(darasa) Ubunifu sahihi wa inveter huu hapa.

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,001
1,509
UBUNIFU WA INVETER



Jambo la msingi katika uundaji wa inveter ni kubadili voltage kidogo ya umeme wa battery (Umeme wa battery ni umeme mnyoofu Direct Current”DC”) na kuupeleka katika umeme mwingi unao rukaruka(umeme tunaotumia kuwasha TV,sub-woofer n.k ni umeme unao rukaruka kiasiri Alternating current “AC”).



MATUMIZI YA INVERTER.



1. 1. Hutumika kama Power Back –Up(kifaa kinacho endelea kutoa nguvu ya umeme hata baada ya umeme wa Tanesco kukatika)



2. 2. Hutumika katika mfumo wa solar,katika kuubadili umeme wa solar utumike kwenye TV,music n.k.



3. 3. Pia hutumika kuzalisha umeme maeneo ambayo hayana umeme kwa kuubadili umeme wa battery na kuwa umeme mkubwa ambao unaweza kutumika katika shughuri mbalimbali za uzalishaji.



VITU VINAVYO KAMILISHA MFUMO WA INVERTER










1.Sakiti ya Oscillator.




Sakiti hii ndiyo inayo geuza umeme mnyoofu(DC) kuwa umeme mgeuko (AC).



Sakiti hii hufanikiwa kutengeneza aina hii ya umeme wa (AC) kwa kuzalisha mawimbi (Hz), mawimbi haya ili yaweze kufaa lazima yawe mawimbi yenye idadi ya mruko wa mara 50 au 60 kwa sekunde(50Hz au 60Hz ).



Mawimbi haya ndiyo ambayo umeme tunao utumia majumbani unacheza cheza,Ni vigumu kuona kwa macho kuchezacheza huku kwa umeme majumbani kwetu kwa sababu mawimbi haya yanaenda kwa kasi sana.



Vifaa vyetu vya majumbani vimetengenezwa kutumika katika aina hii ya mawimbi tazama chaji yako ya simu utakuta wameandika inatumika katika mawimbi ya 50Hz,60Hz.)



Haya ndio mawimbi ambayo ni lazima tuyatengeneze kwanza.Baada ya saketi hii kutengeneza mawimbi hayo kazi yake huwa imekwisha.



2.Saketi ya pili huwa ni Driver circuit.



Hii kazi yake ni kuingiza umeme wa battery ndani ya transformer.




NB.




Ili transformer iweze kukuza umeme ni lazima umeme huu uwe katika hali ya kurukaruka(AC).



Hivyo umeme ukitoka katika battery huingia katika sakiti hii ya driver ndipo unaingia katika transformer.



Sakiti ya driver huwa na vitu vinavyo itwa power transistors,hizi ndizo huingiza umeme kwenye transformer.



Transistor hizi husubili kuwashwa na mawimbi yanayo toka katika Oscillator;Hivyo basi kwakuwa mawimbi haya yanakuja na kuondoka mara 50 au 60 kwa sekunde basi hata transistor hizi zitakua zinawaka na kuzima mara 50 au 60 kwa sekunde.



Matokeo yake umeme unaoingia katika transformer utakuwa unaingia na kukata(unaruka ruka);mara 50 au 60 kwa sekunde.



Kwakuwa transiformer huhitaji umeme unaorukaruka ili iweze kuukuza basi umeme huu hukuzwa kirahisi na kutoka upande wa pili wa transfomer kwa ajili ya matumizi ya kuwasha taa,TV,Radio n.k



3.Saketi ya tatu ni Output stage(transformer)



Hiki ni kifaa muhimu ambacho ndio hupokea umeme huo unao rukaruka na kuukuza.



Transformer inayo tumika hapa ni aina ya transiformer chocheo (step up transformer)



Transformer hii hua na sehemu kuu mbili ambazo ni



(a)Primary winding



Huu ni upande ambao umeme unaotoka katika driver circuit unaingilia



Kwa kawaida upande huu huwa na mizunguko pacha miwili ambao kila mmoja unauwezo wa kubeba volt 12;Hivyo kitaalamu transformer hii huitwa center tapped transformer ambayo itakuwa12v-0-12v.



