Jc Simba
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 300
- 423
Kuna kijana alishikwa na kiu kali akiwa msituni kwa bahati alikua na kikombe, akiwa chini ya mti aliona matone ya maji yakidondoka juu ya mti akaona nafuu imempata,
Akakichukua kikombe na kuanza kukinga matone hayo mpaka yakafika nusu ili anywe,Ghafla akatokea ndege akakipiga kikombe cha maji aliyoyakinga kikaanguaka na maji kumwagika.Kijana huyu akasikitika sana na kulia.
Akaanza kukinga tena ndege huyo akafanya tena mara mbili zaidi.Kijana akakasirika akafanya namna zote akamuua ndege huyo,
Alipomaliza kumuua ndege..Mara akaona nyoka mkubwa akishuka kutoka katika mti ambao ndipo matone yalikua yakitoka kumbe matone yale yalikuwa ni mate na sumu ya nyoka.
Kijana akaumia sana moyoni kumuua ndege ambaye Mungu alimtumia kuokoa maisha yake kwa kupiga kikombe cha maji ambayo yalikua ni sumu ya nyoka.
Katika Maisha kuna mambo tunayaona ni mazuri yatusaidie ila ni sumu.tukiyakosa tusiwaumize wenzetu lakini tambua kwamba Mungu anajua hatari zinazotuzunguka na huwatuma watu au vitu mbali mbali kwa ajiri ya kutusaidia kuepuka mambo yanayotudhuru au kupata mambo tunayotamani kwa kulinda uhai wetu dhidi ya hatari tusizozijua kiroho.
Mungu Akulinde na sumu ya nyoka .Sisi ni watu Maalum wa Mungu.kama umeguswa na ujumbe huu share darasa hili na kwa wenzio ili waache kuuwa ndege waliotumiwa na Mungu kuokoa maisha yao.Ameeen