Dar, Kimara: Nyumba yateketea kwa moto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,875
Heshima kwenu wakuu,

Kuna nyumba inateketea kwa moto maeneo ya Kimara Baruti.

Chanzo inadaiwa ni Hitilafu ya umeme.

Natoa pole kwa mwenye nyumba.

Je, Watanzania tunayo tabia ya kukata bima kwa ajili ya nyumba zetu?
IMG-20200128-WA0012.jpg


 
Pamoja na Bima swala la Maintenance kwenye mifumo ya umeme majumbani watanzania bado mwamko ni mdogo sana. ukiangalia nyumba inayoteketea kwa moto ni ya miaka 15 iliyopita na unaweza kukuta imeanzia juu ya Dari.
 
Ahsante kwa taarifa mkuu kuhusu moto kwenye nyumba hii its a sad news kwa waathirika wote na tunategemea hakuna aliyeumia kuanzia wanadamu hadi wanyama waliokuwa wanaishi ndani ya nyumba hiyo,mimi nina mtazamo tofauti kabisa kuhusiana na majanga haya,ajali zinatokea ILA nyingi zimesababishwa na sisi wenyewe wanadamu kwa kutokuwa na utaratibu wa kuishi kwa mujibu wa kisheria,angalia picha hiyo hiyo nyumba inaonekana imejengwa kwenye eneo ambalo ni vigumu mno kwa uokoaji kufanyika kwa haraka na ufanisi(tatizo la serikali zetu za mitaa kuruhusu ujenzi holela),ni wajibu wa serikali zetu za mitaa kuwa na vikosi vya uokoaji vyenye vifaa na utaalamu wa kupigana na majanga kama haya(vikosi hivi visiwe vya kijeshi na viwajibike kwa local council),huwezi kuhamia ndani ya nyumba mpya kama haina certificate inayotambuliwa kisheria kuhusiana na wiring ya nyumba,na hii ni muhimu mno kwa unayetaka kununua nyumba ni lazima ujihakikishie hili kuwa wiring ilifanywa na wataalam ,nguvu ya gas ni muhimu ila kuna sharia zake,mitungu ya ges ni lazima iwe nje ya jingo na safe,kama ipo ndani ya nyumba ni muhimu iwe secured na kila mtu ndani ya nyumba aelewe basic ya utumiaji wake;tusiwe tunakimbilia sababu ambazo tunaona kabisa kwa mazingira yetu sio rahisi ,bima ni muhimu but sio kila mtu atamudu kuwa nayo,ha... This issue ilitakiwa Halmashauri ya jiji ije na uchunguzi na kuchukua lawama hizi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom