GE2025 Daraja la Mkuyuni; Mgombea Urais kupitia CCM (Rais Samia) atakua na hoja gani Oktoba 8, 2025 ili wananchi wakamsikilize

GE2025 Daraja la Mkuyuni; Mgombea Urais kupitia CCM (Rais Samia) atakua na hoja gani Oktoba 8, 2025 ili wananchi wakamsikilize

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Okk

Senior Member
Joined
Dec 29, 2024
Posts
171
Reaction score
421
Kwa jiografia ya Mwanza, mji huu una njia kuu mbili za kutoka katikati ya jiji na kuliunganisha jiji la Mwanza na mikoa jirani, yaani kwa kifupi hizi njia mbili zikipata hitilafu, mji hauingiliki wala kutoka, inakua kero tupu.

Daraja la Mkuyuni kwa msiofahamu lipo njia kuu ya Mwanza mjini kuelekea Nyegezi, njia kuu ya uchumi na kitovu cha biashara Mwanza maana linaiunganisha Mwanza na mikoa yote ya nchi hii moja kwa moja isipokua Mara na Simiyu ambayo iaunganishwa moja kwa moja na njia ya lilipo daraja la Mabatini ambalo nalo halifanyi kazi.

Ndugu msomaji vuta picha ya barabara muhimu sana kama hii ya Nyegezi kwenye jiji halafu haipitiki, then unasikia Mgombea Uraisi na Raisi wa jamhuri ya muungano anaenda huko kufanya mikutano ya kampeni, unajiuliza atakua na hoja ipi ya kufanya watu wachache waliobaki washawishike kutoka siku ya tarehe 29 kwenda kumpigia kura, ikiwa tu kidaraja kidogo cha kujenga ndani ya mwezi mmoja ni takribani mwaka sasa hakuna lolote.

kwa taarifa nyingine, kidaraja hicho ni kile ambacho hua kinajaa maji mvua ikinyesha na kimeungana moja kwa moja na ziwa Victoria, wengine wanasema ni bora wangekiacha vile vile maana mvua hainyeshi kila siku kuliko kukibomoa na kuleta kero sasa yapata mwaka mzima na hakuna matumaini.

Kwenye ziara yake iliyopita jijini Mwanza nadhani ilikua June 2025 mheshimiwa Raisi hakuambiwa ukweli, walimdanganya wakampitisha njia za pembezoni na hivyo hakuuona ukweli, ni wakati sasa wa kutoa kauli kuhusu daraja hilo.

Raisi anza na msimamizi mkuu wa barabara hiyo na mamlaka ya mkoa, pili nyooka na mkandarasi akwambie shida ni nini, nafahamu wewe si kama yule mwendazake pengine watendaji wanakuchukulia poa, lakini katika hili toa kauli.

sisemi kwamba kwa kutoa kauli utapata kura nyingi la hasha, kura ni siri ya kila mmoja wetu, na kwa hali niliyoiona kule nilipoenda kuzuru, kura zako nadhani ni za kuokoteza maana watu wengi walishajikatia tamaa. Lakini huwezi kuongelea maendeleo ya jiji la Mwanza bila barabara ya Nyegezi, maana ni njia kuu ya usafirishaji kutoka na kwenda mikoani.

NB: Ikikupendeza sana Raisi na mgombea uraisi wa JMT, fanya kama ulivyofanya kwenye mwendokasi Daresalaam, watu wamechoka sana wanasubiri nani wa kumfunga paka kengele tu, warudishie matumaini, hata ikiwezekana kabla ya tarehe 29/10/2025 daraja liwe limekamilika

Ni hayo tu
Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom