Daraja la Kamishango–Muleba ambalo limegharimu Bilioni 12.5

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
506
Reaction score
806
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amekagua ujenzi wa Daraja la Kamishango lililopo katika Kata ya Ikondo, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera. Mradi huo umetajwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 12.5.
IMG_20260329_204743_071.jpg

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kihongosi amesema fedha zilizotumika kujenga daraja hilo zimetolewa na Serikali ya Tanzania, akibainisha kuwa licha ya kutajwa kuwa na ufadhili wa Benki ya Dunia, bado ni mkopo ambao taifa litalazimika kuurejesha.

Kihongosi ameeleza kuwa daraja hilo ni mkombozi kwa wananchi wa Muleba, likirahisisha usafirishaji, kukuza uchumi wa eneo hilo, na kuokoa maisha ya wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za kuvuka eneo hilo.
IMG_20260329_204743_023.jpg

Aidha amewataka wananchi kushirikiana na serikali pamoja na CCM katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo dhidi ya vitendo vya uharibifu na wizi wa vifaa, kama taa na mifumo ya nishati ya jua. Pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu.

Itakumbukwe mwazoni mwa Mwezi January 2026 Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Mhandisi Julius Ryoba Festo alieleza kuwa daraja la Kamishango lina mita 45, upana mita 11.1 ambapo lilikuwa limefikia asilimia 97 ya ujenzi.

Pesa za ujenzi huo ulianza kufuatia ufadhiri wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa dharura (CERC PROJECTS ) ambapo ilitangazwa kutolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 45.6 kwa ajili ya kutekeleza miradi mitano ikiwemo Daraja la Kamishango ambalo limetajwa kugharimu Bilioni 12.5.
IMG_20260329_204743_741.jpg
 
Pamoja na contradiction ya hizo gharama lakini ilo eneo la mto ngono lilikuwa korofi sana bora aise kwasasanyumbani kunaendeka vizuri .
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amekagua ujenzi wa Daraja la Kamishango lililopo katika Kata ya Ikondo, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera. Mradi huo umetajwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 12.5.
View attachment 3564257
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kihongosi amesema fedha zilizotumika kujenga daraja hilo zimetolewa na Serikali ya Tanzania, akibainisha kuwa licha ya kutajwa kuwa na ufadhili wa Benki ya Dunia, bado ni mkopo ambao taifa litalazimika kuurejesha.

Kihongosi ameeleza kuwa daraja hilo ni mkombozi kwa wananchi wa Muleba, likirahisisha usafirishaji, kukuza uchumi wa eneo hilo, na kuokoa maisha ya wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za kuvuka eneo hilo.
View attachment 3564258
Aidha amewataka wananchi kushirikiana na serikali pamoja na CCM katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo dhidi ya vitendo vya uharibifu na wizi wa vifaa, kama taa na mifumo ya nishati ya jua. Pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu.

Itakumbukwe mwazoni mwa Mwezi January 2026 Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Mhandisi Julius Ryoba Festo alieleza kuwa daraja la Kamishango lina mita 45, upana mita 11.1 ambapo lilikuwa limefikia asilimia 97 ya ujenzi.

Pesa za ujenzi huo ulianza kufuatia ufadhiri wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa dharura (CERC PROJECTS ) ambapo ilitangazwa kutolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 45.6 kwa ajili ya kutekeleza miradi mitano ikiwemo Daraja la Kamishango ambalo limetajwa kugharimu Bilioni 12.5.
View attachment 3564260
Gharama walizotumia katika msafara huo kuja 'kuliona' hilo daraja ni kubwa kuliko gharama halisi za ujenzi wa daraja husika, bilioni 12? Mambo ya kula kwa urefu wa kamba.
 
"Engono yahabha"
Huu msemo una maana gani enyi ndugu zangu wahaya?
 
🤣🤣🤣 so kama hilo daraja ni BL 12' lile daraja la Wami situtaambiwa ni Trillion 30
 
"Engono yahabha"
Huu msemo una maana gani enyi ndugu zangu wahaya?
Mto wa Ngono uliopotea, ni msemo wa zamani unaohimiza umoja na ushirikian9, unakataza tabia ya ubinafsi na kujitenga ukirejerea huo mto kuwa ulijitenga na mito mingine kwa kufuata njia yake hadi ukapotea
 
Imeelekezwa wezi watajwe ili waone aibu.
Sijui na yeye atajitaja?
 
Back
Top Bottom