DAR WATU WANAPUMZIKA LINI NA STAREHe

mkuu jamaa wanahudhuria huko kila siku,kama wewe huwa unalala mi nakwambia wanaenda,jaribu kuzunguka huko utakuta mtu nyomi,mfano hiyo jumatatu jahazi nenda ddc magomeni.utakosa hata pa kupita jinsi kulivyojaa.

Msisaau :welcome::welcome: jumamosi ya tar 22 apa Vatican City
 
Na isitoshe mtu huyohuyo,na usiku mmoja,anaanzia let say kona bar baada ya mda kidogo utaskia ngoja
nkachungulie MEEDA meeda anakunywa bia mbili baada ya mda kidogo ngoja nkachulie SAN CIRO napo
bia mbili baada ya mda kidogo ngoja nkachungulie KWA MACHENI napo bia mbili baada ya apo ngoja
nkamalizie MANGO GARDEN akifika mango garden ni saa kumi alfajiri ebu niambie uyo mtu ofisini asubui
yake mtaelewana kweli?????????????:A S angry:
 
Na isitoshe mtu huyohuyo,na usiku mmoja,anaanzia let say kona bar baada ya mda kidogo utaskia ngoja
nkachungulie MEEDA meeda anakunywa bia mbili baada ya mda kidogo ngoja nkachulie SAN CIRO napo
bia mbili baada ya mda kidogo ngoja nkachungulie KWA MACHENI napo bia mbili baada ya apo ngoja
nkamalizie MANGO GARDEN akifika mango garden ni saa kumi alfajiri ebu niambie uyo mtu ofisini asubui
yake mtaelewana kweli?????????????:A S angry:
saa ingine anapiga na supu kiria bar saa 12 asubuhi akirudi homu ni mswaki tu juu juu kisha anaulamba huyo anaingia job na akienda saa nne lazima akazimue
 
BARNOMA.JPG BARNOMA.JPG
jumanne saa tano asubuhi jamaa na ulabu
NA HEMED KISANDA
Hii ndiyo Bongo bwana, wenyeji wa jiji la Dar es Salaam wanamisemo mingi ya kulitukuza jiji lao na mara nyingi utawasikia wakisema ‘tumia Bongo uishi Bongo’wakimaanisha kuwa ili uweze kuishi maisha safi ukiwa ndani ya jiji hili basi inakubidi utumie akili nyingi, achilia mbali kujifunza utapeli wa hapa na pale.

Licha ya kuwa jiji liko kwenye moja ya nchi maskini duniani ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane,lakini limeendelea kuwa ni moja ya miji mikubwa yenye umaarufu wa starehe kuliko maendeleo yake kimazingira.

Hii inaamanisha kuwa wakazi wengi wa Bongo wanapenda kustarehe zaidi kuliko kufanya kazi, hivi sasa hapa jijini imeshakuwa kawaida kukuta watu wakiendelea kuchapa kilevi (Kunywa pombe) muda wa kazi na mambo yakawa safi kama kwamba walikuwa kwenye ofisi zao siku nzima.

Unapotembelea mitaa ya Sinza, Kinondoni, Tegeta, Mbezi Beach, Temeke utakuta siku hizi baa zipo hatua chache kutoka ilipo nyingine na si ajabu kukuta baadhi ya baa zilizoko meneo hayo zimefurika watu wakipiga soga na juu ya meza zimetapakaa bia lakini ukiangalia saa yako mkononi utagundua kuwa ni saa za kazi na hapo ndipo utakapo jiuliza maswali mengi kuwa watu hawa wamefanya kazi wakati upi?

Haielewiki hali hii inasababishwa na nini, uvivu wa wananchi ama hali ya amani iliyopo hapa nchini ndiyo inasababisha watu kujisahau na kuhisi maendeleo ya nchi yanapatikana baa na siyo kwa kufanya kazi kwa bidii kwenye shughuli zao za kuzalisha mali.

Lakini Kitu cha ajabu ni kuwa wakazi na wenyeji wa jiji la Moscow huko nchini Urusi ndiyo wanashikiria rekodi ya ‘wapiga mtungi’ (walevi) kuliko sehemu nyingine yoyote duniani lakini mbona wako juu kimaendeleo?

Maswali bila majibu: Tufanye nini Bongo ifanane na Tokyo ama Seoul?, ishu ni viongozi wabovu ama uzembe wa wananchi kwenye kazi kwa kukimbilia ulabu, hakuna mtu kutoka Ulaya ambaye atakuja kutuelezeka tufanye kazi kama sio sisi wenyewe.

Iliwahi ripotiwa kuwa wafanyakazi wa idara za Serikali na sekta mbalimbali huko nchini Japani hufanya kazi masaa 24 ndiyo maana wameweza kufika hapo walipo. Je, mfumo huu unafaa kuigwa hapa Bongo? Je, Wabongo watalipokeaje hili endapo litapitishwa?

source:global publishers
 
na wewe shem unapumziika lili
shem upo?mi ni weekend tu ndio naburudika kwa nafasi,tena hata marafiki wananishangaa nnavozichapa,na huwa nawaambia mkienda kwetu ndio mtajua siri ya urembo maana hii ni kama maji ya kunywa.
 
............ Ijumaa mpka jumapili mchana na jioni vikao vya harusi, ndugu vyama nk....

Tufanyeje sasa kama kuanzia top kwenyewe kwa Mhe. Presida ndo hivyo hivyo kujirusha?..kama baba na Mama wanatoka kwenda kujirusha nje ya nchi sie tupo hapa nyumbani bana makamuzi kama kawa!!
 
Wabongo twapenda sana starehe kuliko kazi
Si kweli tatizo kubwa hapa ni ajira hakuna watu wanalewa maana hajui kesho akiamka anaenda, na kwa utafiti wangu wengi unaowaona mabaa usk siku za kazi ni madalali na day work{dei waka} ambao ni kundi kubwa
 
dah haya wakuu programu inaendelea jumanne sasa ni ngwasuma pale billicanass enendeni mkaendelee kuchoma pesa zenu enyi wana wapotevu,kwani mchunga kondoo mwenyewe kaacha kondoo zake na kukimbilia ughaibuni kila siku.
 
mi mgeni hapa Dar,ina maana watu wa mbagala, Temeke , kigogo ,mburahati kwa mtogole,kijichi hawaendi ktk starehe hizo isipokuwa watu wa sinza,kinondoni na knyama tu?nisaidieni wajameni
 
Duh,imeleta raha moyoni na kicheko cha haja,mazee wapendwa msemayo,mimi naona ni sahihi,kila mtu anamipangilio yake hapa mjini,haiwezekani maskini aneyeishi kwa kiwango cha nusu dola ayaweze makuu haya,pia kuna watu wengi bongo,haiwezekani wote wakajirusha kwa siku moja kama babu kijana alivyochangia,pia wengine wale mapopo,wapo kikazi zaidi,na wengine mapopo wao hawana dili, tayari starehe ipo kwenye damu,hata kama hawana pesa.kwa kweli pia kuna wengine wao wamezidisha,kila siku starehe ndio kwao,wajirekebishe tulikomboe Taifa letu nafasi zisichukuliwe na wageni.:angry:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom