Simulizi fupi ya kusisimua ya Jestina

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
8,799
8,706
JESTINA-1

"Jestina....Jestina....Jestina...tafadhali usifunge macho eeeh mungu usimchukue Jestina wangu nitabaki na nani hapa duniani" hiyo ilikuwa ni sauti ya kijana Alwin akiwa amempakata katika mapaja yake mschana aliekuwa akimpenda zaidi kuliko kitu kingine chochote duniani.

Wakati huo Jestina alikua akivuja damu maeneo kadhaa katika mwili wake. "Alwin kwanini unanipenda kiasi chote hicho na wakatii nilishaakwambia zamani kuwa sina hisia za kimapenzi juu yako" Jestina aliongea japo kwa tabu sana. "Jestina kukupenda mimi haikuwa na maana na wewe unipende, penzi la upande mmoja lilitosha kabisa kuishi na wewe" Alwin aliendelea kuongea huku machozi yakimchuruzika ka maji machoni mwake.

"Alwin nakuomba unyamaze na uniache nipumzike kwa amani, nakuahidi kuwa nitazaliwa tena kwa ajili yako iwe katika maisha haya au yoyote yale..... tafadhali niache niende kwa amani" alimaliza kuongea maneno hayo na kukaa kimya, Alwin alijaribu kumtingisha lakini hakushtuka, alipeleka kidole kwenye pua na hapo ndio akagundua kuwa tayari Jestina alishaamuacha peke yake duniani. "no...n.o...no ple...ase Jestina...Jestina... Jestinaaaaaa" alipiga kelele na papo hapoa akapoteza fahamu.

***********

Mwaka 1993 katika mji wa Mashvile, iliskika sauti ya mwanamke akipiga kelele za uchungu. "sukuma..jitahidi mama mtoto kashafika mlangoni" hiyo ilikuwa ni sauti ya daktari aliekuwa akimzalisha mama huyo. Sekunde kadhaa baadae iliskika sauti ya kichanga kikilia, "hongera bwana Hendrix umepata mtoto wa kike" alitoka daktari na kumpasha habari hizo mume wa mama aliekua akijifungua. "naruhusiwa kuingia" aliuliza bwana Hendrix kwa furaha sana, "ndio" dokta alijibu na bila kuchelewa alipita na moja kwa moja alielekea kitandani alipokuwa mkewe.

"pole mke wangu" aliongea kwa bashasha na kumbusu mkewe katika paji la uso, "naweza kumbeba mwanangu" aliuliza bwana Hendrix, "ndio" alijibu nesi mmoja, basi nae bila kuchelewa alimchukua mtoto huyo kutoka mikoni mwa mkew na kumbeba. Kwa kweli siku hiyo ilikuwa ni siku nzuri sana kwa familia hiyo ya kitajiri.

Hiyo imetokana na kuwa, ni miaka mingi sana wameishi katika ndoa bila kupata mtoto japo walipata misukosuko kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini wao hawakujali waliamini siku zote mtoto ni riziki kutoka kwa Mungu. Basi baada kukamilika taratibu zote waliruhusiwa kurudi nyumbani, walitoka hospitalini na kuingia wene gari na kuondoka.

Njia nzima kila mmoja alikuwa kimya akitafakari ni jina gani ampe mtoto wao, walikuja kushtuka baada dereva aliekuwa akiwaendesha kuwaambia kuwa tayari washafika nyumbani.

Wafanya kazi wote walikuwa nje wakiwassubiri kwa hamu, waliposhuka tu kwenye gari watu walipiga vigelegele na kuwakaribisha ndani. Kwa vile walikuwa wamechoka sana waliekee chumbani kwao na kupumzika. Siku ya pili mapema asubuhi waliamka na kushuka chini, walishangaa kukuta kumebadilika sana, kwenye meza kulikuwa na keki kubwa ilioandikwa "Welcome to the world little princess".

Ukweli nyumba hiyo ilijaa furaha kupita maelezo, na hiyo ilitokana pia na ukarimu wa matajiri hao kwa wafanya kazi. Kiufupi hawakuwachkulia kama ni wafanya kazi bali ni kama ndugu zao tu.

Siku kadhaa zilipita na muda wa kumpa jina ulifika, hapo sasa kukawa na mshikemshike maana wafanya kazi wa kike walikuwa wakimsapoti mama na wafanya kazi wa kiume walikuwa wakimsapoti baba. "Bora aitwe Jessey" huyo alikuwa ni bwana Hendrix, "bora tumuite Christina" na huyo alikuwa ni mke wake, mdahalo huo uliendelea kwa muda mrefu bila kupata jibu mpaka iliposkika sauti yenye kukwaruza ikisema "kwanini msimuite Jestina, Jes kutoka Jessey na Tina kutoka christina", "lakini kweli hapo itakuwa vizuri maana atakuwa na jina alilochaguliwa na baba yake na mama yake pia" wote walikubali na kumuita mtoto wao "JESTINA".

"Prisca mama yangu kwanini usiache tena kufanya kazi maana umri ushakwenda sana" Mr Hendrix alimuita na kumueleza hayo mfanya kazi huyo ambae alikuwa akimheshimu kama mama yake maana ndie aliemlea tokea wazazi wake wapo hai mpaka wamekufa na ndie anaejua ni kwa jinsi gani utajiri huo umepatikana "mwanangu Hendrix kama nitaacha kufanya kazi nitapata wapi pesa ya kula" aliongea mwanamke huyo alienekana kuzeeka na umri wake ulikuwa ni kati ya miaka sabini hadi sabini na tano.

"Sijamaanisha uondoke hapa, hapa wewe ni kwako na mpaka mwisho wa maisha yako utaendelea kuishi hapa. Ninachomaanisha ni kwamba uache kufanya kazi tu kula utakula na mahitaji yako yote nitakupatia"Aliongea Hendrix na kumkumbatia bibi huyo ambae alimpenda kupita kiasi. "kama ni hivo sawa ila naomba kitu kimoja tu, niwe nacheza Jestina" aliongea bibi huyo huku machozi yakimtoka jambo ambalo Hendrix alilikubali kwa mikono miwili.

Baada ya hapo aliamuru chumba cha Jestina kiongezwe kitanda kimoja kikubwa kwa ajili ya Prisca na kazi hiyo ilifanyika siku hiyohiyo kisha kila kitu cha bibi huyo kikahamishiwa chumbani huko. Ukweli bibi huyo alikuwa akimpenda sana Jestina na yeye ndie alieshauri kuwa mtoto huyo aitwe Jestina.

Jestina alikuja na baraka ndani ya nyumba hio, maana mambo mengi yalikaa sawa huku bishara zikinawiri. Maka ilisogea na hatimae ilifika siku ya kusheherekea kuzaliwa kwa Jestina akiwa anatimiza miaka mitatu, watu wengi sana walialikwa katka sherehe hiyo. "mke wangu fanya haraka tushachelewa" mzee Kelvin alikua akimharakisha mkewe ili wawahi kwenye sherehe. "nishamaliza mume wangu nakuja" alijibu mkewe huku akitoka na mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka minne akiwa amembeba.

Waliwasha gari na kuelekea katika sherehe, na kwasababu hakukuwa mbali, walitumia dakika tano tu mpaka kufika, walishuka kwebye gari na kuelekea ukumbini. "karibu Mr na Mrs Kelvin" aliongea Mr Hendrix baada kuwaona wakiingia, "asante lakini samahani kwa kuchelewa" alijibu Mr Kelvin ambae alionekana ni mwenye busara. "mbona kijana wenu anaonekana hajachangamka" Aliongea Mr Hendrix baada kumuandalia mtoto aliebebwa na mke wa Mr Kelvin. "ah ni kawaida yake huyo hawezi shangwe" alijibu Mr Kelvin huku akicheka, "anaitwa nani" aliuliza tena Mr Hendrix, "Alwin ndio Jina lake"alijibu Mr kelvin huku akimchukua Alwin kutoka mikononi mwa mkewe na kumshusha chini.

"Alwin nenda kacheze na wa wenzako" alimwambia lakini Alwin wala hakusogea hata hatua moja, "mume wangu si unajua mtu mwenyewe huyo hawezi kujichanganya, acha tu nitakaa nae mimi" mkewe aliongea. "muache akacheze na wenzake na wewe nenda ukasalimiane na wanawake wenzako" alijibu Mr Kelvin akiwa amekunja sura.

Bila kuuliza kitu mkewe aliondoka na kumuacha Alwin akiwa amesimama pembeni ya babaake. "unajua sikujali sana hii tabia ya mwanangu kutojichanganya kipindi ambacho nilikuwa naishi nje ya mji huu, lakini sasa hivi lazima ajifunze kwa sababu hapa ni kwao" aliongea Mr Kelvin, basi Mr Hendrix alimwita mfanya kazi mmoja na kumwambia ampeleke Alwin kwa watoto wenzake.

Baada Alwin kuchukuliwa wao walianza kuongea mambo yao ya kibiashara huku wakisubiri muda ufike Jestina aletwe ukumbini. Baada ya nusu saa mlango ulifunguliwa na Jestina akaingia ukimbini huku aksindikizwa na mziki wa happy birthday mpaka kwenye meza ya keki.

Alwin ni miongoni mwa watoto waliosimama mbele kabisa karibu na meza yenye keki lakini hakuimba, alinyamaza kimyaa na kutulia kama maji mtungini. Ni utamaduni wa mji huo katika kusheherekea mwaka wa tatu tokea kuzaliwa, yule ambae ndie mwenye sherehe huchagua mtoto mmoja na kucheza nae. "sasa tunamtaka Ms Jestina amchague mtoto mmoja wa kiume ili acheze nae kama sehemu ya kudumisha utamamduni wetu" MC aliongea na bi Prisca alimsogelea Jestina na kumnong'oneza jambo, Jestina alitabasamu kidogo na kutoka kwenye meza ya keki.

Hakika kila mtoto mwenye umri wa miaka mitano kushuka chini alitamani iwe ni yeye ambae atapata bahati hiyo isipokuwa Alwin peke yake ,yeye aliomba asionekane haswaa lakini ni tafauti na alivotarajia. Jestina aliomsogelea na kumkabidhi uwa ikiwa ni kama ishara "njoo tucheze". Mama Alwin alijishika kichwa baada kuona mwanae ndie aliechaguliwa maana alielewa kuwa kungetokea vituko tu katika dance floor.

Alwin hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali japo kuwa alikuwa katika wakati mgumu sana, maana akili yake ilikuwa haikubaliana haswaa na jambo hilo. DJ aliweka mziki laini unaojulikana kama slow germ, pamoja na kuwa Jestina alikuwa mdogo lakini yeye alishaafundishwa kucheza japo hakuwa akijua sana tafauti na Alwin ambae ilibidi amfuate Jestina anavyokwenda. Lakini maajabu yaliotokea baada dakika kidogo kupita, Alwin alionekana kuanza kuchanganya katika kucheza hata babaake na mamaake walishanga kuona mtoto wao anacheza huku ametabasamu.

Mziki ulikwisha na sherehe ikawa imeanza rasmi, Jestina alikata keki na kuwalisha watoto wenzake wote. Baadae mziki ulifunguliwa tena na kila mtu akawa anashereheka kwa njia yake isipokuwa Alwin peke yake ambae aliondoka kabisa ukumbini na kuelekea varanda, "wewe mbona uko huku" ni sauti ya kitoto iliomuuliza. Alipogeuka alikutana na tabasamu liloipamba uso wa Jestina, "sijiskii kucheza" alijibu. "basi kama hutaki kucheza shika hichi kibox na ukipange mpaka rangi zinazofanana zikae pamoja" Jestina aliongea huku akimpa puzzle box Alwin na yeye alikuwa na kingine.

Alwin alitabasamu kidogo na kumwambia "unaonaje tukashindana yupi atakae maliza mwanzo", "sawa" alijibu Jestina na wote wakakaa chini na kuanza mashindano. "jamani Jestina na Alwin wako wapi" bi Prisca alikuwa alikuwa akiwauliza wafanya kazi ambao hata wao walisema hawajui.

Bila kuchelewa aliekea kwa Mr Hendrix na kumwambia kuwa Jestina na Alwin hawaonekani, wala hakushtuka sana "usijali ni watoto na hawajotoka ndani ya nyumba,we nenda kapumzike mi nitawatafuta" alisema na kumwambia Mr Kelvin amfuate. Walizunguka nyumba nzima lakini hawakuwaona mpaka wasiwasi ukaanza kuwapata.


Upande wa pili huko mpambao ulikuwa mkali kupita maelezo, kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alwin kucheza mchezo ule ilikuwa ni vigumu sana kushinda lakini akili yake ilionekana kutokubaliana na kusindwa hivyo alienedele kuminyana na puzzle hio huku kijasho chemba kikimtoka. Wakati wakiendelea kutafuta, wazo lilimjia Mr Hendrix na kumwambia mwenzie waelekee varanda. Walipokaribia tu waliwaona wawili hao wakiwa katika mtanange huo na Mr kelvi alipotaka kuenda kuwashtua Mr Hendrix alimzuia na kutoa simu na kuanza kurikodi pambano hilo.

Kila mpambno ulivyokwenda ulizidi kuwa mkali huku kila mmoja akihakikisha anamaliza mwanzo kuliko mwenzake. Lakini bahati ilikuwa mbaya kwa Jestina baada kushindwa na Alwin ambae ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanga puzzle ile. Kwa kweli llilikuwa pigo kubwa kwa Jestina, alianza kulia baada kuona kuwa ameshindwa wakati yeye ndie aliezoea hasa kupanga vibox hivyo. Mr Hendrix alimsogelea na kumbeba mwanae "mbona unalia", "baba kanishinda yule" alijibu huku akimnyooshea kidole Alwin. "kushindwa ni kawaida katika maisha, lakini ipo siku na wewe utamshinda" aliongea huku akimfuta machozi mwanae ambae alianza kutabasamu.


ITAENDELEA
 
JESTINA-2
"Alwin njoo" Mr kelvin alimuita mwanae na kumbeba, "Mr Kelvin" aliitwa na rafiki yake. "nishaalijua tatizo la mwanao la kushindwa kujichanganya" aliongea Mr Hendrix na kumshangaza rafiki yake, "Alwin ni genius" aliendelea kuongea. "acha utani wewe" alijibu Mr Kelvin huku akicheka akidhani rafiki yake anamtania. "unadhani nakutania, huyo mwanao ni genius na kama huamini kesho asubuhi njoo nae tuende hospitali akafanyiwe IQ test" aliongea Mr Hendrix akionyesha yuko serious sana. Basi walkubaliana kesho yake aje ili waende hospitali kwa ajili ya kazi ile.

Baada ya hapo walirudi ukumbini na kuendelea kushereheka mpaka muda wa kuondoka ulipofika. Kila mtu aliaga na kurudi makwao, mawazo yalikiandama kichwa cha Mr Kelvin huku akijiuliza maswali kadhaa yaliokosa majibu. Alifika nyumbani kwake na kupumzika, siku ya pili mapema alimueleza mkewe kila kitu na kumwambia amuandae Alwin anataka kutoka nae. Baada ya nusu saa Alwin alikuwa tayari na safri ya kuelekea kwa Mr Hendrix ilianza, alimkuta rafiki yae huyo akimsubiri na hwakukaa sana waliondoka kuelekea hospitalini.

"habari za saa hizi dokta" Mr Hendrix aliongea baada kukaribishwa kwenye viti, "salama tu, niwasaidie nini". "ah tumemleta kijana wetu kwa ajili ya kupimwa uwezo wa akili", "ahaa basi haimna shida nifuateni". Dokta aliinuka na kuongoza njia mpaka alipofika katika chumba kilichoandikwa IQ test room na kuingia.

Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu kumi ambao walionekana kama maprofesa "karibuni naomba mkae hapo,huyo mtoto nipeni mimi" aliwaonyesha sehemu ya kukaa na yeye akamchukua Alwin na kumpeleka kwenye kiti kilichokuwa katikati ya chumba hicho kisha yeye akarudi na kuungana na kina Mr Hendrix. "jina lako nani" aliuliza mmoja kati ya wale watu kumi, "jina langu ni Alwin Kelvin Alfred". "una miaka mingapi" aliuliza mwengine. "nina miaka mitano". "sasa Alwin tutakuuliza maswali kumi, matano ya kawaida matano ya hesabu" aliongea mwengine "na kila swali utapewa sekunde kumi kulijibu", "sawa" alijibu Alwin.

swali la kwanza: "umeingia kwenye banda la wanyama, chini kuna nyoka wawili, kwenye mti kuna nguchiro wanne na ndege watano wamekaa na wawili wanaruka, je kuna miguu mingapi iliokanyaga ardhi?"
Alwin: "kuna miguu miwili na hiyo miguu ni ya kwangu"
Swali la pili: "juu ya mti kuna mananasi nane, yakachumwa matatu. je yatabaki mangapi?"

Alwin: "mananasi hayaoti juu kwenye mti"

Swali la tatu: "ikiwa simba anauwezo wa kumuua swala kwa dakika mbili, je chui atakua na uwezo wa dakika ngapi kumuua swala huyo huyo?"

Alwin: "haiwezekani kwa sababu swala huyo kashakufa tayari, kauliwa na simba"

Swali la nne: " Clinton ana uraia wa nchi mbili wa Jamaica na wa Brazil, alizaliwa Jamaica lakini sasa anaishi Brazil, kwa sababu za kisheria Clinton hawezi kuzikwa Brazil. Je sentensi ya mwisho ni kweli ama uongo?"

Alwin: "ni kweli, kwa sababu Clinton bado hajafa"

Swali la tano: " kuna wakati kipindi cha christmas, Santa Claus hakuwapa watoto zawadi. Alikwenda North pole akiwa na chupa mbili za wiski, chupa tatu za wine na chupa nne za bia katika begi lake. Alikunywa zote mpaka tone la mwisho kisha akalala. Alikuja kuamka saa tatu asubuhi akiwa na chupa tisa ambazo zinakaribia kuwa tupu. Ikiwa sentensi tatu za mwanzo ni kweli basi sentensi ya mwisho ni kweli au uongo"

Alwin: "uongo, kwa sababu kumebakiwa na tone moja katika kila chupa, hata hivyo hakuna asubuhi wakati wa decmber katika north pole, kuna usiku tu".
Swali la sita: " kati ya namba hizi ipi haigawinyiki kwa tano. 786, 981 na 123"
Alwin: "zote zinagawanyika, ukichukua 786 gawa kwa tano unapata 157.2, 981 gawa kwa tano unapata 196.2 na 123 gawa kwa tano unapata24.6"

Maswali yaliendelea mpaka yote yalipoisha akawa amejibu yote kwa usahihi bila kukosea hata moja. Baada ya hapo alipelekwa katika chumba kingine lakini huko waliambiwa hawaruhusiwi kuingia ndani hivo walisubiri nje. Baada ya nusu saa daktari alitoka na Alwin na kuwaambia kuwa wasubiri muda si mrefu watapata majibu. Robo saa baadae daktari alitoka na ripoti kamili ya Alwin huku akitabasamu na kuwaomaba wamfuate. "kwanza niwape hongera kwa kuwa na kijana mwenye uwezo mkubwa sana wa akili, Akili ya Alwin inafanya kazi kwa kasi mara nne zaidi kuliko binadamu wengine, ninaposema hivyo namaanisha kuwa Alwina ana uwezo mkubwa sana wa kufikiri.

Hii hapa ni ripoti yake kamili , ana IQ ya 170 . Hii ndio sababu ya yeye kupata ugumu katika kushirikiana na wenzake kwa sababu uwezo wake wa kupambanua mambo si wa kawaida, hivyo lolote utakalo mwambia basi yeye atalitafutia maana kwa undani zaidi"

Daktari aliendelea kuawafafanulia tabia za Alwin na kuwaambia kuwa wasipokuwa makini basi watamsababishia matatizo makubwa sana kwa sababu akili yake huwa haiko tayari kulazimishwa kufanya jambo ambalo halitaki. Baada ya kuelezwa kila kitu walifanya malipo na kuondoka zao kurudi nyumbani, wakiwa njiani "Umejuaje kama Alwin ni genius" aliuliza Mr Kelvin. "ni kwa sababu hata Jestina pia ni genius lakini yeye IQ yake ni 150, na ile puzzle waliokuwa wakishindana kuipanga nilipewa na daktari ili nimpe mwanangu wakati anaposhindwa kutatua jambo, ni watoto wachache sana ambao wana uwezo wa kupanga puzzle ile wakati mawazo yao yapo kwengine, wakati ule wakishindana mawazo yao yalikuwa ni kwa jinsi gani wangeweza wangeweza kukabiliana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo ukumbini. We unadhani hawakutuona wakati tuna warikodi, walituona lakini kwa vile kimawazo hawakuwa pale basi hawakutushughulikia tu.

Usiniulize nimejuaje yote haya, ni kwa sababu nimesomea saikoloji" alijibu Mr Hendrix na kumfafanulia rafiki yake kila kitu. Walifika nyumbani kwa Mr Hendrix na kuagana, Mr Kelvin aliekea kwake akiwa na furaha kubwa sana na alipofika alimueleza mkewe kila kitu.

********************

Akiwa na miaka mitano Jestina alimpoteza mtu muhimu sana katika familia yake, Bi Prisca aliaga dunia baada siku chache tokea kusheherekea mwaka wa tano tokea kuzaliwa kwa Jestina. Hili lilikuwa pigo kubwa sana hasa kwa Jestina kutokana na mapenzi makubwa aliokuwa nayo juu ya bibi huyo. Walifanya maziko na kuomboleza baada ya hapo kila mtu alirudi kwake, na kadri muda ulivyokwenda Jestina alikaa sawa na kuendelea na maisha kama kwaida kwa sababu alielewa hapa duniania tunapita tu na kila mtu ipo siku atakufa.

