Dar: Polisi wa Magomeni, inadaiwa wamemuua mahabusu, pamoja na kupigwa sana hajapelekwa Mahakamani wala Hospital

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Heshima kwenu wakuu,

Kuna taarifa zinadai kwamba Polisi wa Kituo cha Magomeni wamemuua mahabusu waliyekuwa wanamshikilia. Marehemu anajulikana kwa jina la Ramadhani aka Ramso.

Ramso alikamatiwa Kinondoni usiku akiwa na Mwanamke, huyu mwanamke hajajulikana sababu alikimbia, kisa cha kupigwa inadaiwa aliwajibu vibaya.

Baadhi ya Mashuhuda wanasema, Ramso kapigwa na Sungusungu na Polisi walikuta kapigwa.

Kupigwa sawa, ninqchojiuliza ni kwanini Polisi hawajampeleka Hospital wakati waliona hali yake ni mbaya?

Ramadhan alikamatwa jumatatu usiku wa kuamkia jumanne, asubuhi ndugu walienda kumuwekea dhamana ila Polisi walikataa kwa kile walichodai kwamba Ramso ni Jambazi Sugu.

Ramso yeye anajishughulisha na kazi za Udereva jijini dar.

Ilipofika Jumatano, ndugu wa Ramso walipigiwa simu na Polisi kwamba waende kumchukua ndugu yao bila masharti yoyote wala dhamana. Walipofika wakampakia kwenye bajaj. Ile anaingia kwenye bajaj akakata roho.

Ikabidi wamshushe, Polisi wakampakia kwenye gari la Polisi na kumpeleka Mochwari. Ndugu walipouliza mumempeleka wapi, waliadai Mwananyamala. Walipofika Mwananyamala Hospitali hawajakuta mwili wa ndugu yao. Kumbe Polisi walidanya, mwili ulipelekwa Muhimbili na ndipo ulikutwa. Wakakuta wameandikisha kule Muhimbili kwamba ni jambazi limeokotwa likiwa limepigwa na wananchi wenye hasira kali.

Mwili wa Ramso umesafirishwa kwenda kuzikwa Mkoani huko Masasi

My take;

Mambo sasa naomba utakapoongea na Wanahabari mtolee ufafanuzi hili swala tujue ukweli ni upi.

Nakemea na kulaani hii tabia ya Polisi kujichukulia Sheria mkoni. Juzi kule Mara waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola alikemea pia hili swala.

Sisi raia ni ndugu zenu, acheni kutupiga na kutuua.

Mahakama zipo na zinatenda haki. Je sisi raia tujifunze nini kutoka kwenu?

Nakala kwa;

*Kangi Lugola

*IGP Sirro

*Mambosasa.

*Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro.

Naamini taarifa imefika na tutapatiwa majibu kama ni tuhuma za kweli kwamba amekufa bahati mbaya au amepigwa.
 
Screenshot_2018-08-16-22-15-11.jpg
tapatalk_1531465620116.jpeg
tapatalk_1532184352917.jpeg

Naomba kuwasilisha
 
mwendawazimu kapewa rungu .... ..... either ..... tutakoma au tutakomaa au tutahama ... ..... ..... moja wapo... .!....
 
Yaani hawa polisi omba Mungu usiingie kwenye anga zao hata kwa bahati mbaya watakuua tu kwa kipigo. Maana hii ndio imekua desturi yao awamu hii ma mwisho wa siku wakubwa zao wanawatetea hakuna hata mmoja atayewajibishwa.
Usipopata haki yako duniani utakija kuipata ahera maana Mungu hana sifa ya dhulma hata kidogo.
 
Back
Top Bottom