Darweshi ni nani?

Laiti sote tungeijua kazi aloifanya muhammad abdulwahhab naamini tungemkubali sana, tatizo sisi ni wavivu wa kutafuta ilmu na hata kwenda kusikiliza darsa kwa watu wa haki hatutaki tumekuwa watu wa kusambaza maneno ya propaganda na chuki dhidi ya watu wema.
Allah tuongoze sote.
 
Mkuu hicho kijiji kilikua kinaitwaje,na hiyo jela aliokua anashikiliwa ni ipi maana zote zina majina.mh!sisimizi akifanya tukio la ajabu kila mtu atajua eneo la tukio na jina lake.hizi ni story za kufikirika tu kama zile hadithi za vikapu vikarukaruka huku mawe yakiwa yanashangilia kwa furaha..
 
Mkuu ongezea na Babu wa Loliondo
 
Mimi nishamsoma Darwesh mwingine kabisa aliyekuwa kwenye kile kikosi kazi kilishiriki katika mapinduzi ya zenjbar darwesh alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kikamilifu kufanikisha mapinduzi hayo.
Historia inamtaja kama mtu kutoka Mtwara sasa sijui kama ndiye au?
 
Ma
Kuna mmoja alivuma miaka ya 90 kama mganga alikuwa akitibu ukimwi. Aliishi moshi maeneo ya dsm street jina lake kamili lilikuwa:shaaban darweshi .. Sijui ndo mwenyewe??
Mama Shaban darwesh alikuwa mganga na full ninja
 
Naona humu wamejazana madaruweshi tu


Maendeleo hayana chama
 
na wewe ukaamini kuwa anaenda makka kwa dakika? kweli akili ni kimiminika wengine zimevuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha porojo wewe aliyeenda hijja Makkah hawezi andika uchafu huu acha unafiki
 
Darwesh kimuktadha tajwa ni mwanadini aliejaliwa kutangaza dini lakini elimu yake ni ndogo kwa maana anayoyasema ni sahihi lakini hajuwi yanapatikana aya gani au sura gani.
Kuswali mnaleke ni jina la kupewa likiwa na maana Kuswali msiache (makonde) ndugu huyu bado yu hai kwa mara ya mwisho nilimuona 2010 lakini ni mzee hasa kwani uwezo wa kuongeaa upo chini mno.
kajaaliwa uwezo mkubwa ambao wengi waliombishia waliumia na waliathirika kama Pharaoh kwa Mussa(Maji), hii ilitokana na dua zake zilikuwa zinakubaliwa kwa haraka mno Allah SW hivyo kama ni - basi mtaona majabu yake(wenye kuamini).
kuhusu kupaa-inaamkinika kuwa enzi za ujana wake alikuwa mtembeaji mzuri sana pasi kuwa na usafiri hivyo alitembea kwa miguu, lift au kupaa. kuna mikasa kadhaa ya kunyimwa lift na gari lakini akakutwa mbele ya safari mf Dar-Mtwara endapo yupo mtwara asubuhi sio ajabu kumkuta jioni Dar bila kutumia usafiri wowote. unatoka Dar unaenda Dom ye anajuwa kuwa unaenda wapi so hukufuata na kuomba lift ya Moro tu(private car) kama ukikataa unaweza mkuta Moro na lazima aje akusalimie ili akusute uache roho mbaya.
Hija-katika umri wake wa nguvu alienda hija kila mwaka i.e zaidi ya mara 33 ni Mtanzania pekee kufikisha idadi hiyo.
wanamtwara wanaamini maafa yaliyotokea vijiji 2 Mwena(Ndanda) hapa ni mafuriko na Chiwindi huko Newala hapa ni mashimo makubwa yaliyotokana na mvua za kawaida tu. wahenga wanaamini kauli za kejeli na kabehi (bangi hizo, chizi huyoo, njaa hiyo ) za vijana enzi hizo juu ya mtu huyu ambae alitembela vijiji hivyo kutoa neno vilipelekea kukasirika na kuomba dua mbaya iliyodhuru maeneo na watu wake.
ni kwa wenye imani tu maana hata Firauni hakuamini hadi alipomuona papa anakuja kumla
 
wacha dharau dogo usidhanie hatujui maana fasaha ya daweshi ni 'mtakatifu' we wahabi nini?
,kaka Dulla usipaniki,hiyo ndio maana yake,Darweshi kiarabu ni jumba tupu lisilo na jambo,na jina hili walikuwa wakijipa baadhi ya wasomi wa zamani wachamungu walioipa nyongo dunia,pamoja na kuwa na elimu kubwa na utukufu wao mbele ya jamii walikuwa wakihiita kuwa ni darweish yaani pangu pakavu,kwa unyenyekevu,badala yake ule upangu pakavu wa jina lenyewe ukaja kugeuka utukufu kwa sababu ya uhalisia wa utukufu ya wabebaji wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah wewe utakua umeishi Moshi na umeaoma Muungano Primary hahahha


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mimi nimeishiwa Ms 85-99 nimesoma Mawenzi ps, Mawenzi sec then old Ms sec adv huyu mwanae mama darwesh nakumbuka tukiwa njuka alikuwa form 3 watata alikuwa anakuja shule na farasi au tractor ikivuta tela yake ilikuwa burudani ligi zake na walimu shuleni pale
 
Reactions: T11
Ebu tupe ukweli japo kidogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…