Kutokana na uwezo mkubwa wa akili Jestina na Alwin walipelekwa shule ya vipaji maalum, na huko moto uliwaka wanafunzi wengine waliisoma namba maana wawili hao walikuwa hawapitiki. Hiyo ilipelekea mpaka wanafunzi wengine kuwachukia lakini wao hawakujali hilo, kwao masomo yalikuwa wanayapa kipao mbele. Miaka ilisonga mbele huku kila siku uwezo wao akili ukizidi kuwa mkubwa, hatimae walimaliza shule ya msingi na kujiunga na high school kwa ajili ya kujiendeleza na masomo zaidi. Kwa wakati huo Alwin alikuwa na miaka kumi na tatu na Jestina alikuwa na kumi na mbili.

Pamoja na umri mdogo lakini uzuri wa Jestina uliwavutia mapaka shume na kuanza kumtongoza. Lakini wengi waliambulia pakavu, lakini kwa Alwin ilikuwa tofauti japo yeye alimpenda alishindwa kumwambia. Lakini aliuonyesha dalili zote za upendo hata hivyo Jestina hakuonyesha dalili zozote za kumpenda zaidi ya upendo wa kirafiki tu.

Maisha yalisonga mbele huku walimu wakivutiwa sana na juhudi za wawili hao japo walikuwa magenius, hatimae walimaliza high school na kujiunga na college. Sasa Alwin alikuwa na umri wa miaka kumi na saba na Jestina alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, uzuri wa Jestina ulizidi kunawiri huku ukitii kanuni za kibaolojia.

Macho yake makubwa yalimpendeza yakisindikizwa na uso wa duara uliopambwa na pua ndogo nzuri pamoja na mdomo wenye lipsi ambazo muda wote ziling'aa. Hakuwa na kifua kikubwa lakini kilitosha kumueleza rijali yeyote kuwa tayari kifua hicho kilishamea vya kutosha, kiliambatana na mdidimio mkubwa kiunoni na hips zilitanuka vizuri sana huku zikiruhusu mwili huo uonekane kama nambari nane ambayo imeandikwa na fundi alieumba kila kitu.

Kwa kweli uzuri wake ulipitiliza sasa na kuanza kuwachanganya walimu pamoja na wafaunzi na kila aliepishana nae njiani. Wapo waliojikwaa na kudondoka, wapo waliokosa kupata ajali kwa kumshangaa pindi anapopita, lakini kwa Alwin yote hayo yalikuwa yakawaida sana ukizingatia yeye amekua nae. Wakiwa college ukaribu wao ulimjengea uhasama mkubwa Alwin na kujikuta akipewa vitisho mara kwa mara. "Jestina na Alwin munaitwa ofisini" aliingia mwanafunzi darasani na kutoa tangazo hilo. Bila kuchelewa waliinuka na kuelekea ofisini walipoitwa.

"Vijana najua mtakuwa na maswali kwanini nimewaita" aliongea mwalimu mkuu huku akiwaangalia wawili hao kwa makini. "hivi punde tu nimepokea barua kutoka wizarani kuwa kumeandaliwa mashindano ya kielimu kwa ajili college zote hapa mjini na kwa kweli sisi tumekuwa wa mwisho kupata taarifa hiyo na mashindano yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa" aliendelea kuongea mwalimu mkuu.

"Maswali yanahusu nini" aliuliza Jestina, "mengi yatakuwa ya kielimu hususan upande wa sayansi" alijibu mwalimu. "sawa sisi tumekubali kuiwakilisha shule" walijikuta wakiongea kwa pamoja kisha wakaangaliana na kutabasamu. "sawa basi mnaweza kwenda tukutakane kesho kutwa asubuhi" mwalimu mkuu aliwaruhusu na wao wakaondoka na kuelekea darasani huku kila mmoja akiwaza itakuwaje siku hiyo ambayo hata maandalizi hawakuwa nayo.


Muda wa mapumziko ulifika na wanafunzi wote wakatika madarasani kuelekea sehemu tafauti. "Habari yako Jestina" ilikuwa ni sauti iliotokea nyuma ya Jestina, "safi" alijibu huku akigeuka na macho yake yakagongana na kijana Matt, kijana huyo ni mtanashati sana na wengi wamempa jina la HANDSOME. "tunaweza kuongea kama utakuwa unanafasi" aliomba Matt, "sawa hamna shida" alijibu, hiyo ni sifa kubwa sana aliokuwa nayo Jestina, hakutumia uzuri wake kuwanyanyasa watu kama walivyo waschana wengi.

Waliongea mengi lakini madhumuni ya kikao hicho ilikuwa ni kijana Matt kumueleza Jestina hisia zake juu yake, na alionekana ni bingwa katika tasnia hii ya kutongoza maana hakuwa na historia ya kukataliwa na mwanamke yeyote yule aliemfata. Basi Jestina aliomba muda ili atafakari ombi hilo na kijana Matt hakufanya makosa ya kukubaliana na ombi hilo.

**********************
 
Wasi wasi wangu ni kuwa, mwanzo mnaanza vizuri, mkifika katikati mnaharibu. (mgema akisifiwa ,tembo hulitia maji)
 
JESTINA-3
"mwanangu sidhani kama kuna mtu atakaeweza kumtongoza Jestina", "ah lakini yule si ana bwana wake ". "yupi" ,"si yule genius mwenzake", kiliskika kiundi cha vijana kadhaa wakiongea na wengi walionekana kuwa na uchu wa kumvua nguo msichana huyo mrembo kuliko wote college hapo. "hakuna mkate mgumu mbele ya supu nyinyi" hapo ndipo ikaskika sauti ya Matt, "lakini mkate ule sidhani" mmoja aliongea. "ok, ikiwezekana je mtanipa nini" aliongea Matt kwa kujiamini. "we kama kweli unajiamini nenda kuhusu malipo ukishafanikiwa tutajua sisi tukupe nini" mmoja wao aliongea na wengine wakamuunga mkono. "basi siku mbili tu, ya tatu atakuwa kashakuwa wangu" aliongea Matt na kuondoka huku akijiapiza kuwa lazima ampate kwa njia yeyote ile hata kama haitakuwa nzuri.
"Alwin nishauri kitu" Jestina aliongea wakati akiwa rafiki yake kipenzi, "kitu gani hicho" Aliuliza. "si unakumbuka niliwahi kukwambia kuwa nampenda Matt", "ndio". "sasa leo muda wa mapumziko kanifata na kunambia ananipenda". Kwa kweli ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Alwin kumshauri Jestna hasa ukizingatia yeye pia alikuwa akimpenda sana lakini alipenda muda wote Jestina awe na furaha. "mimi nikushauri nini tena zaidi ya kukuona ukiwa na furaha" Alwin alijikaza na kuongea japo alielewa ndo kashamkosa tayari. Jestina alimkubatia Alwin kwa furaha bila kujua ni kwa jinsi gani Alwin ameumia, hii ndio inakuwa shida kwa magenius wengi wanashindwa kugundua kwa muonekano fulani basi mtu anakuwa yupo katika hali gani. Wao hujali furaha yao tu, na ndivyo ilivyotokea baada kumkumbatia aliinuka na kuenda kwao akiwa mwenye furaha sana na uzuri ulizidi mara dufu.
Alwin aliinuka na kuelekea kwao huku njia nzima akiwa ni mwenye mawazo kupita maelezo, usiku huo ndio ulikuwa usiku mrefu ambao hajawahi kuuona tokea azaliwe. Palikucha na kama kawaida wanafunzi wote alienda mashule, siku hiyo ilikuwa ni siku mpya kwa Jestina ambae alionekana kupebdeza kupita maelezo. Muda wa mapumziko ulipofika alimwita Matt na kumwambia kuwa amemkubalia ombi lake, Matt alijpongeza kwa ushindi ule japo moyoni hakumpenda hata kidogo na alifanya vile kuwaonesha kama yeye next level. Maisha mapya ya kimapenzi yalianza kwa Jestina lakini kwa Alwin yalikuwa ni magumu hayajawahi kutokea.
Siku ya mashindano ilifika, mapema asubuhi Alwin na Jestina walichukuliwa na kupelekwa katika ukumbi ambao ungefanyika mashindano hayo yaliokuwa yanatarajiwa kurushwa live kati runinga. Saa mbili mashindano yalianza na kweli yalipamba moto huku timu ya magenius hao ikiogoza kwa kupata alama nyingi sana na mpaka mashindano yanakwisha waliondoka na alama elfu moja bila kukosa swali hata moja. Walirudi shuleni na kupokewa kwa shangwe kubwa sana na kuambiwa wajiandae kwenda mashindano ya kitaifa ambayo ilikuwa ni hatua ya pili kuelekea mashindano ya kimataifa. Kwa muda mfupi tu alioingia katika wimbi la mapenzi Jestina, urafiki wake kwa Alwin ulianza kupungua kwa kasi. Japo Alwin alijitahidi kuwa karibu nae lakini yeye alionekana kumtenga na mapenzi yake yote aliyahamishia kwa Matt.
Unyonge na upweke ulianza kumtafuna Alwin, "nikiruhusu hali hii ya upweke iendelee itaniathiri kisaikolojia, sasa ni muda kukubali kuwa Jestina nimeshanpoteza" alijisemea moyoni wakati akiwa peke yake. Baada ya kusema hivyo akili yake ilikubaliana nae na kuanza maisha mapya ambayo ndani yake hayakuwa na Jestina zaidi ya yule aliemzoea tokea udogoni kwake. Kuna wakati ilifikia hata salamu yake ikawa haiitikiwi na Jestina lakini wala hakushtka wala kuacha kumsalimia. Taratibu ubongo wa Jestina ukaanza kufanya kazi ndivo sivo, muda mwingi alimfikiria Matt badala ya kusoma hivyo kuanza kuathiri hata maendeleo yake ya kimasomo.
Alwin alijaribu kumueleza lakini sasa alionekana kama adui yake, kuna wakati alimtolea maneno ya kashfa kama vile "achana na mimi sio wa aina yako", "kwani we baba yangu mpaka unambie ninacho fanya ni kizuri au kibaya". Alwin hakuamini kama maneno hayo yalitoka kinywani mwa rafiki yake kipenzi "ama kweli mapenzi ni ulemavu" alijikuta akijisemea maneno hayo baada kukaripiwa na Jestina mbele ya umati wa watu. "hapa ni katika nyumba ya ibada usipokuja kwa kusali basi utakuja kwa dhiki au kuagwa lakini utakuja tu" Alwin aliongea maneno hayo kwa nguvu na kupenya sawa sawia katika masikio ya Jestina na alipogeuka alimuona Alwin akitokwa na machozi.
Bila kuongea neno jingine lolote aligeuka na kuelekea kwenye gari yake na safari ya kuelekea kwao ikaanza. Kwa mtu mwenye akili za kawaida alielewa maneno yale yalimaanisha nini lakini kwa Jestina kutokana uelewa wake mdogo juu ya kutambua hisia hakuyaelewa kabisa akabaki anacheka tu na kumfanya kila mtu kumshangaa.
Hata hivyo Jestina aliwapuuza watu waliokuwa wakimshangaa, "hivi kweli Jestina wewe leo ni wa kumdhalilisha rafiki yako kipenzi tena mbele za watu" Miryam ambae ni rafiki mkubwa pia kwa Jestina alimuuliza. "na wewe usianze kuwa kama Alwin niache na maisha yangu" alijibu kwa kejeli, "laiti ungeujua uzito wa maneno aliyoyasema wakati anaondoka basi ungemkimbilia na kumuomba msamaha" aliongea mwanamke huyo ambae alionekana kusikitishwa na mabadiliko ya Jestina. "au wewe unamtaka Alwin, sema kama unamtaka nikuunganishie" Jestina aliendelea kujibu utumbo, "kwa taarifa yako bibie kila mwanamke hapa shule anatamani kuwa na mwanaume kama Alwin, mwanaume ambae anajua thamani ya mwanamke, mwanaume ambae hakubali kuona mtu wake wa karibu anakunja uso, mwanaume ana utu na anajua kama mwanamke ni wa kuheshimiwa na sio kufanya kama mdoli" aliongea maneno hayo kwa ukali huku akimuangalia Jestina kwa macho makali "halafu unasema kama namtaka Alwin uniunanishie, wewe mapenzi umeyajua juzi tu tena kwa taarifa yako kwa Matt umebugi step shosti, subiri akutanue miguu tu uone kama atakuthamini tena. Hebu zunguka uulize waschana wangapi walihadaika na uzuri wake lakini baada kuwavua chupi amewatupa. Kwa Matt mwanamke ni kama tishu tu, ukishaaitumia mara moja unaitupa na kwa taarifa yako sina haja ya wewe kuniunganisha mimi kwa Alwin. Nimeridhika na upendo wa kirafiki anaonionyesha tafauti na wewe. Mwanamke gani usie na fadhila, hustiriki kama harufu ya mavi au kwa sababu unaakili nyingi ndio unamuona kila mtu bwege. Pole kwa hilo na kama nimekukasirisha kunya boga" Miryam aliongea kwa hasira sana na alipomaliza hakusubiri jibu aligeuka na kuondoka maana alielewa kukaa pale kungezuwa matatizo.
Ukweli Miryam anampenda sana Alwin lakini baada kugundua kuwa Alwin ametokea kumpenda Jestina hakutaka aingilie kati na badala yake aliomba kuwa rafiki wa Alwin na Jestina ombi ambalo lilipokewa kwa mikono miwili na marafiki hao. Miryam ni mtoto wa tatu katika familia nambari moja kwa utajiri katika mji wa Mashvile, ni mschana mrefu mwenye asili ya kivenezuela na weupe wa kungaa. Kichwa chake kilipambwa na nywele za kimanga zilizonyooka kama nguo iliopigwa pasi, Kwa bahati mbaya yeye ndie mtoto pekee alieyepona katika ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao akiwemo mama yake pamoja na kaka na dada yake. Kwa sasa anaishi na baba tu ambae kwake ndie baba na ndie mama.
Wanaume wengi walijaribu bahati yao kwa lengo la kula vya bure lakini waliambulia pakavu, na hakukuwa na kitu cha kumlaghai maana kama gari yeye binafsi ana miliki gari kumi tena tafauti na pia ni za bei mbaya. Kama vito kila siku anavaa vipya, kiufupi hakuna anachokosa kwao hivyo wengi walishindwa kumkamata ndege huyo. Siku ya pili mapema Alwin aliwasili college na kuendelea na ratiba zake kama kawaida bila kusahau kumpa salamu best yake Jestina ambae hakuijali kabisa. Hata hivyo alijisemea moyoyni "mimi wajibu wangu ni kukupa salamu tu, kujibu hiyo ni juu yako" japo aliumia kwa upande mwengine lakini alijikaza kiume tu.
******************************
"Alwin, Alwin, wewe Alwin si nakuita" Miryam aliita mara kadhaa lakini Alwin hakuskia mpaka pale alipomtingisha. "eh, samahani nilikuwa sipo kabisa hapa" aliongea Alwin huku akilazimisha tabasamu kitu ambacho Miryam alikishtukia mapema. Lakini alielewa nini cha kufanya hasa anapomkuta Alwin katika hali hiyo, "unajua kawaida yetu watu kama sisi tunapokutana na jambo ambalo ni gumu kulitatua basi njia pekee ya kutusaidia ni kutupa swali" aliakumbuka maneno hayo ambayo aliambiwa na Alwin siku za nyuma. Basi alifungua begi lake na kutoa kitu kama kiboxi kidogo na kumkabidhi. "nisaidie kufungua hicho kiboxi nimepewa na baba lakini mimi kimenishida" aliongea Miryam kwa sauti ndogo sana. Alwin alikiangalia kidogo kisha akamuangalia Miryam "lakini mbona hiki kimepangika vizuri tu".
"Baba kanambia ikiwa hizo picha zitapangika basi kitafunguka chenyewe" alijibu Miryam. Hapo sasa Alwin alikiangaliwa kwa umakini na kugundua picha zote zilikuwa sawa lakini kulikuwa na tofauti ndogo katika kila picha. Tofauti hio ndio funguo wa kufungua kibox hicho, alimpa Miryam kibox na kumwambia azipangue zile picha kisha yeye akafunga macho. Alizipangua zote na kumwabia "tayari".
Alwin alifungua macho na kuanza kuzipanga zile picha upya. Kila baada dakika moja aliandika namba kwenye karatasi mpaka zilipotimia sita akatoa pumzi kwa nguvu na kumuangalia Miryam ambae alikuwa amekodowa macho utadhani mjusi aliebanwa na mlango. Kisha Alwin alianza kuvipanga vipande vya zile picha na kila baada ya mizunguko sita aliahamisha kipande kimoja na kukiingiza upande wa pili wa kiboxi hicho mpaka ilipotimia mizunguko thalathini na sita, aliandika namba hiyo na kuigawa mara tatu na kundika kumi na mbili. Alinza tena kukipanga na kila alipofika mizunguko kumi na mbili alihama upande mpaka ilipotimia mara kumi na mbili.
Baada ya hapo akaivunja kumi na mbili mara nne na kupata tatu, kisha akaanza tena kuzipainga lakini mara hii alidili na mstari wa tatu tu. Na kila baada kupanga vipande vitatu alihama upande na mwisho alikamilisha zoezi hilo. Kumbe zile picha zilikuwa na maandishi yalioadikiwa "HAPPY FRIENDSHIP DAY ALWIN", na ghafla kilifunguka na ndani kulikuwa na funguo ilioandikwa "SPECIAL FOR ALWIN". Miryam alimuangalia Alwin kwa makini kisha akamwambia "unakumbuka siku niliokwambia nikipasi kuingia mwaka wa tatu college nitakupa zawadi", "ndio nakumbuka" Alwin alijibu kwa sintofahamu. "nifate" Miryam aliongea na kuinuka na kuondoka na Alwin alinyanyuka haraka na kumfata.
Wakati wanatembea Miryam alito simu yake na kupiga "uleteni mzigo wangu" kisha akakata, walipofika barabarani. Miryam alionesha ishara ya kusimama na ghafla ikaja gari kubwa aina ya scania na kusimama mbele yao ikiwa imebeba kontena. Milango ya kontena ilifunguliwa na kushushwa pikipiki moja nyeupe kama zile za mashindano. Katika pipa la mafuta iliandikwa "SPECIAL FOR ALWIN", Alwin alibakia ametoa macho tu maana alipanga atengenezesha pikipiki kama hiyo akishapata kazi yake. "umejuaje kama nilikuwa napanga kutengeneza pikipiki ya aina yangu peke yangu" hilo lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kinywani mwa Alwin, "siku ile ulionambia nikachukua kitabu katika begi lako nilikuta picha ya pikipiki hii ulioichora na kuandika chini MY FUTURE RIDE.
 
JESTINA-4
Namimi nikaona kwanini nisikuapatie zawadi hii kama fadhila za msaada wako mkubwa katika masomo yangu. Ndipo nikaipiga picha pamoja na vifaa vyote ulivovichora kisha nikampelekea baba yangu na kumwambia anitengenezee, aliponiuliza ni kwanini nataka itengezwe nikamjibu kuwa hii itakuwa zawadi kwa mtu aliefanikisha mimi kupasi japo nilikuwa mzito kwenye masomo. Hapo akanambia nimueleze wewe ni nani na mimi nikamwambia kila kitu, basi alisafiri kuelekea ujerumani kwa ajili ya kazi hii tu. Kwa vile wewe ni genius akaamua kutengeneza kiboxi hichi na kuweka funguo na kunambia kuwa mwenye uwezo wa kufungua kiboxi hichi ni mtu mwenye IQ kati kati ya 165 na kuendelea juu. Na ameweza kukidizaini hicho kibox kwa mfumo wa hesabu" aliongea Miryam na kumshangaza Alwin, "basi kama baba yako ndie aliekitengeneza koboxi hici bila shaka na yeye ni kama mimi" Alwin aliongea.
"hujakosea mwanangu ila mimi nimekuzidi sana" iliskiaka sauti ikitokea nyuma yao. Alikuwa ni baba yake Miryam " mimi nina 197 IQ capacity na ndie niliendaa mashindano ya magenius" alijib Mr Alexander Harison, hilo ndio jina lake nainasemekana ndie mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani. "mimi na wewe tutaonana kwenye fainali za mashindano haya na nakutakia siku njema" alimaliza kuongea na hapo hapo ikaja gari, aliingia na kuondoka. Alwin hakuamini macho yake kama mtu aliemuona mbele yake ndie mtu ambae alikuwa akimkubali tokea udogoni kwake. Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwa Alwin alijikuta kwa muda akisahau machungu yote na maumivu aliyoyapata kutoka kwa Jestina.
Alwin alijikuta akimkumbatia Miryam kumbatio ambalo kwa wengi lilitafsiri kuwa ni upendo. Kwa mara ya kwanza Miryam alijikuta akilihisi joto la mwanaume huyo ambae alitokea kumpenda kupita maelezo. Mkumbatio huo ulidumu kwa dakika kama mbili hivi, kisha wakaachiana huku Miryam akiangalia chini kwwa aibu. "asante sana Miryam kwa zawadi yako nzuri" Aliongea Alwin huku machozi kwa mbali yakilowanisha macho yake. "usijali Alwin hivyo ndivyo marafiki wanavotakiwa kuwa" alijibu Miryam na kutoa kitambaa chake na kumfuta machozi ambayo tayari yalishaanza kulowanisha mashavu ya Alwin.
Yote hayo yalifanyika huku Jestina akishuhudia kila kitu, lakini hata hivyo alipotezea na kuondoka eneo hilo. "ah halafu nimesahau subri na mimi nikupe zawadi yako" Alwin aliongea na kufungua begi lake na kutoa kitu mfano kama wa simu. "hiki kifaa nimekiteneza mwenyewe na nimekiprogram na maswali mengi sana ambayo yatakusaidia ikiwa utahitaji msaada na sitokuwa karibu" Aliongea na kumkabidhi kifaa kile. Miryam alirukaruka kama kidege huku meno yote thalathini na mbili yakiwa nje. Baada ya hapo kila mtu aliondoka na Alwin aliltafuta Jestina ili ampe zawadi ya siku ya marafiki duniani lakini alichokutana nacho huko kilikuwa kinyume maana Jestina alitoa maneno machafu huku akimwita Miryam malaya. Hakumaliza kuongea alichezea kibao kizito kutoka kwa Alwin na kumfanya ayumbe kidogo kabla ya kuzuiwa na bwana wake Matt "umeniacha bila chaguo Jestina ila kukufunga mdomo na nikwambie kitu huna haki ya kumuita Miryam majina machafu kama hayo. Nimejaribu sana kukueleza lakini inaonekana Matt anakutia kiburi sana" Alwin aliongea na wakati huu alivimba kwa hasira.
"We dogo sikia nikwambie, kama unataka kupimana uzito pimana na saizi yako na sio kukimbilia waschana" Matt aliongea huku akimsukuma Alwin. "Na wewe mwanaume mpumbavu usie na akili, kwa muonekano tu hata kurusha jiwe huwezi achilia mbali kukunja ngumi. Kama unadhani kuwashusha sketi wanawake ni uanaume basi umebugi na nikwambie kitu kama kweli unaweza ndondi tuzame uwanjani nikuonesha kama mwanaume hasifiwi kuchungulia wanawake" yalitoka maneno hayo kinywani mwa Alwin na kushangza umati mzima maana huyo hakuwa Alwin aliezoeleka hapo college. Basi Matt alitaka kumjaribu Alwin japo Jestina alijaribu kumzuia lakini ilishindakana.
Jestina alimfahamu vizuri sana Alwin anakuaje hasa pale anapojaribu kuwalinda wale anaowajali sana. Basi kwa kutaka kuonyesha kama yeye ni kidume alianza kumsukum Alwin ambae kwa wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hasira, alipomsukuma mara ya tatu Alwin alijibu mashambulizi kwa kumpiga ngumi mbili kwa wakati mmoja kwenye mabega yote mawili. Bila kutaka Matt alijikuta akikibetua kifua chake huku mikono ikikosa ushirikiano na mwili, hapo Alwin alimtandika ngumi nzito ya kifua iliotuwa kwenye chembe na kumfanya Acheuke damu na bila kutarajia alidondoka chini na kupoteza fahamu. "huu ni mfano tu, nikuskie unamtovukia tena adabu Miryam na akiinuka huyo basha wako mwambie akae mbali na mimi" aliongea Alwin na kugeuka, alikwenda mpaka lipo Miryam na kumwambia waondoke.
Siku ya mashindano ya magenius kwa ngazi ya kitaifa ilifika na matokeo yalikuwa kama yalivotarajiwa na wengi. Alwin na Jestina waliiwakilisha shule yao vizuri huku wakiibuka na alama nyingi sana. Walirudi college na kupokewa kwa shangwe "mashindano ya kimataifa yatakuwa mwezi ujao hivo naomba mujiandae vizuri ili mtusaidie kurudisha sifa ya college yetu" mwalimu mkuu aliongea wakati alipowaita ofisini kwaaajili ya kuwapongeza. "usijali mwalimu, tutajitahidi na kuhakikisha jina la college hii linakuwa zuri kama la zamani. Baada ya maongezi hayo walitoka na kuelekea nje, huko Jestina alipokewa na MAtt na Alwin alipokewa na mtoto Miryam. Maisha yalindelea huku maandalizi kwa ajili ya fainali yakipamba moto. Hatimae siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu ilifika, Jestina na Alwin walisafiri kuelekea nchini England maana huko ndipo fainali zilipokuwa zinafanyika. Watu wote wa Mashvile walikusanyika katika nyumba za ibada kuwaombea makinda hao ushindi wa kishindo.
"habari zenu mabibi na mabwana, karibuni katika THE WORLD ULTIMATE GENIUS CHALLENGE. Mgeni rasmi atakuwa profesa Alexander Harison mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili kuliko watu wote duniani mpaka sasa. Kwa ujumla mwaka huu timu zitakuwa hamsini na mchezo utakuwa na jumla ya mizunguko mitatu" MC alindelea kutangaza huku akiwekwa mbwembwe nyingi. "Jestina, huu ndio wakati tulikuwa tukijiandaa nao" Alwin alimwambia Jestina huku akimuangalia kwa makini. Wakati huu walizieka pembeni tafauti zao, "lakini mi naogopa" Jestina alijibu kwa sauti ya kutetemeka. "sasa unaogopa nini, usiwe na hofu kombe mara hii linakwenda nyumbani" Alwin alimjibu huku akimshika mkono.
Mashindano yalianza huku kila timu ikijitahidi kubakia mpaka mzunguko wa pili, lakini ni kawaida ya mchezo wengine kuwa wasindikizaji tu. Maunguko wa kwanza uliisha zikiwa zimebakia timu ishirini na tano tu na nafasi ya kina Alwin ilikuwa ni ya ishirini jambo ambalo lilimtia wasiwasi Alwin. "Jestina una nini lakini mbona ulikuwa unakosa maswali kizembe" Alwin alimwambia wakiwa mapumziko. "hata sijui kwa kweli" alijibu, "sasa ukiendelea kuwa hivyo tutatolewa mzunguko wa pili" Alwin aliongea na kumsisitiza arudi katika hali yake ya kawaida.
Kengele ya mzunguko wa pili ililia na washindani wote wakaingia ulingoni, mzunguko huo ulikuwa na maswali magumu sana na yalihitaji uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Kwa upande wa Alwin kazi haikuwa ngumu sana kwa sababu alitrain akili yake katika kiwango kikubwa cha kufikiri. Lakini kwa upande wa Jestina mambo yalikuwa magumu sana, hii ilitokana kila alipojaribu kufikiri mawazo ya Matt yaliingilia kati. Mzunguko wa pili ulikwesha na kwa bahati walipenya japo waliponea chupuchupu kutoka. Walikuwa katika nafasi ya tano katika timu tano zilizopita, kiufupi walishika mkia.
"Jestina, Jestina una nini lakini" Alwin alimlalamikia, "ukiendele kuwa hivo basi ushindi utatupitia mbali" aliendelea kuongea. Mapumziko yalikwisha na muda wa kurudi uwanjani ulifikia lakini hali ya Jestina ilibadlika ghafla na wakati wanatoka alidondoka chini na kupoteza fahamu. Watu wa huduma ya kwanza walimuwahi na kumpeleka katika chumba cha huduma ya kwanza. Na kwa bahati mbaya sana majibu yalikuja vibaya, Jestina asingeweza kushiriki mzunguko huo kutokana na kuwa akili yake imechoka sana. Sasa maamuzi yalibakia kwa Alwin ima aendelee kupambana peke yake au akubali kuachia mzunguko huo. "yaani nitoke kote huko mpaka hapa halafu niachie kirahirahisi hivi" alijsemea moyoni "litakalokuwa na liwe kombe linakwenda Mashvile".
Aliingia uwanjani akiwa peke yake. "sasa ni ule mzunguko wa akili nyingi, mabibi mabwana si mwengine bali ni THE ULTIMATE BRAIN STORMING CHALLENGE, mzunguko huu ni wa hatari hivyo tunaomba machela ziwe karibu na watu wa huduma ya kwanza msiwe mbali na ukumbi maana ni shiiiiida" MC alizidi kuweka vikombwelezo vingi. "mzunguko huu utakuwa na swali moja tu na kila timu itakuwa na nusu saa tu kumaliza mchezo, itaanza timu kutoka London" waliingia vijana hao walikuwa wamevaa miwani mikubwa, honi ililia na kuanza mchezo huo. Mchezo ulindelea "na sasa timu ya mwisho kuingia uwanjani ni kutoka Mashvile" Alwin aliingia peke yake na kuwafanya watu wote washangae.
********************
Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa, "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema"
Upande wa Alwin watu walizidi kushangaa maana walielewa kuwa jaribio hilo la mwisho mtu mmoja hawezi hata siku moja kushinda akiwa peke yake. "Alwin Kelvin inabidi uingie makubaliano kwamba lolote litakalotokea jumuiya ilioandaa mashindano haya haitahusika", "ndio nimekubali lolote litakalotokea litakuwa ni juu yangu" Alijibu Alwin kwa kujiamini. "Una dakika thalathni kuipanga ramani hii na muda wako unaanza sasa", honi ililia na dakika zikaanza.
Alwin aliangalia fumbo hilo ambalo kwa akili ya kawaida tu ungedhani michoro tu ya kitoto, "ikiwa watu wawili wanatumia dakika ishirini na tano zaidi kutatu fumbo kama hili, mimi natakiwa nitumie chini ya hapo kwa sababu niko peke yangu na hakuna wa kupingana na mawazo yangu" alijisemea mwenyewe huku akiendelea kuliangalia fumbo hilo. Baada kuridhika alitoa kalamu na karatasi na kuanza kazi, tayari dakika tatu zilishakatika. Kitu kimoja ambacho wengi hawakukijua juu yake ni kwamba ameifanya akili yake kufanya kazi kasi mara tatu zaidi kuliko computer, alianza kuandika namba namba nyingi huku akizikata kwa kuzipiga michoro. kila baada sekunde tano aliandika namba na kukata namba, wengi walimuona kama kijana anaepoteza muda kjaribu kutafuta umaarufu kwa kujaribu kujibu fumbo hilo peke yake wakati anajua kuwa hatoshinda.
"profesa mi naona anapoteza muda huyu kijana" mmoja kati ya watu waliokaa karibu na profesa Alexander Harison aliropokwa. "Huyu kijana atashinda tena atatumia dakika ishirini tu" Alijibu profesa huku akiwa hamuangalii mtu huyo, lakini ukweli alichukizwa na swali hilo. Dakika saba zilishakata huku Alwin akiendelea kuandika namba tu, kumbuka hapo yuko peke yake. Zilipotimia dakika kumi alibadilisha mfumo na kutumia mfumo wa matrix, kazi iliendelea huku watu wengi wakitegemea atashindwa kumaliza. Kutokana na kufikiria sana mishipa ya fahamu iliopita pembeni ya kichwa ilianza kuvimba na haukupita muda alianza kutoka damu za pua. Lakini wala alikuwa hajui hasa kama anachuruzika damu, MC alitaka kumwambia ache lakini Prof Alexander Harison alimpa ishara amuache kwani kumshtua pale kungepelekea kupasuka kwa mishipa hiyo.
 
JESTINA-5

Dakika kumi na tano zilikata na Alwin alianz kutabasamu baada hesabu zake kwenda kama alivyotaka. Alianza kuipanga ramani hiyo huku akiangalia saa iliokuwa ikimwambia kuwa zilibaki dakika kumi na tatu.
Aliongeza kasi ya kupanga ramani hiyo huku akihisi maumivu makali ya kichwa, Prof Alexander aliligundua hilo baada kumuangalia usoni. Aliinuka alipo kaa na kushuka kuelekea kwenye jukwaa alipo Alwin huku akiangalia saa yake ambayo ilimwabia bado dakika moja tu kutimia dakika ishirini. Alifika na kusimama nyuma yake na ilipotimia tu dakika ishirini Alwin aliinua mikono kuashiria alishamliza kupanga na hapo hapo Profesa akamgusa kwenye shingo kidogo na kumminya, alianguka na kupoteza fahamu. Kisha akatoa ishara watu wa huduma ya kwanza wafanye kazi yao na kuwaambia wamtundukie dripu ya damu pamoja na maji ya glucose, pia aliwaambia baada dakika tano atazinduka. Alirudi kwenye kiti chake na kutulia, dakika tano baadae Alwin alizinduka na kuruka kwa furaha. Watoa huduma wote walishangaa kumuona vile, walimtuliza na baada ya dripu kuisha alinyanyuka na kurudi ukumbini. "jamani makofi kwa mshindi wetu wa shindano hili gumu ALWIN KELVIN" MC alitangaza na watu wote walipiga makofi. "ndugu Alwin umepata nafasi ya kufanya mawasiliano na profesa Alexander Harison hapahapa ukumbini" aliendelea kutangaza na kumuelekeza kwenye kiti na majadiliano yakaanza.
Prof : Pole kijana kwa kazi nzito
Alwin: asante profesa
Prof: Tunaomba utuambie uwezo wako wa akili
Alwin: 176 IQ capacity
Prof: unajua kama leo umevunja rikodi ya mtu mkubwa sana
Alwin: hapana sijui
Prof: Hongera Alwin kwa kuvunja rikodi yangu, mimi nilimaliza ndani ya dakika ishirin na sekunde moja.
Alwin: Ah asante lakini wewe utabaki kuwa kama ulivo
Prof: na pia hongera kwa kujinyakulia cheo cha uprofesa katika hesabu hasa kwenye Matrix
Ukumbi mzima walishangaa kusikia maneno hayo kutoka kwa profesa huyo, mjadala ulikwisha kwa namna hiyo huku Alwin akinyakua tuzo tatu moja kama mshindi, ya pili ya kuvunja rikodi na ya tatu cheo cha uprofesa. Katika vyombo vyote vya habari, habari ilikuwa ni hiyo tu "KIJANA ALIEVUNJA RIKODI YA PROFESA ALEXANDER HARISON". Walipumzika siku hiyo na siku ya pili walipamnda ndege na kurudi Mashvile, walipokewa kwa shangwe hasa Alwin ambae alionekana shujaa wa sehemu hiyo.
Kama njia ya kutoa shukrani college iliamua kupanga safari kwa ajili ya Alwin na Jestina, ilikuwa ni safari ya kuelekea Mashvile National Park. Wanafunzi walifurahi sana kwa sababu kwa mwaka huo ilikuwa ni safari ya kwanza.
****************************
"hawezi kunifanya mimi nionekane bwege kiasi chote hichi, tokea tuingie katika mahusiano hajawahi kunipa penzi" Matt alikuwa akiongea peke yake huku akionekana mwenye hasira sana "lakini subiri atatoa tu, anadhani mi kaka yake". Siku ya safari ilifika na mapema asubuhi wanafunzi waliondoka na kuelekea Mashvile National Park (M.N.P), walifka saa sita mchana kwa sababu kulikuwa mbali sana. Muda mwingi Alwin alikuwa na Miryam na walionekana kufurahi sana, upande wa Jestina alikuwa hana amani kabisa hasa baada kugundua kuwa aliingia woga na kukubali kudhalilishwa na Alwin ambae kwa alivyotafsiri yeye ni kwamba "sina haja ya kuwa na mwenza kama wewe hata peke yangu naweza kushinda". Hivyo ndivyo alivokuwa akitafisiri Jestina, basi walindelea kufurahia safari hiyo huku wakitembezwa maeneo mbali mbali, jioni lipofika walikwenda kuogelea katika mto.
Usiku uliingia na wote waliambiwa wapumzike katika mahema yao. "Jestina....Jestina amka mpenzi" Matt alikuwa akimuamsha Jestna, "unataka nini bwana" Jestina aliongea kwa uvivu "twende nje tukaangalie mwezi". Basi waliinuka na kutoka lakini wakati wanatoka Alwin aliwoana na alihisi kuna kitu hakipo sawa kwa jinsi Matt alivyokuwa akimvuta Jestina, Hivyo aliamua kufwatilia kimyakimya. "Jestina kwa kweli nimevumilia muda mrefu na sasa nimechoka, naomba unipe penzi" Matt aliongea kwa macho makavu. "si nimekwambia tusubiri nikishakutambulisha nyumbani nitakupa" Jestina alijibu huku akijaribu kujitoa mikononi mwa Matt. "we nipe saa hivi ukishanitambulisha ndio itakuwa kawaida yetu" Matt aliendelea kusisitiza na alipoona Jestina hakubaliani nae alipiga mruzi wakatokea wenzake wengi wakiwemo waschana, kwa haraka idadi yao ilifika kama ishirini hivi.
Basi akatoa ishara watu wanne wakamvamia Jestina na kumlaza chini "mpumbavu wewe unajifanya unajua kubana si ndio sasa leo nataka nikuoneyeshe mimi ni nani" Matt aliongea huku akivua mkanda. Baada Alwin kuona vile alichomoka alipokaa na kutaka kutoa msaada lakini aliwahiwa na kupigwa gongo la kichwa lilimfanya aanguke chini. "we boya shuhudia ninavokata utepe wa genius mwenzako" Matt aliongea bila kuchelewa alimuinamia Jestina na kuanza kufanya uchafu mbele ya Alwin Jestina alijaribu kupiga kelele lakini mschana mmoja alimuwahi na kumtia kitambaa cha mdomo. Damu nyingi zilianza kumtoka lakini Matt hakujali hilo aliendelea kufanya yake mpaka aliporidhika alimuacha na kunyanyuka "oya anaetaka kujisevia na ajisevie tu mimi nishaafungua dimba" baada kutamka hivo vijana kadha walitaka nao kuonja utamu wa genius, jambo hilo lilimuumiza sana Alwin lakini hakuwa na la kufanya kwa sababu alikuwa ameshikwa kisawasawa.
Waliendelea kupokezana lakini waliingia wasiwasi baada kuona kuwa Jestina alitulia kimya chini huku damu nyingi ikimtoka sehemu za siri. Mmoja alijaribu kumtikisa lakini hakushtuka "toba kashakufa" mmoja wao aliropokwa na kila mmoja alitimua upande wake wakamuacha Alwin peke yake ambae alijivuta mpaka alipokuwa amelala Jestina. Alimuinua na kumuweka mapajani kwake. "Jestina... Jestina amka nakuomba" Alwin aliita huku akimpiga vibao vidogo vidogo mashavuni, "Alwin najua kama unanichukie sana kwa nilokufanyia" Jestina aliongea kwa sauti ya chini yenye maumivu makali ndani yake, "hapana sijawahi kukuchukia hata kidogo, nilikuwa nakupa muda tu ugundue tu njia ulochagua sio salama lakini ukweli nakupenda sana kuliko kitu chchote kile katika maisha yangu" Alwin alijibu huku machozi yakimtoka. "we unadhani kwanini nimeenedelea na mashindano hata baada ya wewe kutofanikiwa kushiriki, nilitaka ujue tu kama sikuwa tayari kukubebesha lawama za kushindwa, nilitaka ujue tu kama bado nakujali japo mengi yametokea" aliendelea kuongea kwa kwikwi.
"Alwin kwanini unanipenda kiasi chote hicho na wakatii nilishaakwambia zamani kuwa sina hisia za kimapenzi juu yako" Jestina aliongea japo kwa tabu sana. "Jestina kukupenda mimi haikuwa na maana na wewe unipende, penzi la upande mmoja lilitosha kabisa kuishi na wewe" Alwin aliendelea kuongea huku machozi yakimchuruzika ka maji machoni mwake. "Alwin nakuomba unyamaze na uniache nipumzike kwa amani, nakuahidi kuwa nitazaliwa tena kwa ajili yako iwe katika maisha haya au yoyote yale..... tafadhali niache niende kwa amani" alimaliza kuongea maneno hayo na kukaa kimya, Alwin alijaribu kumtingisha lakini hakushtuka, alipeleka kidole kwenye pua na hapo ndio akagundua kuwa tayari Jestina alishaamuacha peke yake duniani. "no...n.o...no ple...ase Jestina...Jestina... Jestinaaaaaa" alipiga kelele na papo hapo akapoteza fahamu.
*************************************************************
(miaka kumi baadae)
"Jestina amka" iliskika sauti laini ikimuamsha Jestina, alikurupuka kutoka kwenye usingizi huo akihema. "karibu katika ulimwengu wa waliodhulumiwa" alisikia tena sauti ikiongea lakini aliongea hakumuona. Na alipoangalia vizuri aligundua kuwa alikuwemo ndani ya jeneza, alitoka mbio huku akijaribu kutafuta njia lakini hakuiona kutokana na kiza kizito kilichokuwepo katika macho yake. "niko wapi" aliuliza, "khah! kwani hujui uko wapi" alijibiwa ,"sasa ningekuwa najua ningeuliza" alijibu Jestina kwa hasira kidogo. "wewe upo katika dunia ya wafu kwa maana nyingine tayari umeshakufa" alijibiwa lakini alionekana kutokubaliana na jibu hilo "haiwezekani mara ya mwisho nilikuwa mikononi mwa..." hakumalizia picha za tukio la yeye kubakwa na Matt halafu akaruhusu wenzake wajisevie zilianza kurudi kichwani mwaka. Akajikuta anaanza kupiga kelele huku machozi yakianza kumotoka lakini alipojaribu kuyafuta aligundua kuwa hayakuwa machozi bali ilikuwa ni damu iliokuwa ikitiririka machoni mwake.
"Kweli Matt ni wa kunifanyia vile, kumpenda kote kule ameamua kunifanyia unyama wa aina ile" alijikuta akijesemea mwenyewe huku hasira zikianza kumpanda. "usijali hapa upo kwa sababu wewe umedhulumiwa na hukupaswa kufa siku ile lakini Matt na wenzake wamekuhujumu na kusababisha kifo chako na matatizo mengine mengi sana ambayo ukiyaona lazima machozi yatakutoka". Ghafla mandhari ilianza kubadilika, muangaza mkali ulitokea mbele yake na kumfanya afunge macho yake. Alipoyafungua alijikuta yuko mbele ya watu wengi sana tena walikuwa wanatisha sana. Wapo waliokuwa hawana vichwa na wengine walikuwa wakivuja damu mwili mzima. "karibu katika ullimwengu wa mpito wa watu waliodhulumiwa" aliongea mwanamke mmoja alionekana kama kiongozi wa sehemu hiyo. "hapa upo kwa ajili ya kuwalipa wale waliosababisha kifo chako na kusababisha watu wako wa karibu kufarakana, kifo chako kimeacha utata mkubwa sana duniani na haki haiwezi kutendeka kwa sababu mtu mmoja tu ndie anaujua ukweli juu ya kifo chako lakini hawezi kutoa ushahidi kwa sababu amepata matatizo ya akili" alizidi kufafanua mwanamke huyo ambae alionekana ni Malikia.
"oh samahani Jina langu naitwa Malkia Alina" aliongea mwanamkwe huyo baada kugundua kuwa hakujitambulisha. "na utakaa katika ulimwengu huu mpaka pale kazi yako itakapo kamilika" aliendelea kuongea. Jestina alianza kujiangalia kwa makini sana na kugundua kuwa kucha zake zilikuwa kubwa sana tena ngumu huku macho yake yakiwa meupe bila kuonesha kiini, nguo alioivaa ilikuwa imetapakaa damu iliokuwa ikiendelea kutoka katika sehemu zake za siri. Sura yake ilikuwa imeharibika kabisa na ilikuwa ni vigumu hata yeye mwenyewe kujitambua. "najua utakuwa na maswali mengi sana, lakini ukiachilia damu inayokutoka sehemu zako za siri mabadiliko mengine yametokea kwa sababu hata wewe ulimdhulumu mtu haki yake wakati ukiwa hai na si mwingine bali ni Alwin" aliongea mwanamke huyo na kumfanya Jestina atoe macho akijiuliza amemjuaje Alwin.
"mimi mbona sijamdhulumu Alwin" alijaribu kujitetea lakini ghafla aliskia maumivu makali sana sehemu zake za majeraha, alipiga kelele akiomba msaada lakini yule malkia akamwambia "huku hakuna kusema uongo, na ukifanya hivo maumivu yatakuwa yanazidi kila saa". "kwani mi nilimdhulumu vipi Alwin" aliuliza kwa sauti iliojaa maumivu, "kwanza inabidi ukubali kama ulikuwa ukimpenda Alwin lakini kutokana na kuwa alikuzidi kiuwezo wa akili uliapa kutokuwa nae kama mpenzi wako, unakumbuka siku ya kwanza kukutana na Alwin nyumbani kwenu". "Ndio nakumbuka" alijibu Jestina. "siku ile Alwin alikushunda katika kitu ambacho uliamini hakuna anaekuweza hivyo tokea siku hiyo uliacha wivu wako wa kimasomo ukutawale lakini unajua alichijisemea Alwin baada kukuona unalia siku ile". "hapana sijui" alijibu Jestina, "sasa ni hivi baada Alwin kugundua kuwa ulikuwa ukilia kwa sababu amekushinda, aliapa kutokukuliza tena na kuahidi kuwa daima atakupa furaha". Jestina baada kusikia hivo alihisi maumivu makali sana moyoni mwake, huku akijisemea "kwanini Alwin".
**************************************
 
