. mwenyekiti Vs Zitto Mwanachama wa kawaida....
 
hakuna namna yoyote ya zitto kubaki chadema , atafukuzwa bila shaka yoyote ( bali atapiga sana kelele ili kuwafurahisha waliomtuma , kama tunavyotarajia ) lakini cdm itasonga mbele .
 
Kafulila baada ya kupokwa ubunge na MBATIA akawa mbunge wa COURT then kaenda kuwalilia PANYA kule kigoma,kalia mpaka machozi na kumwangukia mbatia then akasamehewa ila KAPUNGUZA KIHEREHERE.ana ugonjwa uitwao Zittophobia

nADHANI ZITO ILE APPROCAH NI YA KIHUNI KABUGI STEP. nO cREDIBILITY AT ALL. aKALIME MAWESE SASA.
 


David Kafulila


KINACHOTOKEA CHADEMA ni Changamoto za ukuaji wa demokrasia...na ndio Chama kinapumua...bado naamini mbowe na zitto wanaweza kumaliza tofauti zao na wakatoka pamoja wakiwa imara zaidi Kama Chama kwa maslahi ya demokrasia ya ushindani nchini. Najua wanajuana kuliko tunavowajua sisi, TUWAPATIE nafasi. Naamini wanatambua hasara ya kusambaratisha upinzani nchini.

Kufukuzana kwenye Chama sio sifa Bali woga..kukabiliana kwenye Chama ndio sifa kuu isiyoepukika kwa Chama kinachokua na chenye uhai. Hakuna Chama kulichofukuzana na kuimarika.vyote vilivyofanya hivyo vilisinyaa..naamini vikao vya juu vya CHADEMA vitabatilisha maamuzi ya kamati kuu yake. Watambue kuwa CHADEMA ikifa Leo itachukua sio chini ya miaka10 kujenga up ya Imani ya umma kwa upinzani.

Hivyo watazame kwa mapana wakitambua kuwa hakuna Chama hai duniani ambacho HAKINA mapambano ya ndani( internal struggle), ndio uhai wa Chama, Chama kilichokufa hakiwezi kuwa na mapambano ya ndani, ndio maana siamini Kama kuwa na mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya Chama ni uhujumu au dhambi kwa Chama Bali ustawi.

Ndio maana ni wajibu wa Chama makini kiwe na mfumo wa kukabili migogoro ya ndani isipitilize kuhatarisha uhai lakn iwepo kwajili ya uhai aw Chama kwasababu isipokuwepo hakitakuwa Chama Bali magereza ya kisiasa. Hivyo Ndivyo nionavyo Mimi Kafulila.

Vipi ANC walipomfukuza Julius Malema, chama kimesinyaa? Unadhani Nguvu ya Malema ANC na ya Zitto CDM ipi kubwa?sio kwa kuwa kiongozi basi lazima u-spit out, kama una maelezo yenye mashiko, kaa kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Back
Top Bottom