Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,077
- 1,439
Ni January 28, 2016 Mkuu. Hiyo ni kesi ya Ubunge ktk uchaguzi wa Oktoba 2015.mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
Mkuu umetishaIkishinda CCM Zanzibar uchaguzi ulikuwa wa haki na huru,ikishinda CUF kura ziliibiwa
Shauri hilo litaendelea tarehe 28 kipi usichoelewamie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
Hii ni kesi ya kikatibaHivi ukiwa ukiwa mbunge wa ccm unasimamiwa na mwanasheria kutoka serikalini ila ukiwa upinzani unatafuta mwanasheria wako kwani hii kesi ni juu ya kafulila na tume ya uchaguzi au ni kesi ya kafulila na mgombea wa ccm naomba kusaidiwa wanajamii
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2016 katika mahakama hiyo.
Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;
- Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
- Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
- Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria
Katika uamuzi wa Mahakama, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
- Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.
- Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.
- Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, Mahakama imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo
Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2016.
Nimekupenda bure nifahKafulila akishinda hii kesi atanipunguzia machungu ya uchaguzi mkuu kwa 50%
Kila la kheri.
mie naomba mnisaidie sijaelewa vizuri jamani. kwamba kesi kuendelea kusikilizwa January 28/2015? hii ilikuwa kesi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014? na sasa kesi yake tayari ilisikilizwa January 28/2015 kwani Kafulila alikuwa anamtetea mwekiti nani wa serikali za mitaa ambaye ccm walimchakachua, je maamuzi yaliendaje. vinginevyo sijaelewa hiyo January 28/2015 mleta maada anamaanisha nini.
Kafulila akishinda hii kesi atanipunguzia machungu ya uchaguzi mkuu kwa 50%
Kila la kheri.