JESTINA-6

Kelele ziliendelea kusikika huku kila kichaa akiongea na kuimba anachokijua yeye isipokuwa mmoja tu ambae alikuwa kimya huku akiuwangalia ukuta alioandikwa kwa maandishi fulani kwa damu, maandishi hayo hayakufahamika kabisa isipokuwa jina moja tu ambalo lilikuwa juu kabisa na jina lenyewe lilikuwa ni JESTINA. Naam chizi huyo hakuwa mwingine bali ni Alwin ambae ubongo wake uliingia ufa baada ya kifo cha mwanamke aliempenda. Yeye pekee ndie aliewajuwa wahusika lakini alishindwa kusema kutokana na kuwa hakukuwa na mawasiliano kati ya akili na mdomo wake hivo hakuweza kuongea chochote kile. "inspecta Hans hapo utajisumbua tu, huyo hawezi kuongea" dokta alikuwa akimwambia inspecta huyo ambae ameifufua kesi ya mauaji ya Jestina iliotokea miaka kumi iliopita. "Asante dokta mimi sitaki kuongea nae bali nataka kujua tu kile alichokiandika kwenye ukuta, kivipi kinahusiana na kifo cha Jestina".
Alitoa camera ndogo na kupiga picha yale maneno, aliporidhika aliondoka na kurudi kituoni kwa ajili ya kuendelea na upelelezi. Inspector Hans ni afande machachari sana na ni kawaida yake kuona kila mtu anapata haki yake. Hivyo baada kuhamishiwa Mashvile alikutana na kesi hiyo ambayo ilishaafungwa muda mrefu. Lakini kutokana na ukaribu wake na profesa Alexander Harison aliombwa aifungue upya kwa kile alichoambiwa na profesa huyo kuwa "ili kumrudisha Alwin kama alivyokuwa zamani ni lazima kesi hii itatuliwe". Aliayakumbuka maneno hayo alioambiwa na rafiki yake huyo. Profesa Alexander alifanya kwa sababu ya mwanae Miryam ambae ilibidi amhamishe mji baada matatizo yaliotokea lakini pia alihofia mwanae kuchizika. Hivyo akaamua kuvalia njuga kesi hiyo ambayo ni ngumu kupita maelezo kutokana na kuwa mwenye ushahidi hawezi kuutoa.
Upande wa Jestina, "Jestina utarudi duniani kama mzimu, lakini jambo la kwanza ukifika ni kwenda kumwambia ukweli Alwin ili arudi katika hali yake ya kawaida ila kwa sasa huwezi kuonekana mpaka pale Alwin atakapokusamehe na kukubali kuwa wewe umekufa maana mpaka sasa ni mtu pekee ambae anaamini hujafa" Malkia Alina aliongea na kumueleza kila kitu Jestina. "Baada ya hapo muombe akupe damu yake kidogo kwa sababu damu yake itakufanya uweze kuonekana na kutoonekana na pia jitambue kuwa wewe si binaadamu tena" aliendelea kuongea, "sasa kama unasema siwezi kuonekana mpaka nipate damu yake, nitaongea nae vipi" aliuliza Jestina. "Njia pekee ni kuongea nae ni akiwa usingizini" Alijibiwa na papo hapo mwanga mkali ukatokea. Ulipotoweka alijikuta yuko pembeni ya mtu mwenye manywele mengi sana huku akionekana kama kichaa lakini alipomuangalia vizuri akagundua kuwa alikuwa Alwin. Basi alisogea mpaka pembeni ya kitanda na kupiga magoti, Alwin nae alianza kuota na katika ndoto yake alimuona mschana analia. Taratibu alimsogelea ili kjua nini kilichomsibu.
Alwin: mbona unalia, (lakini alipouangalia vizuri akagundua kuwa mschana huyo si mwengine bali ni Jestina, bila mategemeo alimkumbatia kwa ngvu huku machozi yakimtoka) mi nilijua tu kama hujafa.
Jestina: Alwin naomba unisamehe kwa yote nlokutndea, ukweli ni kwamba nilikuwa nakupenda lakini wivu wangu wa kimasomo ulinifanya nisikubali kuingia katika mapenzi na wewe. mambo yote nilioyafanya nilitaka nikuchanganye ili japo mara moja na mimi nikupite darasani lakini nikajikuta nimejichanganya mwenyewe.
Alwin: mi nilishaakwambia kama nishaakusamehe kwa kila kitu kilichotokea, sasa naomba tuinuke nikupeleke kwenu maana wazazi wako wanakusubiri kwa hamu.
Jestina: Haiwezekani Alwin mimi tayari nilishakufa muda mrefu sana, saa hivi nimepata nafasi ya kuja kulipa kisasi changu kwa wale ambao ndio chanzo cha kifo changu, lakini kwa sasa unaeniona ni wewe tu hivyo ntahitaji damu yako kidogo ili niweze kurudi katika hali yangu ya kawaida na kweza kuonekana pale nnapotaka mtu anione.
Alwin: (kwa hasira) damu yangu nitakupa lakini nakuomba uniahidi kitu kimoja, wale wote waliohusika na kifo chako na wao wafe vifo vibaya sana.
Aliokota kama chupa pembeni na kujikata mkononi, kisha akamzogezea mkono Jestina ambae aliushika mkono huo na kuanza kunya damu. Alwin akiwa usingizini alianza kupiga kelele kutokana na maumivu makali ya kichwa alioyaskia. Wale madakatari waliokuwepo zamu walifika katika chumba chake na kumuwahisha hospitali. Hali ya hewa ilibadilika ghafla na radi pamoja na ngurumo zikaanza kupiga zikiamabatana na mvua kali sana yenye upepo ambao si wa kawaida. Katika kaburi alilozikwa Jestina ilipiga radi kali sana na papo hapo Jestina akatokea juu ya kaburi lake huku macho yakiwa mekundu mithili ya damu. "Matt na wenzako jiandaeni kwani hata mungu hawezi wasaidia sasa, mtalipa kwa kile mlicho nitendea" alijisemea hayo kishaa akacheka kicheko kikali sana na kutoweka eneo hilo.
Harakati za kuokoa maisha ya Alwin zilianza punde tu alipofika hospitali huku madaktari wakijitahi kadri ya uwezo wao. Habari zilimfikia profesa Alexander Harison na bila kuchelewa alitoka kuelekea hospitali, dakika kumi baadae aliwasili hospitali na kutokana na cheo chake aliruhusiwa kuingia katika chumba ambacho matibabu ya Aklwin yalikuwa yakiendelea. Wakati huo daktari alikuwa na sindano ya usingizi mkononi, nia ilikuwa ni kumchoma Alwin ili alale kwa sababu ingemsaidia kukabiliana na maumivu lakini Profesa Alexander alipiga kelele kumzuia "usijaribu kumchoma hiyo sindano utamuua kabisa" aliongea profesa. Kisha akasogea mpaka pembeni yake na kuanza kumgusa sehemu mbali mbali za mwili wake "muacheni hivohivo, yupo katika wakati mgumu sana, akifanikiwa kupita wakati huu basi huenda akapona lakini pia kuna uwezekano kupoteza maisha kwa sababu anazinduka kutoka katika usingizi wa kifo" aliongea Profesa na kuwafanya madaktri wote wamshagae na swali kubwa lilikuwa anajuaje vile bila hata kufanya uchunguzi wa kitaalamu. Lakin hakuna aliemuuliza swali lolotea na waliamua kutoka hasaa katika chumba hicho na kumuacha peke yake akiwa na Alwin.
"Leo nataka nikuoneshe nina uwezo gani katika sita kwa sita" kijana Frank akiwa na mpenzi wake kwenye gari. Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana bila kuchukua tahadhari kama huo ulikuwa ni usiku na barabara ilikuwa imepita katikati kijipori kidogo. Wakati anaendesha alifungua zipu na kutoa uume wake "oyaa fanya huduma ya kwanza basi" alimwambia mpenzi wake, "we huoni kama ni hatari hiyo" alijibiwa. "acha uboya wewe sasa dereva si mimi, we utakuwa unaramba pipi mi ntakuwa naendesha" alijibu huku akimshika kichwa na kumuinamisha, kuona mpenzi wake kakomaa ilibidi amridhishe. Kutokana na raha kuna wakati Frank alifunga macho, lahaula alipoyafungua aliona mschana kasimama katikati ya barabara na katika harakati za kumkwepa gari ilimzidi na kuacha njia na kupinduka. Ilipotulia Franka alimuangalia mpenzi wake ambae muda mrefu alikuwa ameshakata roho, wakati akihangaika kujitoa akaona miguu kwa nje huku ikichuruzika damu nyingi sana tena yenye kutoa harufu mbaya sana.
Alipepesa macho ma alipoyafungua hakuiona tena, alijitahidi na kufanikiwa kutoka kwenye gari huku damu zikimtoka kichwani. Alianza kutembea taratibu huku akiskilizia maumivu lakini alihisi kama kitu kikimfata kwa nyuma, alipogeuka hakukuta kitu lakini apogeuka tena mbele uso kwa uso na mschana . "wewe ni nani" aliuliza huku akirudi nyuma maana kwa muonekano tu hakuwa mtu wa kawaida, "leo umenisahau" alijibiwa kwa sauti yenye kujirudia. Aliiskiliza kwa makini na ndipo sauti hiyo ikagonga vizuri kwenye ubongo wake "hapana, haiwezekani Jestina kashakufa" aliongea huku haja ndogo ikianza kumtoka. Na ndipo Jestina akaziondoa nywele zake usoni na kumfanya Frank atoe macho kama mjusi aliebanwa na mlango. "Utalipa kwa ulichokitenda, kifo" aliongea Jestina na kupotea, kushuhudia vile Frank alitoka nduki.
"Jestinaaaa...." Alwin alizinduka kutoka usingizini kupiga kelele huku akiliita jina la Jestina, kwa bahati nzuri Profesa Alexander alikuwepo hivyo alimuwahi na kumwambia atulie. Alwin alianza kulia kama mtoto mdogo "kweli Jestina wakufanyiwa vile", "tulia Alwin mimi nipo kwa ajili yako" aliongea Profesa huku akimbembelea. "kwanza nataka kumuona Jestina" aliongea Alwin huku akijaribu kusimama. "mwanangu huwezi kumuona tena", "kwanini" "Jestina ameshafariki na huu ni mwaka wa kumi tokea kifo chake" alijibu Profesa. Machozi yalizidi kumtoka Alwin huku akijilaumu kwanini aliruhusu Jestina wake afanyiwe unyama kama ule. Ilibidi profesa atumie njia za ziada kumtuliza mpaka alipohakikisha ameshaanyamaza, "sasa pumzika kesho utakwenda nyumbani kwani wazazi wako wanakusubiri kwa hamu" aliongea profesa na Alwin alikubali. Baada ya hapo profesa aliondoka na kuwaambia madaktari kuwa keshi atakuja kumchukua Alwin.
Wakati Alwin akiwa amepumzika huku machozi yakilowanisha mashavu yake, ghafla umeme ulizimika na papo hapo Jestina akatokea lakini alikuwa katika umbile lake la kibinaadamu "Jestina" Alwin aliita kwa uoga. "usiogope Alwin mimi siko hapa kukudhuru" Jestina alijibu. Alwin alijaribu kumgusa lakini mwili wa Jestina ulikuwa wa baridi sana. "wewe si ushakufa" aliongea Alwin, "ndio" alijibu Jestina "sasa kama umeshakufa hapa unafanya nini" Alwin aliuliza tena. "ndio hilo nnalotaka kukwambia, mimi nimepewa nafasi ya kuja kuwalipa wale wote walionifanyia ubaya kwa hivyo nakuomba uvumilie kwani wote watalipa vilivyo" aliongea Jestina huku machozi yakimtoka lakini hayakuwa ya kawaida zilikuwa ni damu zilizokuwa zikitoka machoni. Alwin alimshika mkono na kumwabia "mimi niko pamoja nawe na sito pumzika mpaka nihakikishe wamemalizika" kisha akamvuta ili amkubatie lakini Jestina alipotea na kujikuta akikumbatia hewa.
***************************
Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa. "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema". Kijana huyo hakuwa mwengine isipokuwa Frank ambae alionekana kuchanganyikiwa, "oyaa tuambie basi nani huyo anaetaka kukuua". "Jestina jamani" aliongea Frank na kuwafanya wenzake waanze kucheka, "wee hebu tuambie leo umekunywa ngapi" Jay aliuliza. "washkaji mimi sijalewa, amini msiamini nimemuona tena anatisha si mchezo" alijaribu kujitetea Frank lakini wenzake walizidi kumcheka. "oya hebu msindikize geto akalale kwanza labda pombe imepanda kichwani" Jay aliongea na watu wawili wakamchukua Frank mkukumkuku na kumpeleka chumbani. "oya dogo pumzika kwanza kesho asubuhi tutaongea fresh" James aliongea na kutoka, kwa bahati mbaya aliufunga mlango kwa nje.
Frank alijaribu kutafuta usingizi huku akijipa moyo labda kweli atakuwa kalewa lakini ghafla hali ya hewa ndani ya chumba hicho ilianza kubadilika. "ah hahahahahah......" sauti kali ya kicheko iliskika, "nisamehe Jestina, ujinga tu ulikuwa ukinisumbua" alianza kuomba msamaha. "hahahaha msamaha wako haukubaliki na leo utakiona cha moto" Jestina aliongea huku alizidi kutisha na kuanza kuangua kilio ambacho kilimbana na mruzi mkali uliopenya kisawasawa kwenye maskio ya Frank. Alianza kusikia maumivu makali sana, na damu ziianza kumtoka kwa wingi sana masikioni. "Jestina nakuomba unisamehe niko chini ya miguu yako" aliomba lakini ni kama alikuwa akiomba azidishiwe adhabu. Kwa makucha makubwa katika mikono ya Jestina alianza kumchanachana bila huruma, Frank alipiga sana kelele lakini hazikuskilikana kutokana na chumba hicho kuwa katika nyumba nyingine tafauti na ile waliokuwepo wenzake. Alikimbilia mlangoni kujaribu kujiokoa lakini wapi mlango ulikuwa umetiwa loki kwa nje. "unakwenda wapi unadhani" Jestina aliuliza kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, wakati huu alikuwa kashaabadilika na kuwa katika mwili uliokuwa ukitoka funza wengi na wenye harufu kali sana ya kuoza. Harufu hio ilimfanya Frank anze kutapika, mpaka aliishiwa nguvu. Jestina alimsogelea alipo na kumshika koo na kuanza kuliminya mpaka kulinyofoa kutoka shingoni. Frank aliaga dunia huku mwili wake ukiwa hautaminiki, kabla ya kutoweka aliandika ukutani kwa damu "AMELIPA".
 
JESTINA-7
Asubuhi ilifika na Alwin alikuja kuchukuliwa na profesa na safari ya kuelekea kwao ilianza, wazazi wake hawakuamini kama mtoto wao kapona hasa baba ake na kujikuta akimtwanga swali "miliioni saba laki sita hamsini na tano elfu mia mbili thalathini na moja gawa kwa mbili, jibu lake ngapi". "milioni tatu laki nane ishirini na saba elfu mia sita na kumi na tano" alijibu Alwin bila kusita na profesa akathibitisha jibu hilo. Kwa mara nyingine tena ndani ya miaka kumi furaha ilirejea ndani ya nyumba ya Mr Kelvin kwa kumpata mwanae Alwin. Machozi yaliwatoka wanafamilia hao huku wakikumbatiana kwa furaha iliopitiliza.
Asubuhi ilifika na kila mtu aliingia katika mishemishe zake, "oyaa Frank bado hajaamka" Jay aliuliza. "nahisi atakuwa bado maana jana nahisi kanywa nyingi sana" James alijibu, "nenda kamcheki basi" Jay aliongea na James aliondoka kuelekea chumba alicholala Frank. Baada dakika mbili James alirudi mbio huku akihema kwa nguvu, "oyaa nini wewe" Jay aliuliza. "Frank... Fra...nk" alijibu huku machozi yakimtoka, Ilibidi Jay na wengine wakimbie kuelekea chumba alicholala Frank. Wote walipigwa na butwaa baada kukuta damu zikiwa zimetapakaa chumba kizima huku mwili wa Frank ukiwa hautamaniki hata kuangalia. Jay alitoa simu na kuripoti polisi, haukupita muda gari ya polisi ilifika pamoja na gari ya kubebea wagonjwa. Mwili wa Frank ulitiwa kwenye gari na kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Inspecta Hans ndie aliekabidhiwa kesi hiyo, "habari yako kijana mimi naitwa Inspecta Hans na ndie ninae shughulikia kesi hii" alimwambia Jay ambae alionekana kuchanganyikiwa "hebu nieleze kila kitu bila kunificha". "ukweli inspector Frank alikuja jana usiku akiwa na majeraha kadhaa kichwani huku akipiga kelele kuwa amemuona Jestina". "Lakini Jestina si ameshakufa muda mrefu sasa" aliongea Inspector Hans lakini lengo lake ilikuwa ni kujaribu kutafuta ukweli kwa sababu kesi ya Jestina aliifungua tena. "mimi simjui Jestina ndio nani" alijibu kwa kitete huku akiangalia chini. "asante kwa ushirikiano wako nikikuhitaji tena nitakutafuta" aliongea inspector Hans na kuinuka kisha akamfata James ambae alikuwa kafunikwa shuka na mkononi akiwa na kikombe cha kahawa.
"habari yako kijana naitwa Inspecta Hans" alijitambulisha, "mimi naitwa James na ni rafiki mkubwa wa Frank", "Ok James naomba unieleze tukio lilitokea jana". Na yeye alieleza kama alivyoeleza Jay na pia alipoulizwa kuhusu Jestina alisema vile vile na waliobaki wote walisema vile vile.
Baada kumaliza kuwahoji alirudi kituoni kwa ajili ya kuendelea na harakati nyingine, lakini wazo lilimjia aende kwa Alwin huenda angepata pa kuanzia. Bila kuchelewa alitoka na kuelekea kwa Mr Kelvin. "habari za saa hizi mzee wangu na samahani kwa usumbufu, kwa jina naitwa inspecta Hans nina maswali mawili matatu kwa ajili ya Alwin" alijitambulisha na kueleza shida yake. Mr Kelvin ni muelewa sana alijua hilo litakuwa ni swala la usalama hivyo alimwita Alwin na kumwambia nia ya inspecta. "karibu inspecta na jiskie huru kuniuliza chochote na nakuahidi nitakupa ushirikiano" alieleza Alwin na kukaa kwenye kiti. "sawa kijana, nimekuja hapa kwa jambo moja tu. Profesa Alexander Harison alinipa kazi ya kufatilia kesi ya Jestina lakin kazi hii siwezi kuifanikisha bila msaada wako na najua ntakuwa nimekutonesha kidonda lakini naomba unisamehe kwa sababu nimesubiri kwa muda wote uliokuwa huko sawa" aliongea Inspecta.
"hapana Inspecta hujatonehsa kidonda, yaliopita yashapita tugange yajayo" alijibu Alwin huku akitabasamu. Kwa mtu wa kawaida angeweza kusema yuko sawa lakini kwa mtu wa mafunzo kama Inspecta Hans tabasamu hilo lilitafsiri mambo mawili moja lilikuwa ni chuki na pili kisasi. "sawa, sasa jana kumetokea kifo cha kijana mmoja anaeitwa Frank, nadhani unamjua". "ndio namfahamu vizuri", "ok, mpaka sasa kifo chake ni cha utata huku wenzake wakidai kuwa kimesababishwa na Jestina" aliongea. Alwin alitabasamu kidogo "unajua inspecta damu ya mtu haipotei bure, na huo ni mwanzo tu wamebakia kumi na tisa na leo usiku atakufa mwengine" alijibu Alwin huku machozi yakimtoka. "sasa anaefaanya mauaji haya ni nani" aliuliza inspector, "Jestina" Alijibu Alwin na kuachia tabasamu kubwa. Inspector akaona hakuna haja ya kuendelea kuuliza maswali , aliaga na kuondoka.
Hofu ilianza kutawala katika mioyo ya wale walioshiriki katika kifo cha Jestina kwa njia moja ama nyingine. Mazishi ya Frank yalifanyika huku wengi waliomjua walikwenda akiwemo Alwin ambae alioneka kutokuwa na huzuni kabisa. Baada ya kumaliza watu walianza kutawanyika, ila wakati Alwin anaondoka alishikwa bega na alipogeuka "Alwin unanikumbuka" aliuliza inspector Hans. "samahani mbona sijawahi kukuona" alijibu na kumfanya inspecta ashangae kidogo, "leo asubuhi nilikuja kwenu na tukaongea mambo fulani kuhusiana na kifo cha Jestina" alifafanua labda alihisi huenda akawa amesahau lakini bado Alwin alishikilia kuwa hamjui na kuomba aondoke zake. Inspecta alimruhusu huku akiwa na maswali mengi sana kichwani ambayo yalikosa majibu "ikiwa huyu yule sie Alwin sasa atakua nani" alijiuliza mwenyewe. Kwa mchana huo hali ilikuwa shwari kabisa, usiku ulianza kuingia na kila mtu akawa anamalizia biashara zake ili arudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko.
Sara ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimalizia shughuli zao, "Sara kwa heri tutaonana kesho" Bety alimuaga huku akitoka katika chumba cha kubadilishia nguo na kuondoka. Ghafla hali ya hewa ilianza kubadilika humo ndani, Sara alihisi kama kuna mtu mwengine humo ndani. "Sara....sara" alisikia sauti ikimuita lakini mtu hakumuona, alifunga kabati lake ambalo lilikuwa na kioo mbele. Alipoangalia vizuri aliona kuna mtu amesimama nyuma yake lakini alipogeuka hakumuona, sasa wasiwasi ulianza kumuingia moyoni. Mara akaanza kusikia vicheko na vilio, woga ulimpata na kuanza kukimbia kuelekea mlango wa kutokea lakini ghafla taa zikazimika na kumfanya ajikwae na kuanguka chini kama mzigo. "sara....sara.....sara" alisikia tena sauti ikimwita, "we nani" aliuliza kwa sauti ya kilio. "mimi ni kifo chako" alijibiwa na kuzidi kutetemeka, Sara alinyanyuka kutoka chini na alipogeuka aelekee mlangoni ndipo akamuona mwanamke amesimama mbele ake.
"wewe ni nani" aliuliza huku akiokota mbao pembeni, "leo hunijui si ndio" alijibiwa na kwa mbali sauti hio ikagonga kwenye ngoma za masikio yake. "lakini usijali nitakwambia" alijibiwa na ghafla akapotea na kutokea nyuma yake, "geuka" aliambiwa Sara na kuanza kugeuka taratibu na macho yake yakatuwa usoni mwa Jestina na hapo ndipo akamtambua lakini kabla hajafanya kitu alichezea kibao kizito na kuanguka chini "nisamehe Jestina" aliomba sara. "wewe hukunionea huruma na kuamua kuniziba mdomo si ndio" Jestina alijibu huku machozi ya damu yakimtoka. "sasa nataka nikuonyeshe maumivu niliyoyapata siku ile" aliendelea kuongea na ghafla Sara akawa hatoi sauti kwa sababu mdomo wake ulizibwa na kitu kama kipande cha nyama iliyooza. Kutokana na harufu kali ya kipande hicho Sara alianza kuhisi kutapika lakini matapishi hayakutoka kabisa, hali ilizidi kuwa mbaya huku yakianza kutokea puani na kumfanya akose pumzi. Jestina alikuwa mbele ya binti huyo ambae siku ile anabakwa yeye ndie alimziba mdomo ili asipige kelele. Haukupita muda Sara aliaga dunia kutokana kukosa pumzi muda mrefu, kama kawaida Jestina aliandika kwenye ukuta kwa damu "AMELIPA" kisha akatoweka eneo hilo.
Siku ya pili wale waliofika kazini mapema walishudia mwili wa sara ukiwa upo katika hali mbaya sana na pia kulikuwa na harufu kali ya kinyesi. Taarifa zilitolewa polisi na haukupita muda walifika sehemu ya tukio na kufanya kazi yao ikiwemo kuwahoji marafiki wa karibu na binti huyo. Baada ya hapo walirudi kituoni kuendelea na majukumu mengine lakini inspector Hans bado alikuwa njia panda asijue la kufanya. Sasa hofu iliongezeka kwa wale wote waliohusika na kifo cha Jestina "unajua mtu wangu sisi tulikosea sana" Jay alimwambia James. "oyaa acha uoga wewe lazima kuna mtu atakuwa anatufanyia uhuni tu" James alijibu. "inawezekana ikawa Alwin au maana tokea atoke hospitali ya vichaa mauaji yameanza" Jay aliongea. "kama vipi tumuibukie asilete mambo ya kijinga" James aliongea kwa hasira na wakakubaliana hivo. Safari ya kuelekea kwa kina Alwin ilianza na kwa sababu walikuwa na usafiri walifika mapema.
"Alwin yupo" Aliuliza Jay bila hata kutoa salamu, "nipo niwasaidie nini" Alwin alijibu mwenenyewe baada kuzitambua. Walimuomba atoke nje na yeye bila kupinga alitoka, "dogo sikia unajifanya mjanja si ndio" James alihoji kwa hasira. "kwani vipi mbona siwaelewi nyinyi" alijibu bila wasiwasi. "kama hutuelewi basi ngoja tutakuonesha" Jay alijibu na kumpa ishara James waondoke.
"James" Alwin aliita, alipogeuka akamuonesha ishara kwa kupitisha mkono katika shingo akimaanisha ni zamu yake usiku wa siku hio. Lakini alipotezea na kuondoka zake bila hata kugeuka nyuma, Alwin alirudi ndani moja kwa moja alikwenda chumbani kwake. "vipi wameshaondoka" Aliuliza Alwin, "ndio" alijibu Jestina akirudi katika umbo lake la kike. Huo ni mchezo wamekubali kuucheza huku Jestina akiitumia nyumba hiyo kama ngome yake na mtu yeyote atakaekuja kwaajili ya kesi yake basi hujibadilisha na kuwa Alwin. Na hicho ndicho alichokifanya siku ile alivyokuja Inspector Hans kwaajili ya mahojiano. Bado vifo vyote viwili vilibakia kuwa ni gumzo, daktari alieifanyia uchunguzi miili hiyo alikuja na majibu yale yale tu "yoyote aliefanya mauaji haya si kiumbe wa kawaida".
************************************
"Matt mwanangu kwanini uliamua kufanya ushenzi ule"
"Ah ni ushundani tu ndo ulionipelekea kufanya vile"
"sasa umeona madhara yake nimetumia mabilioni ya mapesa kuwahonga majaji na wanasheria waifute kesi ile"
"najua mzee, ila usijali kila kitu kipo sawa na muda si mrefu nitarudi nyumbani"
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya Matt na baba yake kwa njia ya simu, baada kufanya tukio lile ilibidi Matt asafirishwe na kesi ile iuliwe kwa aina yoyote. Sasa anataka kurudi akiamini miaka aliokaa nje ya mji wake ingetosha watu kumsahau na hata wenzake walikata mawasiliano nae kwa sababu aliondoka kimya kimya bila kuwataarifu wenzake chochote. Ni baada tukio lile alilomfanyia Jestina, Matt alisafirishwa na baba yake na kupelekwa Ufaransa.
"Baba naskia Alwin kapona" aliuliza Miryam, "ndio mwanangu kapona kabisa" Profesa Alexander Harison alijibu." Ah basi mimi namaliza mtihani wangu wiki ijayo baada ya hapo nitakuja, lakini usimwambie kitu Alwin" aliongea Miryam kwa furaha sana. Miryam hakuweza kuendelea kusoma Mashvile baada lile tukio na lilisababisha kifo cha Jestina pamoja na kichaa cha Alwin. Na baada baba yake kugundua hilo aliamua kumsafirisha kwa ajili ya kwenda kumalizia masomo yake nchini China na huo ndio ulikuwa mwaka wake wa mwisho wa masomo. Lakini haikupita hata siku moja bila kumuombea uzima Alwin.
 
JESTINA-8

Bado inspecta Hans alikuwa njia panda maana aliona kama Alwin anamchezea mchezo mchafu, baada kufikiria sana bila kupata majibu aliamua kwenda nyumbani kwa Profesa Alexander Harison kwa ajili ya kuripoti alichokiona. Safari yake ilikuwa ni ya dakika kumi tu, alipofika alikaribishwa ndani na kuomba kuonana na Profesa. Haukupita muda aliambiwa aingie katika ofisi, "samahani kwa kuja bila taarifa" aliomba msamaha kwanza, "bila samahani". "ukweli kuna jambo linatitaza, kwa sababu jana nilienda kuongea na Alwin lakini nilipokutana nae msibani alisema hanifahamu na wala hatujaongea kitu" alieleza, " wakati unaongea nae majibu yake yalikuaje" aliuliza profesa. "yalikua yenye chuki ndani yake na baadhi yalikuwa ya mkato" alijibu. "Alwin hana majibu ya mkato, ni kijana ambae majibu yake yanaheshima" aliongea profesa na kumshtua kidogo inspecta Hans ambae sasa alishaanza kuamini kama hakuongea na Alwin, sasa swali lilikuwa aliongea na nani kama si Alwin. "na kuhusu mauaji yanayotokea, mpaka sasa ripoti zinasema kuwa si ya kawaida" alijikaza na kuendelea kuongea. "naweza nikaziona picha za miili yao" aliuliza profesa. "ndio" kisha akatoa fail na kumkabidhi profesa.
Profesa aliziingiza kwenye mashine fulani hivi kama projecta na kuzima taa zote katika ofisi yake kusababisha kigiza fulani hivi, kisha akaiwasha ile mashine na zile picha zikawa zinaonekana ukutani. Lakini aliganda kidogo akiangalia alama za kucha katika miili yote miwili na kubaini kuwa alama hizo zimepigwa katika mtindo mmoja. Haraka alifungua droo na kutoa picha ya ile michoro alioandikwa Alwin kipindi ambacho allikuwa hayuko sawa na kuanza kulinganisha. "unaona kitu gani hapo inspecta" aliuliza profesa, "mi naona michoro tu" alijibu. "angalia kwa makini" alisisitiza profesa ndipo inspecta Hans aliposimama na kusogea kwenye ukuta na kuanza kuzichunguza kwa makini sana. Aligundua kuna maandishi fulani hivi lakini alishindwa kuyasoma "naona kama maandishi hivi" aliongea inspecta. "ndio katika miili yote miwili kuna jina limeandikwa lakini katika lugha ya kale ya wenyeji wa Mashvile na jina hilo ni JESTINA" aliongea profesa na kumfanya Inspecta kutumbua macho kama mtu aliesakamwa na tonge la chakula kwenye koo. "unataka kunambia kuwa muuaji ni JESTINA au vipi" aliuliza kwa sintofahamu, "ndio inspecta muuajai ni Jestina, hivi umewahi kusikia kama kuna ulimwengu wa watu waliodhulumiwa" alijibu profesa na kuuliza. "ah mi hizo story huwa nazisikia tu lakini siamini kabisa" alijibu inspecta huku akitabasamu, "basi kuanzia leo ndio uamini kama kweli huo ulimwengu upo na mtu akifa kifo cha kudhulumiwa basi hupita hapo kwanza na hukaa kwa muda wa miaka kumi. ikiwa ndani ya kipindi hicho kutakuwa na mtu duniani ambae anaamini mtu huyo amedhulumiwa na haki haijatendeka basi hupata uwezo wa kurudi duniani kuja kuwalipa wale waliomdhulumu" aliongea na kufafanua Profesa "inspecta kazi yako imekwisha sasa kwa sababu hakuna utakalofanya kumzuia Jestina asilipe kisasi. Wewe kazi yako itakuwa ni kushuhudia tu mauaji hayo" aliongea profesa na kuonekana kama kufunga kikao hicho.
*****************************
Sauti za huba ziliskika ndani ya chumba kimoja katika hoteli kubwa katika mji wa Mashvile, "James niahidi kama utanioa". "niamini wewe ni wangu na kesho nakupeleka nyumbani nikakutamblishe kwa wazazi wangu" James alijibu huku akionekana kunogewa na penzi la mschana huyo, ndani ya chumba hicho taa zilikuwa zimezimwa isipokuwa taa moja nayo ilikuwa ikitoa mwanga hafifu sana na kukifanya chumba hicho kipendeze. Kuna wakati James alifunga macho kwa raha alioipata, alipofungua alijkuta akimuachia mpenzi wake na kuruka pembeni. Hiyo ni baada kuona sura ya Jestina badala ya mpenzi wake, "James unanini mbona umenikata stimu" aliongea mwanamke huyo kwa kudeka. "ah hamna kitu" alijibu kwa kujibabaisha na kurudi kitandani ili aendelee na mchezo, wakati akiendelea kufanya hivo aliangalia dirishani na kumuona Jestina akimuangalia. "mama" alipiga kelele huku akimsukuma mpenzi wake kwa nguvu na kusababisha ajigonge kichwa kwenye kona ya kitandana na kuanza kutoka damu nyingi na mwisho alitulia tuli. Kicheko kikali kiliskika na kufuatiwa na maneno "na bado utajuta kuzaliwa" kisha kimya kikatawala ndani ya chumba hicho. Alipoona hali imerudi kuwa ya kawaida alimsogelea mpenzi wake na kumtikisa lakini wapi, muda mrefu alikuwa kashapoa. Woga ulimpata na kuamua kuvaa na kuondoka eneo hilo na kuuwacha mwili wa mpenzi wake ukiwa umetapakaa damu.
Asubuhi mapema akiwa kwao, gari ya polisi ilifika na kuonyesha waraka wa kukamatwa James, hakukuwa na jinsi zaidi ya kukubali na kufikishwa kituoni. Alihojiwa kidogo lakini hakutaka kuonyesha ushirikiano, hivo ikatoka amri awekwe mahabusu mpaka atakapokuwa tayari kusema. Masaa yalikatika na hatimae usiku ulifika bila kukubali kuongea chochote. Akiwa kajilaza kwenye kigidoro kidogo, "James...James...hahaha" aliskia sauti ikimwita lakini hakumuona mtu. "Jestina dadangu naomba unisamehe, ujinga tu ulikuwa ukinisumbua" alianza kuomba msamaha huku akilowanisha suruali yake. "mpumbavu mkubwa wewe nani dadaako, kuna mtu anaeweza kumshika dadaake ili abakwe" Jestina alijibu kwa hasira na kumtokea mbele yake. "mamaaaa nakufa" James aliruka huk akipiga kelele, lakini ghafla Jestina akatoweka na kumtokea nyuma yake.
Aliinua mkono wake na kumtandika kucha za mgongo na kumfanya apige ukwenzi wa maumivu. Kwa kweli James alijua hicho ndio kiama chake maana kila alivojaribu kujitetea ni kama alikuwa akichochea moto. Jestina aliendelea kumrarua mpaka alipohakikisha amemmaliza kabisa, kuhakikisha haishi tena alikpiga kucha za koromea na kulikata. Kama kawaida yake aliacha ujumbe na kutoweka, siku ya pili asubuhi maaskari waliripoti kifo cha James. Wengi walishtuka hasa waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kifo cha Jestina. Hali hiyo haikuwatisha wao tu bali mpaka watu wengine ambao hawakujua chochote juu ya matukio hayo. Kila kukicha vyombo vya habari vilitangaza mauaji mapya yanayofanyika hukua ikiaminika kuwa muuaji ni mtu ambae amebobea na anauwa kwa sababu ya kulipa kisasi. Kama kawaida inspeta Hans alirikodi tukio hilo katika mafaili yake na kuondoka. Sasa hakuumiza sana kichwa kwa sababu alishajua muuaji sikiumbe wa kawaida.
Upande wa Alwin hali yake ilizidi kutengemaa na sasa mwili wake ulishaanza kurudi na vidonda vidogo vidogo vilishaanza kukauka. Familia yake ilifurahi lakini haikuwa hivyo kwa familia ya Jestina ambayo bado walikuwa ni wenye majonzi sana hasa kwa kumpoteza mtoto wao pekee. Hilo lilimuathri sana mama yake na kupelekea baadhi ya wakati kuzimia kutokana na msongo wa mawazo. Hata baba yake pia ilimathiri na kupelekea kudhoofika kimwili japo si sana. Siku hiyo Alwin alipanga kwenda kuwatembelea ili kuwajulia hali, aliondoka kwao asubuhi mapema na kuelekea kwa Mr Hendrix. Alipofika alikaribishwa ndani vizuri na mfanya kazi kisha akaenda kuitwa Mr Hendrix. Alifurahi sana alipomuona Alwin na kumkumbatia "Mungu ashukuriwe kwa kukupa uzima mwanangu" aliongea huku akijizuia machozi yasitoke. "asante, habari za siku nyingi" Alwin aliuliza, "kama unavoziona mwanangu, kwa kweli tokea Jestina atutoke maisha yetu yamekuwa magumu sana sijui hata kwanini Mungu ametutenda kiasi hichi" Alijibu Mr Hendrix na wakati huu alishindwa kuyazuia machozi na kuyaacha yatiririke kuonyesha machungu alokuwa nayo.
"hapana mzee wangu usiseme hivo, Mungu hajawatenda ila amekupeni mtihani kama alivowapa wengine tu ili kukupimeni imani. Yeye ndie aliewapa Jestina na yeye ndie aliemchukua kwani kuna ubaya gani mtu kuchukua kilichochake. Nyie jueni tu kama Jestina amepumzika lakini hatopata amani ikiwa bado mtaendelea kumlaumu Mungu kwa kifo chake" Alwin aliendelea kumliwaza Mr Hendrix ambae alikuwa akilia kama mtoto mdogo. "mwangu we huujui uchungu nlokuwa nao, kifo cha Jestina kimepelekea mpaka mamaake kupata maradhi ya kuanguka. Ukweli Alwin naogopa kumpoteza mke wangu" Alwin alivyosikia hivo alishtuka kidogo na kuomba kwenda kumuona. Bila kinyongo Mr Hendrix aliongozana nae mpaka chumbani, alimkuta akiwa amelazwa huku akiwa amewekwa drip. Alwin alisogea mpaka pembeni yake na kukaa kwenye kiti "habari yako mama" aliongea kwa sauti ya chini. "nashkuru sijui wewe Alwin" alijibu mama huyo japo kwa tabu kidogo. "pole kwa yote yaliotokea", "asante mwanangu, kwanini lakini" alijibu huku akilia. ""pole kwa yote yaliotokea", "asante mwanangu, kwanini lakini" alijibu huku akilia. "yote ni kazi ya Mungu na kama tunavojua kazi ya Mungu haina makosa cha msingi mamaangu kukubaliana kama Jestina hayupo tena nasi" Alwin aliongea huku akimshika mkona mama Jestina kwa ajili ya kumliwaza.
"kwanini waliamua kumfanyia ukatili mwanangu, aliwakosea nini" aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka. "usijali mama wote waliohusika na kifo cha Jestina watalipa kutokana na dhambi waloifanya" Alwin aliongea huku hasira zikizidi kumpanda lakini alijitahidi kuzizuia. "nakuahidi mama nitakuletea Jestina mwengine, nipe muda tu mpaka mambo fulani yakamilike" aliongea Alwin na kumfanya mama huyo aachie tabasamu kwa mbali. Waliongea mambo mengine mengi huku kwa muda wakisahau machungu yote ya mambo yaliotokea. Baadae Alwin aliaga na kuondoka na kurudi kwao, moyo wake ulifarijika sana kuonana na familia ya Jestina. Hata wazazi wake waligundua furaha alokuwa nayo na wala hawakujali kumuuliza chochote kile.
***************************
Baada ya kifo cha James waliitana karibu wote wale waliohusika na kifo cha Jestina, "jamani natumai mtakuwa mnajua nini kilichotukutanisha hapa" Jay aliongea baada kikao hicho kilichokuwa na waschana sita na wavulana kumi na moja. "tumeshazika wenzetu watatu, na hatujui atafuata yupi" aliendelea kuongea. "lakini kwa nini tulishiriki kitendo kile" aliongea mschana mmoja alieitwa Christina, "hakuna muda wa kulaumiana saa hivi jambo lile ndo lilishatokea kilichobaki ni kutafuta suluhishi kwa hili linalotukabili sasa hivi" aliongea kijana mwengine alieitwa Mark. "lakini wewe, James, Jay na Matt ndo mloyataka" aliongea mschana mwengine alieitwa Jesca. Walianza kulumbana huku kila mmoja akitafuta wa kumtupia lawama, "sasa mukigombana hivo ndio mtafikia suluhisho, hebu acheni upuuzi wenu" alifoka Jay na wote wakanyamaza kimya. "cha msingi hapa ni kumjua muuaji ni nani" aliongea Jay na kuwashangaza wote. "kivipi wakati muuaji ni mzimuwa Jestina" alijibu Jesca, "kwanza subiri niwaambie kitu, mimi hasa siamini kama mtu akifa anarudi tena duniani eti akiwa mzimu" aliongea Jay. "cha msingi hapa kwanza tuanze kumfatilia Alwin kila anachokifanya, mi nahisi kama si yeye anaefanya mauji basi atakuwa anamjua muuaji ni nani" Aliongea Jay kwa kujiamini.
"oyaa we umekunywa mchana wote huu mtu wangu" aliongea kijana mwengine alieitwa John, "unadhani boya kama yule anaweza kufanya mauaji, hivi we unadhani kuuwa ni kitu cha mchezo" aliendelea kuongea. "hivi nyie hamjiulizi kwanini mauaji haya yameanza baada Alwin kutoka hospitali ya vichaa, kwanini kipindi chote cha miaka kumi hakujatokea matukio kama haya" aliendelea kuongea Jay na sasa maneno yake yalianza kuleta maana ndani ya vichwa vya wenzake. "hapo kidogo inaanza kugonga ndani ya kichwa changu" aliongea Mark kisha akaendelea " sasa tunafanyaje". "hapo ndio kwenye shughuli yenyewe, inabidi tuanze kufanya uchunguzi chini kwa chini mpaka tuapate ukweli" aliongea Jay na kisha wakaanza kupanga mipango ya kuanza kufanya uchunguzi huku kila mmoja akipewa jukumu lake. Baada ya maongezi ya muda mrefu waliagana na kila mtu alikwenda zake kwao.
**************************
 
