DAR: Majambazi wavamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia, wapora fedha na vifaa vya kuendeshea misa

Habari picha kwa msaada wa Muungwana blog.
Screenshot_2018-04-05-12-09-47.jpg
Screenshot_2018-04-05-12-09-53.jpg
 
Wahusika inadaiwa wamekojolea na kunyea sanamu na maji ya baraka!
Kweli bangi na madawa ya kulevya ni hatari..
 
Dah vyuma vimekazi kweli. Ila nanyie Kwanini hizo pesa amkupeleka Bank kuhifadhi jumanne Bank ilikuwa wazi, kawaida baada ya Misa kwisha pesa zinahesabiwa. Pole kwa matatizo
 
Majambazi wamevamia na kuvunja kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, na kupora fedha na vifaa vya kuendeshea misa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo majambazi hao waliingia kanisani hapo na kuiba vitu hivyo, ikiwemo fedha za sadaka zilizokusanywa tangu sikukuu za pasaka mpaka sasa.

“Ni kweli nimepokea simu kuwa kuna hilo tukio, ni vibaka wameingia hapo kanisani na kuiba pesa na baadhi ya vitu, pesa ambazo zilikuwa za sadaka tangu sikukuu, ila thamani yake bado hatujaijua kwa sababu ndio tukio limeripotiwa sasa, baada ya muda nitakuwa na taarifa kamili”, amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuwabaini waliohusika na tukio hilo, ili kuwafikisha mbele ya sheria.
kanisa.jpg
 
Itakua sio majambazi hao. Kuna namna hapo
Siku zote ukiibiwa kama hivi au kwenye boma lako, lazima mhusika ni mtu wa karibu, lazima...
Kama kawaida ya polisi, wataanza na walinzi, watunza sadaka, padri etc etc...
Mtasikia tu waliopanga njama ni wa pale pale kanisani...
Dini haigopewi kama zamani, labda sababu nasi tunavyoitumia dini siku hizi, kulazimishana michango kede kede, hasa ile ya jumuiya, kuumizana kwa kisingizio mwenzetu ahudhurii kanisani, nafikiri haya mambo ya kipuuzi tuliyoyaingiza yamemfanya muumini kuona ni sisi tunaoiharibu dini au dhehebu, inasikitisha sana...
 
Back
Top Bottom