(b)Secondary winding



Huu ni upande ambao umeme unatokea kwa kawaida huwa na uwezo wa kutoa umeme kiasi cha volt 220v hadi 240V aina ya AC ulio katika mawimbi ya 50Hz au 60Hz kwa ajili ya matumizi ya vifaa vyako.






UBUNIFU WA INVETER KWA KUTUMIA IC YA SG3524.



Tambua ufanyaji kazi wa SG3524.









Hii ni Ic ambayo kitaalamu inaitwa Pulse Widith Modulator(PWM),IC hii nitoleo ambalo linasifa ya kuweza kutambua kupanda na kushuka kwa output voltage na kufanya marekebisho automaticall.



Inveter nyingi zimekuwa na tatizo la kupungua kiwango chake cha output pale inveter inapofungwa mzigo au pale battery inapoanza kushuka.hivyo IC hii imekuja kuondoa tatizo hilo.



Ni IC nzuri kwa wabunifu wa inveter za Push-Pull.



Kazi ya miguu ya IC hii.



Mguu wa 1 na wa 2.-Miguu hii ni ya kifaa linganishi(comparator)kilichopo ndani ya IC.



Kazi ya kilinganishi hichi ni kupokea taarifa ya mabadiliko kutoka katika mfumo wa mrejesho.Ikisha pokea mrejesho huo kama kutaonekana kuna mabadiliko kilinganishi hicho hubadilisha mfumo wa frequency,ili kuhakikisha hakuna mabadiliko yoyote katika kiwango cha umeme kinacho toka nnje.Kutokana na sifa hii ndiyo maana IC ya SG3524 imekuwa bora zaidi kuliko IC nyingine za Inveter za mfumo huu wa Push-Pull.



Mguu wa 3.-Mguu huu hutumika kulinganisha matendo ya IC ya pili ili ifanane na matendo ya IC hii,katika mifumo ya saketi ambayo inatumia IC mbili au zaidi mguu huu ndiyo hutumika.Kwakuwa sisi tunatumia IC moja tu mguu huu kwetu hauna kazi hivyo tutauacha bila kuunga.



Mguu wa 4 na wa 5. Miguu hii hutumika kama current limitting kwa saketi zenye mfumo huo hasa katika DC to DC conveter.Kwakuwa sisi hatuhitaji mfumo huo katika saketi yetu hii,miguu hii yote miwili hua inaungwa katika ground(hasi ya battery).



Mguu wa 6 na wa 7. Miguu hii ndiyo hutumika kwa ajiri ya kuunda Mawimbi ya mchezesho(Oscillation) ya IC.Mguu wa 6 hufungwa Resistor na mguu wa & hufungwa capacitor).Rejea katika NOTES hapo chini.



Mguu wa 8.Mguu huu huungwa katika hasi(-) ya battery huingiza negative charge katika IC.



Mguu wa 9.Hushilikiana na mguu wa 1 na wa 2 katika kuhakukisha output voltage inabaki kama ilivyo bila kubadilika,mguu huu kazi yake ni kulipiza yaani huongeza pale palipo pungua na hupunguza pale palipo zidi.



Mguu wa 10. Huu ni mguu ambao hutumika kuizima IC,mguu huu utaizima IC kama tu ukipokea Chaji chanya.Mguu huu huungwa na mfumo wa saketi nyingine ya nje ambayo itasaidia kuizima IC endapo battery inakua imepungua sana au kama kuna short au overload.



Kwakuwa katika saketi yetu hii bado hatujatengeneza saketi za mifumo hiyo mguu huu ni lazima uungwe moja kwa moja katika chaji hasi ya battery.



Mguu wa 11 na wa 14.Ni miguu ambayo hutoa umeme ambao tayari upo katika hali ya mchezesho(oscillation).Umeme huu ndiyo huenda kuchezesha zile MOSFET kwa mawimbi ya mara 50 kwa sekunde(50Hz) ili kuzalisha umeme wa AC ambao utaweza kukuzwa na transformer na kutoka upande wa pili.