JESTINA-9

Jesca akiwa chooni anaoga ghafla moshi ulianza kutanda chumbani kwake, na ulipotoweka alianza kuhisi maji ni mazito sana na alipoangalia vizuri alijikuta anaoga damu. Alipiga kelele kwa nguvu huku akitoka mbio chooni, alianza kusikia sauti za ajabu ajabu zikinong'ona. "we nani" aliuliza kwa nguvu, "Jesaca siku yako ndio leo" aliiskia ikimjibu, "utalipa kwa ulichokitenda" yalizidi kusikika maneno. "unadhani mi nakuogopa, kama unajiamini jitokeze mbele yangu" aliogea kwa kejeli. ghafla taa zikazimika na kuwaka, mbele yake alisimama Jestina huku damu nyingi zikimtoka. Sasa Jesca aliamini kama ule ni mzimu, alianza kupiga kelele huku akikimbilia mlangoni kwa ajili ya kutoka lakini mlango haukufunguka. "nimekoma nisamehe Jestina" alianza kuomba msamaha, "siku ile wakati unafurahia tukio lile hukujua kama ulikuwa unakosea" Jestina alijibu huku akimsogelea na kumkaba koo. Jesca alianza kutapatapa huku akijaribu kupiga kelele lakini hazikutoka. Kwa nguvu Jestina alimrusha ukutani na kumbamiza, alimsogelea na kumtandika makucha mara kadhaa. Jesca alipoona hali mbaya, alijinyanyua na kukimbilia dirishani. Kwa nguvu alijirusha na kuvunja kioo, kwa vile chumba chake kilikuwa gorofani alianguka mpaka chini na kupasuka kichwa na hapo ndio ukawa mwisho wa Jesca. Hali ilirudi kuwa shwari na Jestina alitoweka huku akiacha ujumbe anaouwacha mara zote baada kufanya mauaji.
Kishindo kiliskika na majirani pamoja na wazazi wa Jesca walitoka lakini hali waliokutana nayo iliwafanya washangae, Jesca alikuwa chini huku damu nyingi zikitapakaa sehemu alioangukia. Simu zilipigwa polisi na muda si mrefu walifika eneo la tukio, Inspector Hans alifika kuchelewa lakini alifanikiwa kuona mwili kabla haujapelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi zaid. Aliwahoji wazazi wa Jesca kama wanajua lolote kuhusiana na kifo cha Jesca lakini walikuwa hawajui chochote. Basi baada taratibu zote kufanyika mwili wa Jesca uliingizwa kwenye gari na kupelekwa hospitali kwaajili ya uchunguzi zaidi. Vifo hivo viliendelea kuacha gumzo kwa watu wote, hasa watu wa usalama maana kila walipojaribu kuchunguza waliishia kwenye mambo ya mizimu jambo ambalo wengi hawakukubaliana nalo. "jamani sisi tunaonekana wapumbavu sana" aliongea mkuu wa kituo cha inpector Hans, "tukimuacha huyu muuaji atasababisha kuachishwa kazi" aliendelea kuongea.
"mnajua sisi wote tulikosea mwanzo" aliongea inspecta Hans na kuwashangaza wote, "unamaana gani kusema hivo?" aliuliza mkuu wao kwa mshangao. "nina maana kuwa mauaji yote haya yanahusiana na kesi iliyotokea miaka kumi iliopita" aliendelea kufafanua inspector. "Kwahiyo unamaanisha haki haikuyendeka katika kesi ile au" aliuliza kwa hasira mkuu wake. "kwa kweli mkuu sasa itabidi heshima nieke pembeni sasa maana unataka kunifokea bila msingi, kesi ile ulikabidhiwa wewe na ushahidi wa kutosha kuwa Jestina alibakwa na mwanaume zaidi ya mmoja akiwemo mtoto wa mheshimiwa waziri mkuu Matt, lakini kwa tamaa zako binafsi ukala pesa na kukanusha ushahidi badala yake ukasema kuwa aliebaka ni Alwin. ulifanya hivo makusudi kwa kuelewa kuwa Alwin asingeweza kusema lolote kwa sababu alirukwa na akili. Sasa vyote vinavyotokea leo ujue na wewe umehusika. Na kama nilivokwambia nimekukera basi fanya unalotaka" alimaliza kuongea Inspector Hans na kutoka katika chumba hicho cha mikutano.
***********************************
(miaka kumi iliyopita)
"asante sana inspector kwa kufika hapa japo nimekushtua" aliongea baba yake Matt, "kwa wewe muheshimiwa hata kama ningekuwa nimelala basi ningeamka na kuja" aliongea inspectar Brandon. "sasa inspecta ni hivi kuna kesi umepewa uisimamie lakini kwa bahati mbaya sana kesi hiyo na mwanangu anahusika" aliongea Waziri mkuu ambae ndio baba yake Matt, "una maanisha kijana wetu Matt anahusika na kifo cha Jestina" aliuliza inspecta kwa mshangao. "ndio inspecta, sasa nataka unisaidie kitu kimoja", "kitu gani hicho". "nataka hiyo kesi ife na ikiwezekana ushahidi upotee kabisa au tafuta yoyote tu umbambikizie" aliongea waziri huku akisogeza bahasha iliovimba. "lakini unajua muheshimiwa kazi hiyo ni ngumu sana" aliongea inspecta huku akiimezea mate ile bahasha. "ah halafu ukifanikiwa kufanya hivyo nitaandika barua rasmi upandishwe cheo" aliongea waziri na kuzidi kutia tamaa inspecta Brandon. kuskia hivo aliinuka haraka na kuchukua ile bahasha kisha akasema "usijali mzee nitahakikisha kesi inakwisha mara moja" na kuondoka. Waziri alitabasamu na kujisemea "hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa".
Inspecta Brandon alirudi kituoni huku akipanga jinsi ya kuizima kesi hiyo, alikuwa na mawazo mengi sana kichwani hasa alipofikiria kupandishwa cheo. Alitumia mbinu zote anazozijua mpaka akafanikiwa kupotosha ukweli wa kesi hiyo na kumsingizia Alwin kuwa ndie aliefanya jambo lile. Habari za kukanushwa kesi hiyo zilimfikia profesa Alexander Harison, alisikitishwa sana lakini hakukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali tu. Wakati wote huo Alwin alikuwa hospitali hajitambui kwa maneno mengine alikuwa amerukwa na akili. Na kutokana na hilo kesi hio ilifungwa moja kwa moja na hivyo Matt na wenzake kuwa huru. Baada ya tukio hilo ndipo waziri mkuu akaamua kumuondoa kwa muda mtotot wake huku Inspecta Brandon akipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo chake jambo ambalo hata wenzake hawakujua limetokeaje lakini hakuna alieuliza.
***********************
(baada miaka kumi)
"Profesa tayari wameshaakufa wanne lakini bado hakuna aliekuwa tayari kukubali kuhusika na kifo cha Jestina" alisema Alwin wakati akiwa anaongea na profesa. "tulia kijana madhali hawataki kusema wacha Jestina alipe kisasi kwa kuwauwa mpaka pale watakapokubali kusema ukweli" Aliongea profesa huku akitabasamu. Maongezi yao yaliendelea kwa muda mrefu sana mpaka mwisho walikubaliana wakutane baada wiki moja kujadili tena swala hilo. Baada ya hapo kila mmoja aliondoka na kuelekea nyumbani kwake, lakini Alwin alipita makaburini na kuzuru kaburi la Jestina. "natumai umepumzika kwa amani mpenzi wangu, usijali watalipa kwa kile walichokufanyia" aliongea Alwin na kuweka ua juu ya kaburi la Jestina na kisha akaondoka zake. Jay na wengine waliendelea kumfatilia Alwin wakiamini yeye ndie muuaji na Alwin tayari alishawashtukia hivo kupita kaburini kwa Jestina ilikuwa ni kuwachanganya wanaomfatili pasi na kujua kumbe wao pia wanafatiliwa na Alwin.
"unajua mke wangu Alwin kabadilika sana siku hizi" aliongea Mr Kelvin kumwambia mkewe, "kivipi mbona mi namuona yupo kawaida tu. "hapana mke wangu mi nakwambia tena Alwin kabadilika sana tokea atoke hospitali ya vichaa" alisitiza Mr Kelvin. "mhh haya lakini mi namuona kawaida tu isipokuwa siku hizi kachangamka sana tafauti na zamani" aliongea mama Alwin huku akiachia tabasamu akionesha kufurahishwa na mabadiliko ya Alwin. Wakati wakiendelea kuongea Alwin aliingia na kuwasalimia, waliitika kwa pamoja na baadae Alwin akaenda zake chumbani kwake.
Kwa upande wa inspecta Hans baada ya kutoka kwenye kikao alikwenda nje na kutulia huku akili ikitafakari mengi sana, akiwa dimbwi hilo la mawazo aliskia akiitwa na alipogeuka alikutana na mkuu wake wa kituo inspecta Brandon. "nifuate ofisini" aliongea na kuondoka, bila kusita aliinuka nae akamfuata nyuma mpaka walipofika ofisini. "bwana mdogo chunga kauli zako" hayo ni maneno ya kwanza yaliotoka kinywani mwa inspecta Brandon, "wewe hapa kituoni unaongea vile kama nani" aliendelea kuongea kwa hasira. "samahani mkuu, ule ndio ukweli we unadhani dunia bila haki ipo sawa. Hata waliokufa nao wanataka haki zao, we ulielewa fika kama Matt na wenzake wako hatiani lakini ukaibaitilisha kesi na kumuuzia Alwin. Natamani huo mzimu siku moja ukutembelee na wewe uone machungu ya kudhulumiwa" alijibu inspecta Hans bila woga wowote ule. "sasa unaonekana umeota mapembe si ndio" aliongea inspecta Brandon, "kama ndivyo unavofikiri sawa tena makubwa sana" alijib inspecta Hans na hakusubiri neno jingine kutoka kwa mkuu wake aliondoka maana hata yeye hasira zilishaanza kumpanda. Alimuacha mkuu wake akiwa ni mwenye mawazo tele lakini akaona bora apotezee tu.
Kifo cha Jesca kiliwachanganya wengi miongoni ya waliotenda kosa lile, wapo walioomba usiku usiingie maana walijua Jestina hufanya mauaji yake usiku. Lakini kwa vile hatuwezi kuzuia masaa basi muda uliyoyoma na hatimae kiza kikaana kutanda angani, hatiame usiku uliingia lakini kulikua na mvua kali sana iliondamana na ngurumo pamoja na radi. Usiku huo ulivo ulitosha kuwatisha wengi sana, Mark ndo alikuwa akitoka zake mihangaikononi kwake kuelekea nyumbani kwao ghafla akiwa njiani umeme ukazima.
Hali hiyoilimshtua kidogo Mark lakini akajipa moyo kuwa ameshaakaribia nyumbani kwao, hivyo basi alianza kukazana huku akiangalia pande zote kama kuna kitu ama mtu anamfuata. Nyumba yao ilikuwa imejitenga kidogo kutoka katika makazi ya wtu wengine, aliacha njia kubwa na kuingia njia ndogo ambayo ilikuwa nampeleka mpaka kwao. Wakati akikazana kwa mbali mbele yake akaona kama mtu kapita mbio. Moyo ulianza kumuenda mbio maana alishaanza kuziona dalili za mauzauza, akiwa anatetemeka ghafla alihisi kama kitu kimepita nyuma yake. Aligeuka kwa kasi lakini hakuona kitu, alipogeuka tena mbele kwa mbali akaona mtu akiwa anakuja upande wake taratibu . Kidogo alipata matumaini na kuanza kukazana kumfata yule mtu. Lakini alivomkaribia mwili ulimsisimka na kuhisi kama hakuwa mtu wa kawaida lakini alipiga moyo konde na kunyongea kwa mendo wa haraka. Ghafla tochi yake ilizima, na ilivowaka alikutana sura ya ajabu sana mbele yake. Aliruka na kuiangusa tochi pembeni, japo kulikuwa na baridi lakini kijasho kilianza kumtoka kwa wingi. "maumivu...." alisikia sauti ikitamka neno hilo kwa sauti a kuning'ona, "leo utahisi maumivu nilioyapata" sauti hiyo iliendelea kuongea huku ikizidi kuwa kali. "unataka nini lakini" aliuliza Mark kwa woga, "nataka roho yako" alijibiwa na wakati huu sauti aliifahamu vizuri sana kama ilikuwa sauti ya Jestina.
Aliokota tochi yake na kuanza kukimbia, lakini hakufika mbali alishtukia akichezea kofi zito la uso lililomfanya aanze kuona mawenge kidogo na kuanguka chini. Mark alijua kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wake, "nisamehe Jestina" alianza kuomba msamaha kwa kilio huku damu zikimoka mdomoni. "leo unalia mshenzi mkubwa wewe, siku ile ulikuwa ukicheka" Jestina aliongea na kumnyanyua Mark. Sasa alifanikiwa kumuona uso kwa uso, macho yalimtoka Mark asijue nini la kufanya. Wakati akiendelea kutumbua macho alirushwa kwa nguvu, kabla hajakaa sawa alichezea makucha kadhaa ya mgongo na kumfanya apige kelele za maumivu. "nimekoma naomba unisamehe" aliongea huku akisimama, "nikusamehe kweli, hivi unajua ni maumivu kiasi gani niliyapata siku ile" Jestina alijibu na kumtokea Mark mbele na kumkaba, kisha sura yake ilianza kubadilika na kuwa ya kutisha sana huku damu nyingi zikichuruzika kutoka machoni mwake kama machozi. Mabadiliko hayo yaliambatana na harufu kali sana ya kuoza, kwa nguvu alimpiga Mark na chini kiasi cha kushndwa kuinuka. "leo utakiona cha moto mpumbavu mkubwa wewe" aliongea Jestina na kisha akamfungua mdomo Mark na kumtia funza. Yeye alikaa pembeni akimuangalia kwa jinsi funza wanavomteketeza Mark. Hawakuwa funza wa kawaida kwani punde baada ya kutiwa mdomoni walianza kutoboa sehemu mbalimbali za mwili wa Mark na kusababisha maumivu makali sana. Mark alipiga sana kelele lakini hakuna msaada wowote alioupata mpaka mwisho alitulia tuli na kuaga dunia. Jestina alipotea eneo hilo akiacha ujumbe wake wa kawaida.
 
