Darasa la saba hali ni tete

usiniguse

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,532
2,000
Kufuatia matokea yaliyotangazwa na serikali na kujisifu kuwa ufaulu umeongezeka mwaka huu,ukweli ni Kwamba zoezi la kuchagua wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani 2014 limesimama kwa baadhi ya mikoa ili kusubiri tamko la serikali kushusha alama za ufaulu.
kwa mkoa wa lindi maafisa Elimu wamerudi vituoni kusubiri ruhusa ya serikali ya kushusha alama za ufaulu kwani baadhi ya shule zimekosa wanafunzi kabisa

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
480
250
Jamani serikali yetu tukufu, yenye viongozi waheshimiwa sana, inataka kuona matokeo makubwa sasa. Sasa kesho, wala kesho kutwa, bali ni sasa. Na ili kupata matokeo haya makubwa SASA, kila mtoto aliyehitimu elimu ya msingi anastahili kwenda sekondari. Kama alivumilia miaka yote 7 kukaa katika majengo bila elimu, atashindwaje kuvumilia miaka 4 ya sekondari. Idumu Big Results Now!!!!
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
6,954
2,000
Kwani kuna kosa gani madarasa kubaki tupu?Hiyo ndio fundisho kwa wanaopoteza mda shuleni.
Kuna chuo kikuu Africa kilishindwa kudahili baada viwango vya ufaulu kuwa chini.
 
Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
5,544
2,000
Kufuatia matokea yaliyotangazwa na serikali na kujisifu kuwa ufaulu umeongezeka mwaka huu,ukweli ni Kwamba zoezi la kuchagua wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani 2014 limesimama kwa baadhi ya mikoa ili kusubiri tamko la serikali kushusha alama za ufaulu.
kwa mkoa wa lindi maafisa Elimu wamerudi vituoni kusubiri ruhusa ya serikali ya kushusha alama za ufaulu kwani baadhi ya shule zimekosa wanafunzi kabisa

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
Labda kwa mikoa ya kusini,huku kwetu mwanza km watoto 700 wamekosa nafasi ya kuungia kidatto cha kwanza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom