DAS Nyamagana, Afisa Mtendaji Pamba, Diwani Chadema wapiga Tsh. Milioni 45 za shule

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
DAS Nyamagana, Afisa Mtendaji Pamba, Diwani Chadema wapiga Tsh. Milioni 45 za shule ya Pamba

Pesa hizo zinatokana na kuuza eneo la wazi la shule kwa wafanyabiashara wakubwa

Katibu Tawala wilaya ya Nyamagana, Yonas Alfred, Afisa Mtendaji wa kata ya Pamba Jonas Mugisha na Diwani wa Kata ya Nyamanoro, Abubakar Kapera wanashirikiana kuuza eneo la shule ya sekondari Pamba kwa wafanyabiashara wakubwa jijini Mwanza.

Wafanyabiashara wanaouziwa eneo la shule hiyo ni wale ambao walikuwa na maduka katika soko kuu la Mwanza na wale waliokuwa jengo la Mwadeco.

DAS huyo na wenzake wanauza eneo hilo la shule ambalo lipo mbele ya geti la kuingia na kutoka shuleni hapo kwa wafanyabiashara ambao huingiza kontena hizo nyakati za usiku.

Jinsi wanavyouza eneo hilo ni kwamba wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa wanauziwa eneo kuanzia Tsh. Milioni tatu hadi sita ili waweke makontena.

Wengine wanaoweka vibanda vidogo vya chuma wanauziwa kuanzia Tsh. Milioni moja hadi milioni Tatu kitendo ambacho wafanyabiashara wengine wameanza kugoma na kuomba kurudishiwa pesa zao.

Kontena kubwa ambazo zimewekwa eneo hilo la shule ya sekondari ya pamba zipo kontena sita huku vibanda vidogo vya chuma vipo 20.

Kwa hesabu za kawaida kontena hizo zote sita, zimeingiza kiasi cha Tsh. Milioni 20 huku vibanda vidogo vimeingiza Tsh. Milioni 25.

Jumla ya pesa zote ni Tsh. Milioni 45 ambazo zimeingia mifukoni mwa watu hao watatu licha ya watu wengine wakifichwa ambao ni mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, Mwanasheria wa Jiji Bi. Maliam na Afisa biashara wa Jiji.

Kutokana na wafanyabiashara hao kuvamia eneo hilo na kuweka makontena yao kwa usaidizi mkubwa wa viongozi hao, taarifa zinasema tayari bodi ya shule ya Pamba imekutana.

Bodi hiyo ya Pamba imekutana jana na leo na kufanya kikao, wakihoji kwanini eneo lao la shule kuvamiwa na wafanyabiashara bila kushirikishwa na kwamba eneo hilo limekuwa likitumiwa na wanafunzi katika shughuli mbalimbali.

Bodi hiyo inadai kwamba kabla ya kukutana walipeleka malalamiko yao kwa mkurugenzi wa Jiji la Mwanza lakini hakuna hatua zozote ambazo zilichukuliwa na kuwalazimu kuandika barua kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Bodi hiyo inasema barua ambayo imeandikwa kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, pia itaandikwa nyingne kwenda ngazi ya kitaifa kwa msaada zaidi.


Picha za kontena zilizowekwa hapo Pamba.

IMG20191016105704.jpg
IMG20191016105726.jpg
 
Huyo Kapera ni mzee wa mjini, yeye na mtendaji ndio wenye dili Hilo.

Diwani + Mtendaji ni wahaya, ameingia kutokana na ukabila wao na diwani ndiye anamfundisha upigaji.

Huyo diwani wa Nyamanoro kwenye kata ya Pamba anaingiaje hapo? Tufafanulie vizuri tafadhali
 
Hivi unajua huyo DAS ni ndugu yake nani?
wee haya weee!
Uliza wenyeji wako, utajua huyo dogo ni ndugu yake nani?
๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ
 
Hivi unajua huyo DAS ni ndugu yake nani?
wee haya weee!
Uliza wenyeji wako, utajua huyo dogo ni ndugu yake nani?
๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ๐Ÿƒโ€โ™€๏ธ

Acha uoga wewe, tufumbie macho wizi kisa ya undugu na na ni hii??
 
Hushangai dogo hata kazi hawezi lakini wakubwa wote wanaogopa kumsema, halafu ni ka nyanyasaji kwa watumishi warembo, bado kana ushamba wa kutaka Kei kwa kutumia madaraka yake.
Acha uoga wewe, tufumbie macho wizi kisa ya undugu na na ni hii??
 
Mleta mada umepania ukute mmechengana kwenye madili yenu huko then ukawambia ngoja dunia itajua kwamba umeiba
 
Hapo skuli ilipo kuna pilika nyingi za biashara. Sioni sababu ya hiyo shule kuendelea kuwapo hapo. Mazingira sio Rafiki tena kujifunzia na pashabana sana.
Halmashauri husika itafute eneo lingine hapo wapauze au wapafanye open space/ bustani.
 
Back
Top Bottom