JESTINA-10

Asubuhi taarifa ya kwanza ilikuwa ni kifo cha Mark, huku ikisema bado mauaji hayo hajulikani yanasababishwa na nani. Lakini kilichowashtua watu ni kwamba wote waliokufa walikuwa ni marafiki tokea zamani sana, hivo kukaibua maswali mengi sana. Kituo kimoja cha televisheni kiliomba kufanya mahojiano na mwalimu mkuu wa shule ambayo inaaminika kuwa wote waliokufa wamesoma pale.
"habari yako mwalimu"
"nzuri nashkuru"
"kwa jina naitwa Anita ni mwandishi wa habari kutoka J76 news chanel"
"mimi naitwa Anthon Dickson, ni mwalimu mkuu hapa"
"naam mwalim unazungumziaje matukio haya ya mauaji yanayoendelea hapa mjini hasa ukizingatia wote walipoteza maisha mpaka sasa ni wananfunzi wako"
"kwa kweli ni vigumu kueleza"
"kivipi mwalimu"
"unajua ndugu Anita hapa kulitokea kesi kubwa sana ya ubakaji kama utakuwa unakumbuka, ni takriban miaka kumi sasa imepita na inavosemekana kuna wananfunzi wamehusika na tukio hilo"
"unaweza kuwataja"
"hapana siruhusiwi kufanya hivo"
"na kwanini hasa ukawa unahisi kama mauaji yanayofanyika sasa ya uhusiano wowote na kilichotokea miaka kumi nyuma"
"Unajua tulivokuwa wadogo, tulikuwa tukisimuliwa mambo mengi sana ambayo wengi wetu hatuyaamini"
"kama yapi"
"kwa mfano najua utakuwa umesimuliwa kuhusu ulimwengu wa watu waliodhulumiwa"
"ndio lakini hizo ni hadithi za kufikirika tu"
"hapo ndio kwenye utata sasa na hilo ndilo linalotokea saa hivi, baada kufanyika tukio lile kesi ilipelekwa mahakamani lakini cha ajabu ilizimwa haraka na watuhumiwa wakaacha huru, kwa sababu haki haikupatikana, sasa aliedhulumiwa amerudi kuja kuitafuta haki kwa mikono yake kama tunavojua HAKI ISIPOPATIKANA KWA AMANI BASI ITAPATIKANA KWA VITA. Na hii ni vita ambayo hakuna mtu yoyote kati yetu anaeweza kuizua na kama huamini kama mizimu ipo heebu jaribu siku moja kuuwa halafu uachiwe huru uone kama hutokipata walichokipata hawa vijana walikufa"
Mwalimu mkuu alimaliza kuongea na kuomba kuondoka akaendelee na majukumu mengine ya kawaida. Na kwa sababu kipindi hicho kilikuwa hewani live kila mtu alishuhudia, "ni bora wafe tu ili watu wajue kama haki ya mtu ni mali", "pumbavu nani atakaa aamini upumbavu ule". "mmmh makubwa mi nlijua ni hadithi tu za kufikirika", hayo ni baadhi ya maneno yaliokuwa yakisemwa na baadhi ya watu kila pahali. Kwa kweli story ilikuwa ni hiyo tu kila kona unayopita, Alwin ni miongoni mwa watu waliokiona kipindi hicho na kufurahia sana majibu ya mwalimu, yalitosha kupeleke ujumbe kwa wote ambao wanacheza na haki za watu.
"jamani hali imezidi kuwa mbaya sasa" Jay aliongea katika kikao kifupi cha dahrura kilichoitisha baada ya kifo cha Mark. "sasa tunafanyaje" aliuliza Monica, "ah hatuna la kufanya, sisi tulitenda uovu huku tukifurahia bila kufikiria ni kiasi gani tulichowaumiza wengine" Jay aliongea akionekana kujuta sasa. "akah! we vipi sasa unajuta nini, mi nasema hapa cha msingi ni kumuua Alwin maana nahisi yeye ndie anetufanyia mchezo huu" alifoka Alex kwa hasira. "sasa umeona ulivokuwa huna akili unataka kurekebisha kosa moja kwa kutenda jingine" Jay alimjibu akionekana kuchukizwa na maneno ya Alex. "mi nlikwambieni huyo boya ni mtoto wa mama" aliongea Alex na kumkejeli Jay, "sawa mi ni mtoto wa mama, lakini mi naona bora tujiandae kufa tu maana hatujui anefuata ni nani" Jay aliongea na kuinuka kisha akaanza kutoka nje, "nenda huko na leo utakufa wewe, Jestina kama unanisikia leo Jay amejianda ukamuue sawa" aliongea Alex na kufanya mzaha.
Jay hakujibu kitu,wakati anatoka aliingia unyonge wa ghafla na kupatwa na homa kali sana iliomfanya aanguke barabarani. Wasamaria wema walipiga simu hospitali na punde gari ya kubebea wagonjwa ilifika na kumuawahisha hospitali. Alipofika tu alipatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya sana. Familia yake ilifka akiwemo mkewe na mwanae wa kike mwenye umri wa miaka minne, lakini hawakuruhuisiwa kumuona kutokana na kuwa hali yake haikuwa nzuri. Hali hiyo ilimtia simanzi mkewe kumuona mumewe yupo katika hali mbaya sana lakini angefanyaje na alitakiwa kusubiri.
Walisubiri mpaka jioni lakini hali yake haikuchanganya hico wakaambiwa waondoke na warudi kesho kwa ajili ya kumuangalia walikubaliana na daktaru na kuondoka. Kiza kilianza kuingia lakini bado hali ya Jay haikutengemaa kabisa "kwa kweli tumejaribu kadri ya uwezo wetu sasa ni muda wa kumuachia Mungu atende muujiza" aliongea daktari mmoja na wenzake wakamuunga mkono. Walizima vifaa vyote na kumuhamisha chumba, huko walimuunganisha na mashine ya kupumulia kwa ajili ya msaada maana hata pumzi ilikuwa ni ngumu kuvuta. Baada ya hapo walitoka wote na kumuacha chini ya uangalizi wa manesi.
"Jay.....amka" alisikia sauti ikimuamsha huku akitingishwa, kwa uvivu alifungua macho na mbele yake alikuwa Jestina amesimama akiwa na sura yake ya kawaida, sio ile ya kutisha. "najua umekuja kulipiza" aliongea Jay huku akiitoa mashine ya kupumulia, "lakini nina ombi moja tu kwako, naomba uniache mpaka kesho angalau nimuone mwanangu kwa mara ya mwisho kabla ya kuaga dunia" aliongea Jay kwa masikitiko makubwa. "kwanini ulikubali kushuhudia unyama ule" aliuliza Jestina huku uso wake ukianza kubadilika na kuwa wa kutisha. "kwa kweli siku ile sikutegemea kama kungetokea tukio kama lile" alijibu Jay kiunyonge, "lakini wakati linafanyika ulikuwa na uwezo wa kuzuia lisifanyika" aliongea Jestina akizidi kutisha. "hilo ndio linalonijutisha mpaka leo" aliongea Jay huku machozi yakianza kumtoka, "najua kama nimekukosea na niko tayari kulipa kwa nilolitenda, lakini naomba unipe siku moja tu japo nimuone mwanangu na mke wangu kisha njoo unimalize" Aliendelea kuongea Jay huku kilio kikipamba moto, alijaribu kujifuta lakini aliposusha mkono Jestina alikuwa kashaatoweka. "asante kwa kunikubalia ombi langu" aliongea huku akijiweka vizuri kitandani na kuendelea kulala.
Asubuhi mapema familia yake ilifika kumuona, "nini kimekusibu baba Sophia" aliongea mkewe huku akimuangalia kwa huruma, "hata mimi mwenyewe sijui, homa tu ilinishika ghafla" alijibu huku akilazimisha kutabasamu. "pole mume wangu" aliongea mkewe kumpiga busu katika paji la uso, "pole dady utapona" sauti ya Sophia iliskika huku akimpa pipi baba yake. Sophia alikuwa kafanana sana na baba yake, na alimpenda sana. "Sophia baby njoo nkwambie kitu" Jay alimuita mwanae na kumnong'oneza kitu, Sophia alitabasamu na kumrukia baba yake kisha akasema " wewe ni baba mzuri kuliko wote". Muda wa kutizama wagonjwa uliisha na familia yake iliaga na kuondoka huku wakiahidi kurudi kesho yake kwa ajili ya taratibu za kwenda nae nyumbani. Aliagana nao huku machozi yakimtoka maana alielewa hiyo ilikuwa ni siku yake ya mwisho duniani. Kutokana na hali yake kuimarika mashine za msaada wa kupumua ziliondolewa na kupelekwa chumba cha wagonjwa wa kawaida tu. Aliendelea kupata matibabu madogomadogo, lakini akilini mwake alikuwa akiwaona kama madaktari wanatwangaa maji kwenye kinu maana usiku wa siku hiyo ni usiku wa kifo chake.
Usiku hatimae ulifika na Jay alikuwa tayari kwaajili ya kufa tu maana alielewa kabisa ni aina gani ya mauaji anayofanya Jestina. "Jay, naona uko tayari kwa adhabu yako" alimsikia Jestina akimwambia wakati akiwa amepumzika. "ndio niko tayari kwa chochote" alijibu Jay huku akitetemeka, "Kwa vile umelitambua kosa lako na kulijutia, mimi sikuja hapa kukuuwa maana kwanza una mke anaekuthamini sana na pili una mtoto ambae bado anahitaji malezi yako na upendo wako kama baba yake" aliongea Jestina na kujitokeza mbele ya Jay akiwa katika umbile la kibinaadamu "lakini nataka ufanye kitu kimoja, usijaribu kutoa ushahidi kokote pale na pia nakupa siku tatu uondoke Mashvile na familia yako yote, nenda mbali sana na uwe baba mwema kwa mwanao na pia mume mwema kwa mkeo. Na jengine asijue hata mmoja miongoni mwa marafiki zako waliohusika na kifo changu. Mimi nimekusamehe na nakutakia maisha mema na yenye amani tele lakini kumbuka ukitovukwa adabu nitakurudia" alimaliza kuongea Jestina na kuoweka. Jay hakuamini kama kasamehewa maana alielewa kabisa kuwa Jestina alikuwa hataki masihara, alilala usingizi mzuri huku akijiapiza kufanya yote aliyoambiwa.
*******************
Mapema siku ya iliyofuata familia yake ilifika na taratibu za kutoka hospitali zikafanyika, baada ya kufika kwake alimueleza mkewe kuwa anataka kuhama Mashvile kwani amepata kazi nzuri nchini Italy. Aliwaeleza pia wazazi wake swala hilo na kwa vile yeye ndie aliekuwa analisha familia hakuna aliempinga, maandalizi ya safari yalifanyika kimya kimya bila hata rafiki yake mmoja kujua. Jioni yalikuwa yamekamilika na wote waliondoka mjini Mashvile "nakuahidi Jestina nitatekeleza yote ualionambia" aliongea maneno hayo kimoyomoyo wakati analipita bango liliandikwa KWA HERI MASHVILE.
"Oya Alex mtu wangu mbona tokea jana sijamsikia Jay" Patrick alimuuliza Alex ambae alikuwa bize akijaribu kumchora mwanadada mmoja ambe alionekana kudance vizuri sana, "ah mara mwisho niliskia kalazawa hospitali, lakini nahisi Jestina atakua kashampitia tayari" alijibu Alex na kuinuka kulekea katika ulingo wa kudance lakini nia na madhumuni yake ilikuwa ni kwa ajili ya yule mschana. "habari yako mrembo"
"safi tu"
"Mimi naitwa Alex sijui mwenzangu"
"ahaa mimi naitwa Jessie"
"jina lako zuri, tunaweza tukasogea pembeni tukaongea mawili matatu"
"hamna shida"
basi walisogea mpaka counter na Alex akaagiza vinywaji kisha wakaanza kuongea, waliongea sana mwisho walionekana kukubaliana "oya Patrick wacha mi nitoke na shemeji yako" Alex alimuita Patrick na kumwambia, "oya mwanangu mtoto huyo mkali, kama vipi tupige tungo" Patrick alimnong'oneza Alex. "tulia mtu wangu mi naenda nae geto nikimaliza kula asali na kutwangia na wewe uje kuonja mtu wangu" aliongea na wakakubaliana.
Patrick alirudi kwenye dance floor huku Alex akiondoka na Jessie, "tunaenda wapi sasa" aliuliza Jessie, "ah nyumbani kwangu si mbali na hapa" alijibu Alex na kuzungusha mkono wake kwenye nyonga ya binti huyo. Mwendo ulikwa wa dakika tano tu hatimae walifika geto na kumkaribisha ndani. "kaa kitandani hapo nakuja" aliongea Alex na kuingia chooni, kumbe alikwenda kutega camera ili ajirikodi anavomkuna mrembo huyo. Alirudi na kumkuta tayari ameshavua nguo na kubakia mtupu, tamaa ya ngono ilimpanda Alex kujikuta anamvamia lakini kabla hajafikisha mdomo wake kwenye midomo ya mrembo huyo alijikuta akirushwa kwa nguvu.
 
JESTINA-11
Ghafla mrembo huyo alianza kubadilika, naam hakuwa mwengine isipokuwa Jestina. "wewe hujabadilika hata kidogo" aliongea kwa nguvu sana, "yaani bado wewe na yule mshenzi mwenzako mlikuwa mnafikiri kupiga mtungo" aliendele kuongea huku akimsogelea. "Jestina nisamehe" alianza kuomba msamaha, "umechelewa sana" alijibu Jestina na kupiga kofi la uso akimwachia alama za kucha. Alex aliweweseka lakini alipofungua macho hakumuona ila ghafla akamtokea kwa nyuma na kumchana mgongoni. Alex alipiga yowe la kuomba msaada lakini wapi hakuna lolote lilisikilikana nje ya chumba hicho. Jestina akatoweka tena na kumtokea mbel yake ila hakumgusa alimuangalia tu usoni na Alex mwenyewe akaokota kipande cha kioo na kunaza kujichana. Alipiga kelele kwa maumivu lakini alishindwa kujizuia mwisho alianguka chini, hapo Jestina alimsogelea na kumpiga kucha za shingo na kulitoa koromeo, aliacha ujumbe na kutoweka huku Alex akiwa chini akijaribu kuvuta pumzi ambayo haikua na pakupita mpaka mwisho akakata roho. Patrick baada kuona Alex hapigi simu aliamu kutoka na kumfata geto.
Kwa mwendo wa haraka Patrick alifka geto kwa Alex na kukuta mlango umefungwa lakini kila alipojaribu kugonga haukufunguliwa. Alisubiri kama dakika kumi kumi hivi ila bado kulikuwa kimya, mwisho alikumbuka kuwa ana ufunguo mwengine wa mlango huo lakinialipojaribu kuingiza kwenye kitasa uligoma hiyo ilikuwa ni ishara kuwa kulikua na ufunguo mwingine kwa ndani. Baada kuona jitihada zake zimegonga mwamba aliamua kutoa simu yake na kuandika ujmbe "poa mshkaji wangu tumekubaliana vipi na wewe unafanya nini, mbona mimi nikipata kama hivo tunapiga mtungo safi ila haina noma" aliutuma na kuondoka. Aliondoka na kuelekea nyumbani kwao, baada kufika alivua nguo zake na kwenda kujimwagia maji. Alimaliza na kutoka kurudi chumbani na hapo ndipo aliposhtuka kidogo maana suruali yake chini ilikuwa imeganda damu. Alitahidi kutafuta ni sehemu gani ameumia lakini hakuiona ndipo machale yakamcheza lakini akapotezea na kuingia kitandani.
Asubuhi mapema aliwahi kuamka nakwenda geto kwa Alex, alipofika alishtuka sana baada kuona michirizi ya damu ikitokea ndani ya chumba hicho. Alipiga kelele na watu wakaja kwa pamoja walisaidiana kuvunjia mlango na hapo ndipo wakakutana na mwili wa Alex umelela sakafuni huku ukiwa umetapakaa damu. Bila kuchelewa walipiga simu polisi na kutoa taarifa, ila alichokifanya Patrick ni kuchukua simu ya Alex na kuufuta ujumbe aliomtumia ili asije akaonekana yupo hatiani. Haukupita muda polisi walifika eneo la tukio na kuanza kufanya uchunguzi na katik tafuta yao walifanikiwa kuipata camera alioitega Alex na kuichukua kama sehemu moja ya ushahidi wao. Walimaliza kufanya uchunguzi na taratibu nyingine zikafuata ikiwa ni pamoja na kuupeleka mwili wa Alex hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
"tumefanikiwa kupata camera sehemu ya tukio" aliongea polisi mmoja na kumkabidhi Inspector Hans ile camera. Na yeye bila kuchelewa aliunganisha na computer yake na kuanza kuangalia, ilionyesha Alex akitoka chooni na alipofika kitandani alijirusha lakini hakuonekana mtu mwengine katika kitanda hicho. Lakini ghafla alichomoka kitandani na kujigonga ukutani kisha akaonekana kama akiomba msamaha lakini ghafla alipiga kelele na damu kuanza kumtoka. Waliendelea kuangalia video hiyo mpaka walipoona anachukua kioo na kuanza kujikata wenyewe mpaka akaanguka chini na ghafla akaanza kutoka damu shingoni kama ishara kuwa amekachinjwa, yakatokea maandishi ukutani "AMELIPA". Hapo camera ikaingia chenga na kuzima kabisa,askari wengi waliotizama ile video walishtuka sana hasa pale yalipotokea maandshi ukutani.
"mi si niliwaambia kama mauaji haya hayafanywi na mtu wa kawaida" aliongea Inspecta Hans na kuwaangalia wenzake "sasa mmeamini kama kuna mizimu duniani" aliendelea kuongea lakini alionesha kama kushtuka kidogo na kuamua kurudia kuingalia tena kwa mara ya pili lakini kwa makini zaidi, ndipo akagundua kama shape ya mschana kama iliokuwa inaakisi mwanga. Wenzake walimshangaa na kumuuliza mbona anaangalia tena. "hebu angalieni kwa makini hiyo video kwa mbali sana utaona kama shape ya mschana" aliwaambia na wote wakaikodolea macho ndipo wengi wakagundua kile alichokisema Inspecta Hans.
Alwin akiwa kwao alifutwa na askari kuombwa aende kituoni kwa ajili ya majadiliano, alikubali bila kinyongo na kuondoka nao. walifika kituoni na kuanza mazungumzo.
"kijana hebu tueleze kuhusiana na Jestina"
"mimi sina la kueleza"
"tunaomba msaada wako maana mauaji yamezidi na yantupa sifa mbaya kama kitengo cha polisi"
"sasa mimi niwaambie nini wakati kesi yake ilifikishwa kwenu miaka kumi iliopita lakini mkajifanya wababe kuipindisha sheria, kwa kupewa pesa mkanibambikia mimi"
"tusaidie basi tuweze kumdhibiti"
"hahaha mna kichaa kweli nyinyi, kiufupi mumechelewa sana amerudi mwenyewe kuja kuiweka sawa sheria na nyinyi hakuna mnaloweza kufanya kilichobaki nyie kaeni tu musubiri kukusanya miili ya atakao waua"
"kijana unajifanya jeuri si ndio" inpecta Brandon alifoka
"tena wewe haswaa umo katika list yangu" Alwin aliongea maneno hayo na ghafla alianza kubadilika na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Naam walilipata jibu kumbe hakuwa Alwin bali alikuwa ni mwenyewe Jestina na aliamua kufanya hivo kumpa onyo Inspecta Brandon na polisi wengine juu ya mpango wa kupenda pesa na kupindisha sheria. Kushuhudia hivo Inspecta Brandon alianguka chini na kupoteza fahamu.
"mimi niliwaambia mkaniona namtetea Alwin, sikusema tu ila yalishaanikuta ndio maana nikawaambia haitasaidia hata kama mtamkamata Alwin kwa sababu Jestina ndie anaejibu ukimwita Alwin" aliongea Inspecta Hans, "unamaanisha nini kusema hivyo" aliuliza askari mwingine. "namaanisha kuwa Jestina anatumia sura ya Alwin, hivyo basi hata ukimhoji utaishia kukipata kama kilichompta Inspecta Brandon muda mfupi uliopita" aliposema hivo ndio wakakumbuka kama mkuu wao ameanguka, haraka walimbeba na kumuwahisha hosptali.
******************************
Ndege ilitua uwanja wa Mashvile, miongon mwa abiria walioshuka alikuwemo binti mmoja mrembo sana. Hakuwa mwengine isipokuwa ni mtoto wa Profesa Alexander Harison, Miryam. Baada ya miaka mingi sasa ndio anarudi nyumbani akitoka kuchukua masters katika udaktari akiwa kama daktari bingwa saikolojia. Alitoka nje ya uwanja na kuonana na baba yake mzazi "karibu nyumbani mwanangu" profesa aliongea huku akitanua mikono kama ishara ya kutaka kumkumbatia mwanae. Miryam kwa furaha aliruka na kumkumbatia baba yake. "umekuwa mkubwa mwanangu" aliongea profesa, "ah kawaida tu baba" Miryam alijibu na kuachia tabasamu na kuufanya uzuri wake uonekane vilivyo. "mie ningapata mtoto kama yule pia nisingefikiria kuoa mke mwengine", "dah yule mtoto ni mkali kupindukia kiasi profesa ampe kila anachotak", "sasa wewe unadhani acheze zawadi kama ile kutoka kwa muumba, kama angekuwa mwanangu angetaka hata dunia ningempa". Hayo ni maneo yalikuwa yakisemwa na walinzi walipokuwa wakimpokea mtoto wa bosi wao.
Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, msafara huo ulikuwa ni zaidi ya ule wa raisi, ulikuwa na gari kumi zote aina Rolls royce nyeusi zikisindikizwa na pikipiki tatu mbele na tatu nyuma. Kwa kweli profesa alimpenda sana mwanae kiasi kwamba hakujali anatumia kiasi gani cha fedha kumhudumia tu. Alimpa kila alichotaka na hakusita kumwambia "WEWE NI LULU YA MAISHA YANGU". Mapenzi yake kwa mtoto wake hayakuwa na hayakufanana na chochote. Ila alijua ipo siku itabidi amkabidhi kwa mtu mwengine ili amlee, akimaanisha kuwa ipo siku mwanae pekee ataolewa na kuondoka nyumbani. Na kila alipoifikiria siku hiyo alihisi kama nusu na robo ya maisha yake atakua kayatoa, kuna baadhi ya wakati alijikuta akibubujikwa na machozi lakini angefanyaje na ndio mfumo wa maisha ulivo.
Walifika nyumbani na kupokewa kwa shangwe kubwa hasa ukizingatia anapokuwepo Miryam katika nyumba hio kila siku ni skukuu. Maana binti huyo kajaaliwa upendo wa hali ya juu sana kiasi kwamba wafanyakazi wote walikuwa wawazi katika kuongea nae, Ni mschana ambae hakujiona kwa uzuri wake na utajiri aliokuwa nao bali aliishi na watu wote kama sehemu ya familia yake. "Afadhali amerudi", "nakwambia huyu mtoto ni baraka ndani ya nyumba hii", "hata leo profesa aseme hana mshahara wa kutulipa basi mie nitafanya kazi bure ilimradi niwe karibu tu na Miryam". wafanyakazi wa kike hawakuwa nyuma katika kummwagia sifa binti huyo wa profesa maana aliuteka moyo wa kila mtu alikuwa ndani ya nyumba yao.
Kutokana na machofu ya safari, Miryam alioga na kupumzika. Upande wa Alwin alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na ujio wa Miryam na hata profesa alikubaliana na mwanae kuwa asimwambie chochote.
Sasa kutokana na kilichoonekana kwenye kamera askari wote waliamini kama kuzuia mauaji hayo ni sawa na kuzuia mawimbi baharini. Kila asakri aliamua kushughulika na mambo yake pasi na kuwaza tena njia za kumkamata muuaji, walijisemea "muache auwe tutakwena kukusanya mizoga". Jestina akiwa chumbani kwa Alwin ghafla hali ya hewa ilibadilika ghafla na kutoweka bila yeye mwenyewe kutaka, funga fungua alijikuta yupo kule katika ulimwengu wa waliodhulumiwa. "karibu tena Jestina" aliongea yule malkia, "mbona umenirudisha huku wakati sijamaliza kazi yangu" aliongea akionekana kuchukia kidogo. "kuna jambo nataka nikueleze kwanza ndio utarudi tena katika ulimwengu wa kibinaadamu" baada kusikia hivo kidogo akapoa. "Muda wako wa kukaa huko unakaribia kuisha" aliongea malikia na kumshtuwa kidogo Jestina, "si umenambia muda wangu utakwisha mpaka pale nitakapo wamaliza wote" aliongea Jestina kwa sintofahamu. "ndio, ilikuwa iwe hivyo lakini muda si mrefu utaanza kukutana na kikwazo" alijibu malikia, "na hicho kikwazo kitakufanya upumgukiwe nguvu za kuishi katika ulimwengu wa kibinaadamu", "nambie ni kikwazo gani hicho nikakiondoe mapema" aliaongea Jestina huku akianza kubadilika kwa hasira. "hutoweza kukiondoa hata uwe na nguvu kiasi gani hata mimi pia sikuweza kukiondoa wakati wangu" alijibu malikia akionesha ugumu wa kukiondoa kikwazo hicho. "basi nambie kikwazo chenyewe ni kipi" aliomba sasa Jestina, "MIRYAM" malikia alijibu huku akitetemeka.
 
