DAR kuna vita: Tanzania inakwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAR kuna vita: Tanzania inakwenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Huduma, Oct 9, 2008.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAMIA ya askari wa FFU na magari yaliyomwagwa majiani hivi sasa (asubuhi hii) inaonesha kama vile Tanzania inayodaiwa kuwa kisiwa cha amani Afrika ghafla bin vuu imegeuka Soweto au Guguletu, Afrika Kusini.

  Kisa. Kijimaandamano cha CUF? Mmmh, huyu bwana waziri sijui ni wa ndani au wa ndani kabisa (CCM) anaonesha kama vile ni zao la Marekani na vita vya ugaidi. Hawa ndio ile aina ya watu wanaofaa kuogopwa kama ukimwi. Pengine zaidi ya gonjwa hilo. Maana wanamwabudu Mmarekani. Jamaa ambaye yeye kila kitu chake tokea kuwamaliza wenyeji asili wa bara la Marekani ni ubabe ubabe na miiguvu na kujiona wao ni zaidi kuliko mtu mwinginie. Bahati mbaya iliyoje kuwa na viongozi kama hawa.

  Kumbuka huyu Waziri anayesambaza magari kila kijia na kila barabara jijini hii leo ndiye huyo huyo ambaye wizara yake inashindwa:
  . Kuwalinda wananchi katika majumba yao. Kiasi leo hata Zanzibar watu wanauawa ovyo? Kwingineko itakuwaje?
  . Kutulinda tunapokuwa barabarani na magari mabovu na uendeshaji mbaya.
  . Kuzuia rushwa miongoni mwa askari wa usalama au ufisadi mdogo mdogo barabarani,
  . Kuwalinda watoto, walemavu, wazee na wanyonge katika pitapita zao za malezi, mafunzo na kutafuta maisha.
  . Kuzuia majambo na vitendo vinavyosababisha vifo vya watoto wetu mashuleni na mitaani,
  . Kuuawa ovyo kwa maalbino,
  . Vituo vya polisi kuwa vituo vya kukamua rushwa,
  . Kuzuia madawa ya kulevya kuendelea kuwatesa wenetu
  . Kuwa na utu na ubinadamu katika magereza na jela zetu,
  . Kuzuia uonevu wa wenye nacho dhidi ya wasio nacho,
  . Kuleta usalama na amani ya kweli miongoni mwa wananchi na hata wageni waliopo nchini mwetu.

  Uongozi bora na safi ungelikuwa sikuzote una hakikisha matumizi bora ya polisi katika kulinda jamii na hasa familia zikiwa majumbani; watoto, wazee na wengineo wakiwa mabarabarani na wanyonge na dhaifu katika jamii pale wanapoonewa au kunyimwa haki zao na WALA SIO KUWAJAZA POLISI mabarabarani pale tu panapokuwa na maandamano ya amani ambayo chama tawala kinaogopa yatakiharibia jina au nafasi yake ya kwanza katika jamii!
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Unaposema dar kuna vita hivyo vita nani ametangaza ? Hao cuf na vyama vingine vya kisiasa vikiambiwa hakuna maandamano maana yake hakuna , mambo ya kulazimishana ni katika kuchochea na kuhalalisha uhalifu na ufisadi mwingine

  cuf acheni fujo mkiendeleza fujo tutawafuata hata katika vyumba vyenu huko mlipo au mtakapo kimbilia
   
 3. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa post yako,nafikri sasa walipakodi kimefika kipinda cha kupaza sauti kwa nguvu kwa watawala wetu kubana matumizi ya rasilimali kwenye maeneo yasikuwa na tija.Tuache mfumo wa kuamuru vikosi vyetu tuanze kuwasiliaana na walipakodi kuwajibu mara moja kwa kupitia vyombo vya habari.Njia hii ni bora zaidi kuwasilisha maoni kati ya watawala wetu na wananchi wao kuepuke fikra kwa walipakodi kuwa wanapuzwa.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani hao askari si wamemwagwa kwa ajili ya kulinda mkutano? Au wanapiga watu?
   
Loading...