Miguu hii ukipima umeme wake na Hasi hakikisha unapanda volt kuanzia 3.5 hadi 5.



Mguu wa 12,13, na 15.Miguu hii huungwa katika chaji chanya ya battery kwa pamoja katika saketi hii.



Mguu wa 16.Huu zotoa Volt 5 ambayo hutumika kwa ajiri ya comparator(linganishi)ya saketi husika.



UBUNIFU WA INVETER YA WATT 1000 KWA KUTUMIA IC YA SG3524














(a)Tafuta frequency ya inveter yako



F= 1/ 1.1 x Ct x Rf



Hivi ndivyo vifaa vitakavyo pachikwa eneo la frequency,ambavyo vinaonekana vitaleta kiwango cha 50Hz



Time Capacitor (CT) = 0.22μF






Fixed Resistor (RF) = 56KΩ






Variable Resistor (VR) = 10KΩ(tunaweka hii variable resistor ili uweze kuwa na uwezo wa kurekebisha frequency manually kupata 50Hz.






Time Resistor (RT)=56KΩ+10KΩ = 66KΩ







Namna ya kuthibitisha matokeo ya muungo wa vifaa hivi kikanuni.



F= 1/ 1.1 x 0.22μF x 66KΩ



Thamani ya capacitor inabidi ibadilishwe iwe katika Farad badala ya micro Farad



Thamani ya resistor inabidi ibadilike iwe katika ohm badala ya kilo-Ohm



F= 1/ 1.1 x 0.22μF x 66KΩ



F= 1/ 1.1 x (0.22μF÷1000000) x (66KΩx 1000)



F= 1/ 1.1 x 0.00000022F x 66000Ω



F= 1/ 1.1 x0.01452=0.015972



F= 1/0.015972=62.6Hz



F=62.6Hz






(b)Chagua aina ya MOSFET itakayo faa.



(i) Power ya mosfet.



MOSFET itakayo tumika hapa ni jamii ya N-channel ambayo ina vigezo vifuatavyo



Iwe na uwezo wa watt 200 ambapo utafunga tano kila channel jumla yake utahitaji MOSFET 10.(idadi yake inaweza kuongezeka ama kupungua kutegemeana na wattage ya mosfet husika.)Kumbuka wattage ya mosfet moja izidishe kwa idadi ya mosfet hakikisha unapata 1000 kwa kila channel.



(ii)Frequency za Mosfet



Tafuta muda wa kufunga na kufungua wa MOSFET



Time=1/frequency







T= 1/f =1/50Hz(Nimechagua 50Hz kwasababu mawimbi yatakayotakiwa kusetiwa ni ya kiwango cha 50Hz).



T= 1/f =1/50Hz =0.02 Seconds



(iii) Tafuta kiwango cha current cha MOSFET



Kwakuwa tutataka inveter yetu iwe na watt 1000,MOSFET itakayo faa hapa ni ile yenye uwezo wa kupitisha kiwango cha current ambacho ni.



Kiwango cha watt 1000



Bettery itakayo tumika 12 Voltage



Kwa mujibu wa Ohms Law Current=Power/Voltage



Current= 1000/12=83.3 Ampere



Current = 83.3 Ampere.



Kiwango hiki cha current ambacho kinaweza kupitishwa na MOSFET husika kinajulikana kama Drain Current(ID)



Hivyo kwa mujibu wa Calculation hizo hapo juu ID = 83.3 Ampere.



(c) Tafuta ukubwa wa Transformer inayo hitajika



Transformer inayohitajika hapa ni lazima iwe ya Center Tapped ya 12V-0-12V katika primary



Na 0-220V katika secondary ya 100 watt..



-Primary current = Power ÷ Voltage



Primary current = 1000 ÷ 12 = 83.3 Ampere



Hivyo transfomer ambayo itatumika katika saketi hii upande wake wa primary lazima waya wake uwe na uwezo wa kupitisha kiwango cha 83.3 Ampere.