JESTINA-12
"ah kumbe huyo tu" aliongea Jestina kwa dharau kidogo, "hiyo ni kutokana na mapenzi mazito aliokuwa nayo juu ya Alwin na jambo ambalo wewe hulijui ni kwamba Alwin anampenda sana Miryam japo hajawahi kumuona tokea azinduke, ila kwa sasa Miryam amerudi kutoka masomoni na akianza tu kuwasiliana na Alwin mapenzi yao yatamea tena jambo ambalo litamfanya Alwin aanze kusahau mambo mengine ikiwemo kisasi anachokusaidia kukikamilisha" aliongea malikia na hapo Jestina aliishiwa ujanja.
"lakini kuna kitu unaweza kukifanya ili kuendelea kubakia ulimwengu wa kibinaadamu" aliongea malikia, "kitu gani hicho". "usiwaingilia katika mapenzi yao wala usijaribu kumsogelea Miryam kwa ubaya maana katika ulimwengu hakuna vita kubwa kama ya mapenzi, pia hayohayo mapenzi ni amani ya kutosha" aliongea malikia. "sasa umesema wakianza kukutana mimi nitapoteza nguvu zangu" aliuliza Jestina, "utaweza kuwa nazo ikiwa Alwin atamueleza Miryam juu ya uwepo wa mzimu wako na kama atakubali bila kinyongo na kuamini kama ni kweli basi hapo utakuwa umeshinda maana hata nguvu zako zitaongezeka kwa sababu utakuwa na watu wawili ambao walikupenda sana kipindi cha uhai wako japo mwenyewe hukulifahamu hilo" alimaliza kuongea Malikia na kabla Jestina hajajibu chochote alitoweka na kurudi katika ulimwengu wa binaadamu. Alimkuta Alwin kalala fofofo, alisogea mpaka pembeni yake na kukaa. Alimuangalia kwa muda sana kisha akajilaumu kwa kumpa wakati mgumu sana kipindi cha uhai wake japo alimuonyesha ni kiasi alimpenda na kumjali, lakini kutokana na wivu wake wakimasomo hakutaka kumkubalia bali aliamua kumtesa kwa kutoka na mwanaume mwengine ambae baadae aliamua kumfanyi ukatili wa hali ya juu sana. Machozi yalianza kumtoka na kujikuta ni mwanamke asie na shukurania hata kidogo. Pia alikumbuka kipindi akiwa na urafiki na Miryam mschana ambae walitokea kupendana sana kutoka na tabia zao kuendana sana japo kiakili hakuwa na akili kama yeye "ama kweli kuwa na akili nyingi si kuwa na maarifa" alijisemea moyoni huku akihisi maumivu makali ya usaliti aliowatendea wawili hao pasi na kumthamini sana. Ila angefanyaje na ndio mambo yashaatokea hata kama angetaka kuyarekebisha isingewezekana maana tayari alishaaga dunia.
*****************************
Usiku uliingia huku maandalizi ya sherehe kubwa ya yakifanyika, ilikuwa ni sherehe ya kumkaribisha Miryam. Alwin akiwa kwao aliskia akiitwa na mama yake na aliposhuka alikutana na mtu asie mfahamu. Alikuwa na briefcase mkononi, "Mr Alwin huu ni mzigo wako" aliongea na kumkabidhi kisha bila kuongea kitu yeye aliondoka. Alwin alirudi chumbani kuufungua mzigo huo, alishangaa kuona kuna suti ya rangi ya maziwa au crem, viatu, tai nyekundu pamoja na funguo ya usafir. Pembeni kulikuwa na barua ndogo iliosema hivi.
"jiandae uje nyumbani kwangu by Profesa", yeye akiitwa na profesa huwa hafikirii mara mbili, aliingia chooni na kujimwagia maji. Alipomaliza alitinga suti alioletewa na kuning'iniza tai shingoni, alivaa viatu na kuchukua funguo lakini alipaongalia vizuri aliona saa moja matata sana na yeye bila kuchelewa aliitia mkononi na kuhakikisha kuwa amechukua kila kilicho ndani ya briefcase hilo. Alipojiridhisha yuko sawa alitoka chumbani kwake na kuelekea nje, aliwaaga wazazi wake na kutoka. Nje huko alikutana na gari moja ya bei mbaya aina ya Buggtti supersport vitesse ya rangi ya maziwa. Hakuuliza alibonyeza kitufe na kutoa loki, aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kwa profesa ilianza, kwa mwendo wa umakini zaidi alitumia dakika kama saba hivi kufika mjengoni kwa profesa.
Alishuka gari na kumkabidhi funguo mlinzi aende akaiweke maegesho, "na sasa anaingia mgeni rasmi wa kwanza Mr Alwin Kelvin" MC alitangaza na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe. "mmh jamani huyu kapendezaje", "wee jifanye mwendawazimu tu mali ya watu hiyo shosti". "sasa kwani mimi jiwe" hayo ni maneno waliokuwa wakiongea waschana wawili ambao walivutiwa sana ujio wa Alwin.
Basi aliekezwa meza kuu na kuambiwa akae kwenye kiti, "profesa kuna nini mbona unafanya sherehe" aliuliza Alwin "mambo matamu hayataki haraka" alijibu Profesa na hapo Alwin alielewa kuwa anatakiwa asiulize tena maswali. "na sasa tumkairbishe mgeni rasmi mwengine ambae pia ndie mlengwa mkuu wa sherehe hii Ms Miryam Alexander Harison" MC alitangaza tena na kuwafanya watu wachizike kwa makelele. Alwin alijikuta akitumbua macho kama mjusi aliebanwa na mlango huku akihisi hata moyo wake ulipunguza kasi ya mapigo, bila kujitmbua alijikuta akisemama na kuelekea kwenye ngazi ambapo Miryam alikuwa anashuka, hakuna aliemuuliza watu wote walitengeza njia ili apite bila kikwazo. "kwa kweli umependeza sana" alisema maneno hayo huku akimpa mkono Miryam, "asante hata wewe umependeza pia" alijibu Miryam. walitembea wawili hao huku wameshikana mikono utadhani ni mfalme na malkia wake mpaka kwenye meza.
**************************
Kimbembe kilikuwa kwa Patrick amabe alikuwa anapambana kutetea maisha yake, "Jestina najua nimekukosea naomba unisamehe", "ulikuwa na muda mwingi wa kutubu lakini hukufikiria hilo" Jestina aliongea kwa hasira mpaka radi zikawa zinapiga. Lakini ghafla alianza kupotea bila mpango, Patrick alipoona adui yake anapoteza muelekeo akaamua kutoka nduki. "Alwin nakuomba subiri japo kidogo nimalizane na huyu kwanza" aliongea katika moyo wake, na papo hapo akatoweka na kumtokea Patrick kwa mbele, bila kuchelewa alimpiga kucha za koromeo na kumuulia mbali. Alimpa kifo cha haraka makusudi ili asije akapoteza nguvu kabisa, Patrick alianguka chini kama mzigo huku damu nyingi zikimtoka shingoni. Taratibu Jestina alianza kutoweka kama vile unavofuta mchoro wa penseli kwa ufutio, nguvu zilinza kumuisha na kuanza kusikia maumivu makali sana. Aliona njia peke ya kujinusuru na kutoweka kabisa ni kwenda alipo Alwin na kumueleza yanayomkuta. Kwa nguvu zake kidogo zilizobakia alifanikiwa kutoweka na kutokea nyumbani kwa profesa. Na moja kwa moja alitokea mbele ya Alwin lakini alishangaa na kuona hata Alwin alikuwa hamuoni tena.
Alijaribu sana kumtokea mbele yake lakini hali ilikuwa ileile, kwa wakati ule Alwin alisahau kila kitu kiasi cha kuwa akili yake ilikuwa ikiutathmini uzuri wa Miryam tu. Baada kuona haonekani mbele ya Alwin, akaona njia pekee ya kuongea na Alwin ni kwa kutumia mwili wa mtu mwengine, alizunguka ndani ya ukumbi huo mpaka alipopata mtu wa kumtumia. Hapo aliuingia mwili huo na kuelekea alipo Alwin, "Alwin tunaweza kuongea kidogo" aliongea na kumfanya Alwin kugeuka lakini hakushughulika sana kwa sababu mwanamke aliemuita wala yeye hamjui. Alijaribu kumuita tena lakini haliilikuwa ni ile ile ndipo akaamua kumgusa mkononi, hapo Alwin alizinduka na kumgeukia kwasababu mwili wake ulikuwa wa baridi haswaa.
"Jestina unafanya nini hapa" aliuliza kwa sauti ya chini, "Alwin nakuomba nisikilize kwa makini sana" Jestina aliongea na kumvuta pembeni na kumueleza kila kitu. Alwin alishtuka kidogo baada kusikia vile, "subiri nikamwite Miryam" aliongea na kuondoka. "Miryam tunaweza kwenda kuongea varanda" nae Miryam hakukataa waliongozana mpaka varanda na kuanza kumueleza kila kitu, mwanzo Miryam alionekana kusita. "najua utakuwa huamini, subiri ni nimwite lakini nakuomba usipige kelele" aliongea Alwin baada kuona Miryam anakuwa mgumu kumuelewa. "Jestina jitokeze mbele yake ili akuone". Ghafla Jestina akatokea mbele ya Miryam "Mungu wangu, hivi ni kweli au nasinzia" yaliomtoka maneno hayo bila kujitambua. "Miryam nakuomba unisamehe kwa yale yote nlokukosea kwa sasa naomba unikubali kama rafiki yako kwa mara nyingine tena" aliongea Jestina huku akijitahidi asibadilike.
"Jestina mimi nilishaasahau hasa kama tuligombana mimi na wewe, siku ile nilitaka ufahamu tu kama ulikuwa ukiwaumiza watu wasio na hatia" Aliongea Miryam huku akimsogelea, "kama alivyoniambia Alwin kuwa umerudi kuja kuwalipisha waliokutenda basi mim niko pamoja na wewe" aliongea na hapo alikuwa karibu yake sana, aliamua kumshika mkono ili ajiridhishe kama kweli aliokuwa mbele yake. Alpomshika tu Jestina alitoweka na kumfanya Miryam ashangae kidogo "wow! Alwin its fantastic" aliongea huku akimkubatia Alwin kwa nguvu, "kama sheria ilishindwa kumpatia rafiki yangu haki yake basi mimi niko pamoja na nyinyi katika kuwateketeza wale wote waliohusika na kifo chake" Miryam aliongea lakini sauti yake ilikuwa imebadilika kidogo, Alwin alijitoa na kumwangalia "mbona unalia sasa" aliuliza kwa mshangao. "Alwin najua ulikuwa ukidhani namchukia sana Jestina, ukweli ni kwamba nilikuwa nampenda sana na ndio maana sikutaka apotee" aliongea Miryam kwa kwikwi. "usijali mpenzi wale wote waliohusika na kifo chake watalipa kwa maisha yao" Aliongea Alwin na kwa mara ya kwanza alimvuta Miryam na kukutanisha midomo yao au kama wanavyosema wengine "ROMANCE".
Kwa upande wa Jestina huo ulikuwa ni msimu mpya, maana alihisi mwili wake umepata uhai tena. Nguvu zake ziliongezeka mara dufu, wakati alizidi kutisha kiasi kwamba akikutokea tu kama unariho nyepesi basi unaweza kuaga dunia. Mvua ilianza kunyesha na radi zikawa zinapiga kwa nguvu sana hadi umeme ukazimika, "hahaha mlobakia jiandaeni" aliongea na kutoweka kisha hali ikarudi kuwa kawaida na umeme ukarudi.
Alwin na Miryam walirudi uwanjani huku wakiwa wameshikana viunoni, moja kwa moja mpaka meza kuu. "Profesa" Alwin aliita kwa sauti ya chini, "sema Alwin" alijibu profesa huku akimuangalia. "nataka kukuibia kitu"
"wewe mtoto we, kitu gani hicho"
"ni kitu unachokipenda sana katika maisha yako" Profesa aliposikia hivyo akaelewa Alwin anamaanisha nini. Alisimama na kuelekea kwa MC kisha akachukua kipaza sauti na kuomba watu wamsikilize. "mabibi na mabwana naomba muniazime masikio yenu kwa dakika chache, ule muda niliokuwa nikiusubiria kwa hamu umefika, hatimae Mungu ameitika maombi yangu. Nawaomba wageni rasmi wasogee hapa jukwaani" aliongea na Alwin na Miryam wakainuka na kuelekea jukwaani. "napenda kumtambulisha kwenu rasmi Mr Alwin Kelvin ni mkwe wangu wangu kuanzia sasa" aliongea na ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe "hongera kijana na karibu katika familia" aliongea tena na kukumbatiana na Alwin kisha akairudisha mike kwa MC na kumwambia aendelee na ratiba.
Wakati wakiendelea na sherehe, aliingia mwanamke mwengine aliekuwa mzuri kupita maelezo. Vidume vyote vilianza kutokwa na mate ya kumtamani mwanamke huyo ambae alivaa nguo iliong'ara sana. Alitembea taratibu mpaka alipo Alwin na Miryam "hongereani sana" aliongea na hapo Alwin akashtuka baada kusikia sauti hiyo maana aliifahamu vilivyo kama ilikuwa ni sauti ya Jestina. "duh umebadilika" alikuta akiongea, "Jestina" Miryam aliita. "ndio mwenyewe" Jestina alijibu, Miryam alishindwa kujizuia na kumkumbatia bila kujali kama ule ni mzimu. Marafiki hao watatu waliongea na kufurahi sana, waliongea kama walivyokuwa wakiongea kipindi kabla hawajagombana. "Jestina nina ombi moja kwako" alikuwa Miryam, "lipo tena" aliuliza Jestina "ombi langu ni Matt, naomba umpe kifo chechenye maumivu makali sana" aliongea Miryam na kumfanya Jestina atabasamu kisha akajibu "usijali maana huyo dawa yako ipo kuzimu naipika".
"na mimi nina ombi moja" mara Alwin aliingilia, "haya lipi hilo" aliuliza Jestina. "nikipata mtoto wa kike nitamwita Jestina" aliongea na kutabasamu, "ah hilo si umwambie Miryam" alijibu Jestina, "mimi nimekubali" Miryam alijibu kisha wote wakacheka. "jamani muda wangu wa kuondoka umefika kwa hio tutaonana kesho" aliongea Jestina na wote walikubaliana. Alipiga hatua tatu ghafla umeme ukazima na uliporudi hakuonekana tena.
**************************************
 
JESTINA-13

Veronica akiwa kwenye gari yake anarudi kwao, alikuwa amefungulia mziki mzito hiyo ni kwa sababu alikuwa anatoka club kujirusha. Alipoangalia kwenye kioo aliona kama mtu amekaa siti ya nyuma, lakini alipogeuka hakuona kitu. "ah pombe bwana" alijsemea huku akitoa simu yake kwenye begi ili apige, ghafla alihisi kama kagonga kitu. Alisimamisha gari, kwa uoga akashuka kuangalia ni kitu gani. "toba nimegonga mtu" alijisemea baada kugunduwa kuwa aliemgonga ni mtu. Wakati anajishauri afanye nini mara akaanza kumuona akisimama huku akionekana kuvunjikavunjika viuongo, lakini ajabu vilianza kukaa sawa. Baada kuona hivo aliamua kukimbilila kwenye gari, lakini alipojaribu kufungua mlango ulikuwa na loki. Alijaribu milango mingine lakini hali ilikuwa hiyohiyo, "huwezi kunikimbia" alimsikia akiongea, Alipogeuka uso kwa uso na Jestina. "wewe si ushakufa" alijikuta akiropoka, "ndio" alijibu Jestina na kumtandika kofi la uso Veronica. Kisha akaanza kubadilika na kuanza kutisha sana macho yalikuwa meusi yote huku mwili wake ukitanuka na kutoa harufu mbaya sana. Veronica kuona hivo alianza kukimbia hovyo bila kujua wapi anaelekea, "huwezi kunitoroka" Jestina aliongea kwa hasira na kutoweka.
Wakati Veronoca anakimbia ghafla alijikuta akirushwa na kujipigiza katika mti, alitoa yowe la maumivu makali sana huku akijishika mbavuni. "nisamehe Jestina" alianza kulia huku akiomba msamaha, "wewe huna haja ya kusamehewa, wewe ulikuwa unashangilia wakati mwanamke mwenzako anadhalilishwa pumbavu mkubwa wee" alijibu Jestina na kumsigelea na kumtia vidole vya macho kisha akaanza kumpiga makucha. Alimnyanyua na kumpigiza na chini kisha akamnyanyua tena na kumrusha kwa nguvu, moja kwa moja alikwenda kutua kwenye gogo lenye ncha kali lilipenya mgongoni na kutokea mbele na hapo mia zake zikawa zimefika ukingoni, kama kawaida aliacha ujumbe na kutoweka eneo hilo.
Uwezo aliokuwa nao sasa ulimuwezeshe kuwatokea maadui zake mpaka mchana, lakini hakutaka kutembeza kichapo mchana hivyo aliamua kuendelea na kazi yake nyakati za usiku. Wazazi wa vijana waliouwa waliamua kufanya maandamano na kuitaka serekali iwajibike na vifo vya watoto wao. Walonekana ni wenye hasira sana, "sasa jamani hasira za nini" aliongea waziri mkuu wakati akijaribu kuwapoza. "wewe na serekali yako ni wapuuzi, watoto wetu kila siku wanakufa vifo vya kutatanisha halafu wewe unatuuliza hasira za nini" aliongea mzazi mmoja, macho yake yalikuwa mekundu sana. "au kwa sababu wako wewe hayupo ndio maana unatuona sisi wajinga" mwengine alifoka, "eh yamekuwa hayo tena, basi msijali nawaahidi kuwa muuaji tutamkamata na tutamleta mbele yenu mumuhukumu" aliongea waziri mkuu na kuondoka bila kutaka swali lolote.
"dah mnajua leo nimedhalilika sana" aliongea waziri mkuu katika kikao maalum cha dharura, "mwiteni mkuu wa kituo" alitoa agizo. "hilo haliwezekani" alijibu Inspecta Hans nae pia alikuwepo kenye kikao hicho. "kwanini isiwezekane" alifoka waziri mkuu, "kwa sababu Inspecta Brandon yupo hospitaly kalazwa" alijibu inspecta Hans. "unasemaje wewe, sasa yule aliekuwa anakuja nyumbani kwangu tokea juzi ni nani" aliongea waziri mkuu huku akionyesha kuchanganyikiwa, "ndio muheshimiwa, tokea majuzi Inspecta Brandon amelazwa hospitali kuu akiwa amepooza" alijibu inspecta Hans, "na umesema alikuwa anakuja kwako" aliuliza Inspecta Hans. "ndio kwanini atakuwa nani yule" alijibu na kuuliza kwa wakati mmoja, "huyo ndio muuaji mwenyewe" alijibu inspecta Hans na kumfanya waziri ashtuke kidogo na kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Bila kuongea jambo aliinuka na kuondoka huku kichwani mwake akiwa na mawazo mengi sana kwa sababu amemueleza mambo mengi sana ambaya alitka kuyafanya kabla ya kumaliza wakati wake kama waziri mkuu.
Kwa upande wa Alwin na Miryam mapenzi yalinoga sana, muda mwingi walikuwa pamoja huku wakibadilishana mawazo na hasa wakipanga maisha yao ya ndoa yatakuwaje. Jestina hasira ziliongezeka na kujikuta akitamani kuuwa hata mchana. Alipoona hali imezidi kuwa mbaya aliamua kufunga safari na ya kurudi katika ulimwengu wa watu waliodhulumiwa. "nilitarajia utarudi tu" aliongea malikia baada kumuona Jestina, "tokea nguvu ziongezeka huwa napata hamu ya kuuwa sana" aliongea Jestina. "hio ni dalili ya kuwa muda wako kukaa duniani unakwenda ukingoni" aliongea malikia na kumshangaza Jestina. "unasema nini" aliuliza Jestina, "ndio, mpaka sasa umebakia na siku tano tu" alijibu malikia. "hauwezi kuongezeka muda" aliuliza tena, "haiwezekani hata kidogo, kwa sababu muda wako wakuwepo katika ulmwengu huu pia umekwisha, unatakiwa kuondoka na urudi kwa muumba wako" aliongea malikia na alionekana kama hatanii hata kidogo. Baada ya kusikia hivo aliaga na kuondoka zake. Alirudi duniani hukua akitafakari jinsi ya kuwamaliza waliobakia hasa Matt ambae yupo nje ya mji. Na ukizingatia yeye hawezi kutoka nje mji huo, alihisi kama mpaka ataondoka hatokamilisha kazi yake. Kilichomuuma zaidi ni pale alipokumbuka kuwa Adui yake mkubwa alikuwa hayupo katika mji huo.
**********************************************
Siku mbili zilipita na mauaji yalizidi sasa, kwa siku aliuwa watu zaidi ya wanne, Watu walizidi kulalamika kutokana na mauaji hayo lakini kumkamata ni jambo ambalo lilkuwa haliwezekani. Alipoona zimebakia siku tatu ndipo likamjia wazo, aliamua kwenda kwa waziri na kumuingia mwilini na kumtia kama ugonjwa hivi. Hali ya waziri ilikuwa mbaya sana, aliwahishwa hospitali kwaajili ya matibabu lakini haikusaidia, Alipoona anakaribia mwisho wake akaamuru Matt apigiwe simu na kupewa taarifa hizo jambo ambalo lilitekelezwa haraka sana. Ndani ya masaa kumi baada kupigiwa simu Matt aliwasili Mashvile na moja kwa moja alikwenda hospitali kwaajili ya kumjulia hali baba yake. Masikini hakujua kama amerudi kuja kukifata kifo chake "vipi hali yako baba" aliuliza "ndio kama unavyoiyona mwanangu" alijibu kwa tabu sana. Mwili wake ulivimba na kupata vidonda vingi sana ambavo vilitoa harufu na damu. Jestiina baada kuona windo lake limerudi alisubiri mpaka usiku na kutoka katika mwili wa waziri mkuu, usiku huo alikwenda kuwamaliza waliobakia ili abakie na Matt tu.
Siku iliofuata Matt alikwenda hospitali kumuona baba yake, lakini alipofika alishangaa kuona vidonda vimeanza kupungua na akaambiwa kuwa hali ya mheshimiwa inazidi kuwa nzuri na huenda muda si mrefu akeuhusiwa kurudi nyumbani. Mapenzi yalizidi kunoga kati ya Alwin na Miryam na kutokana na kuwa walikuwa ni watoto wa familia zenye uwezo mkubwa kifedha. Walinunua jumba moja kubwa sana na la kisasa, taratibu walianza kuweka vitu huku wakionekana ni wenye furaha sana. Mtu yeyote aliewaona aliweza kuiona furaha hiyo kupitia macho ya wawili hao. Jestina alikuwa kaishuhudia yote hayo na alionekana kufurahi sana, jioni ya siku hiyo aliwatokea kina Alwin na kuomba kuongea nao.
"najua mupo katika kipindi cha maandalizi ya ndoa lakini naomba dakika kadhaa tu mnisikilize" aliongea Jestina.
"sawa hakuna shida" Alijibu Alwin
"muda wangu wa kukaa katika dunia umekwisha"
"unamaanisha nini" aliuliza Miryam
"namaanisha kuwa muda si mrefu nitawaacha niende nnapostahiki kuwepo
"mbona mapema" aliongea tena Miryam kwa unyonge zaidi
"na vipi kuhusu Matt" aliuliza Alwin
"Matt siku yake ishafika" alijibu Jestina akionekana kupandwa na hasira
"Dah sawa ila tunatamani ungeendelea kuwepo" aliongea Alwin
"Hata mimi pia natamani ingekuwa hivyo lakini ni jambo ambalo haliwezi kutokea kumbuka mimi nilishaakufa muda mrefu sana" aliongea Jestina na kuwaaga "nakwenda kutimiza kilichonileta duniani" aliongea na kutoweka.
 
Back
Top Bottom