Dar kukumbwa na uhaba wa maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar kukumbwa na uhaba wa maji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 22, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  KAMPUNI ya Usambazaji wa MajiSafi katika Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani, (Dawasco) limesema Jiji la Dar es Salaam litakabiliwa na uhaba wa maji kwa siku kadhaa.

  Kufuatia hali hiyo, kampuni imewataka wakazi wa mkoa huo, kutumia maji kwa umakini katika kipindi hiki ya kuifanyia matengenezo ya mifumo ya umeme katika mtambo wa Ruvu Chini.

  Mtambo huo ulizimwa jana , ili kuruhusu makandarasi kuhamisha mfumo wa umeme.

  Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Ofisa Mawasiliano wa Dawasco, Thed Mlengu. alisema matengenezo hayo yatadumu kwa siku kadhaa na kwamba wananchi watakaoathiriwa ni wa maeneo ya mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.

  “Kuna mradi wa wa upanuzi wa mitambo ya kuhamisha mifumo ya umeme wa bomba la Ruvu Chini, lengo ni kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo jirani yanayopata maji kutoka kwenye mtambo huo,”alisema Mlengu.

  Alisema maeneo mengine yatakayoathiriwa na tatizo hilo ni Mlalakua, Mikocheni, Mwenge, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay,Magomeni, Upanga, Kariakoo, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Muhimbili, Ubungo na katikati ya jiji.

  Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wanatakiwa kuhifadhi maji ili kuhakikisha kuwa wanapata huduma hiyo bila matatizo hasa katika kipindi hiki cha matengenezo ya mtambo.

  Dar kukumbwa na uhaba wa maji
   
Loading...