-Secondary current



secondary current = Power ÷ Voltage



secondary current = 1000 ÷ 220 = 4.5 Ampere



Hivyo transfomer ambayo itatumika katika saketi hii upande wake wa secondary waya wake lazima uwe na uwezo wa kupitisha kiwango cha 4.5 Ampere.






(d) Tafuta Power factor ya Inveter yako.



Baada ya kumaliza kusuka inveter yako itakulazimu kujua power factor ya inverter yako.



Formula ya kutambua power factor(PF) ni



PF =Pg/√Pg2 + (VIc)2



Ambapo;-



Pg=kiwango power cha inveter husika



V = Voltage itakayozalishwa na inveter



Ic= Current inayonyonywa na inveter kabla haijafungwa mzigo



Hivyo basi



PF =1000V/√1000V2 + (12v x 50A)2



PF =1000/√1000000 + 360000=1360000



PF =1000/√1360000



PF =1000 ÷1166.19037896906



PF = 0.86



(e)Tafuta Efficiency ya inveter



Baada ya kujua Power factor ya Inveter yako sasa itakulazimu utafute efficiency ya inveter yako



Efficiency = Pout / Pin x 100%






Kwa mujibu wa Inveter yetu power yeke ni 1000Watt,hivyo power out itakuwa ni 1000.



Ili tuweze kutafuta Power in lazima tutafute apparent Power.



Apparent Power = Power in watts ÷ Power factor



Apparent Power = 1000 ÷ 0.86 = 1162.8



Apparent power =1163 VA



Sasa tafuta Efficiency



Efficiency = Pout / Pin x 100%



Efficiency = 1000 / 1163 x 100%



Efficiency = 85%



(f) Kuchagua size ya battery kutokana na matumizi yako.



Tambua kuwa matumizi yako ya umeme ndiyo yatakayo amua ni battery ya ukubwa gani unayo hitaji.



Mfano.



-Unavifaa vya umeme ambavyo jumla yake vina Watt 500watt



-Inveter unayo tumia ambayo ni hii hapa ina Efficiency ya 85%



-Unataka vifaa vyako vifanye kazi kwa muda wa masaa 10



Je ni battery ya size gani utakayo takiwa kununua?



Ukokotozi.



Tafuta True Power



85/100 =0.85



500÷ 0.85 = 588Watt



Tafuta true current =588÷12=



Current=49Ampere



Tambua kuwa size ya battery inatambuliwa kwa kiwango cha AH(Ampere Hour)



Hivyo kujua ni Battery ya AH kiasi gani unahitaji tumia kanuni hii.



Battery AH=Current required x Time in hour



Battery AH=49A x 10Hrs=490AH



Battery ya ukubwa wa 490AH na zaidi ndiyo inayoitajika.






MAJUMUISHO YA PROJECT YETU YA INVETER



Power = 1000watt



Frequency= 50Hz



Voltage input = 12Voltage DC



Voltage Output.= 220 Voltage AC



Wave = Square wave.



Power factor =0.86



Efficiency = 85%





Vifaa vinavyohitajika kuunda inveter hii.



Transistor



Q1 BC557 x1



MOSFETs transtor N-chanel IRFP 460 x10



Resistor



R1=56KΩ



R4=10kΩ



R2 and R3 =4.7k



R6,R9=100KΩ



R7,R11,R12=1kΩ



R8=2.2kΩ



R10= 3.9kΩ



R5=47kΩ



R13=10kΩ



Capacitor



C1,C4,C8 =104 polyster capacitor



C5,C3=10uf/16v Electrolytic capacitor



C2=1uf/50v Electrolytic capacitor



C7=4700uf/35v Electrolytic capacitor



Diode



D1-D5=1N4007



IC =SG3524



Transfomer



T1= 12-0-12 83.3 ampere by 220v



T2 =12v 0.5 ampere by 220v

ENJOY!

Imeandaliwa na Transistor,naomba isitumike katika machapisho mengine nje ya jamii forums bila kibali changu.

Kujifunza zaidi tembelea blog ya electronicsdarasa
 
Mkuu nimejaribu kukufikia ktk blogg yako lakini nimeshindwa. Lakini mimi shida yangu ni ushauri wa kiufundi. Mimi sina elimu ya vifaa vya umeme yaani sijapitia chuo ila ni mtundu tu! wa vifaa vya umeme. Sasa kitu ninacho kiitaji ni jinsi gani naweza ku control reley ya 12volt lakini lengo langu si kutumia 12volt badali yake nitumie 3v kutoka katika terminal ya vibrator ya simu kama ndo iwe input katika upande wa + ili coil iweze kusumakishwa ili iweze kufunga mkondo wa umeme . Nimejaribu kucheck blogg mbalimbali za nje lakini sikupata nikitakacho wengi walinishauri kutumia transista ambazo kama switch lakini nimeshindwa jinsi ya kuunganishwa kwake kutoka katika terminal za vibrator ya simu. Lengo lote la kufanya hivi ni kutaka ku control switch remotely kwa kutumia simu ya mkononi na reley. Nimejaribu kuweka mchoro kama mfano, hapo kwenye A ilitakiwa iwe 12v lakini nataka nitumie 3volt. Nitashukuru kama nitafanikisha.
IMG_20160317_222942.jpg
 
Mheshimiwa transistor somo lako ni nzuri sana sana sana saidia kwa kutuletea equipments mfano transistors, transformer, capacitor, MOSFET n.k kwa kueleza hasa matumizi yake tafadhari nawasilisha mkuu.
 
Natamani kuwa fundi lkn sijui kitu. wacha nikae kimya hata kama nimependa sana huu uzi.
 
Sasa transistor nitajuaje kuwa hii inverter ni ya square wave maana sijaona kwenye maelezo yako mahali palipojionyesha kwamba output wave form yake ni square pia nimejaribu kuingia kwenye hiyo blog yako imenikatalia inaniambia sijaalikwa
 
Mkuu nimejaribu kukufikia ktk blogg yako lakini nimeshindwa. Lakini mimi shida yangu ni ushauri wa kiufundi. Mimi sina elimu ya vifaa vya umeme yaani sijapitia chuo ila ni mtundu tu! wa vifaa vya umeme. Sasa kitu ninacho kiitaji ni jinsi gani naweza ku control reley ya 12volt lakini lengo langu si kutumia 12volt badali yake nitumie 3v kutoka katika terminal ya vibrator ya simu kama ndo iwe input katika upande wa + ili coil iweze kusumakishwa ili iweze kufunga mkondo wa umeme . Nimejaribu kucheck blogg mbalimbali za nje lakini sikupata nikitakacho wengi walinishauri kutumia transista ambazo kama switch lakini nimeshindwa jinsi ya kuunganishwa kwake kutoka katika terminal za vibrator ya simu. Lengo lote la kufanya hivi ni kutaka ku control switch remotely kwa kutumia simu ya mkononi na reley. Nimejaribu kuweka mchoro kama mfano, hapo kwenye A ilitakiwa iwe 12v lakini nataka nitumie 3volt. Nitashukuru kama nitafanikisha.View attachment 330515
Mkuu ulifanikisha project yako?
 
Msaada wa kiufundi, nina solar Panel 150w bettry N100. Matumizi yangu kwa ujumla hayazidi Watt 120. Nimepata Inverter ya 750W. Je inafaa kwa matumizi hayo., je inveter haiongezi matumizi ya Betry?
 
Msaada wa kiufundi, nina solar Panel 150w bettry N100. Matumizi yangu kwa ujumla hayazidi Watt 120. Nimepata Inverter ya 750W. Je inafaa kwa matumizi hayo., je inveter haiongezi matumizi ya Betry?
Battery moja la N100 halitoshi, inverter ni kubwa kwahiyo upoteaji wa umeme kwenye transformer ni mkubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom