Dar HAKUKALIKI

Leo niliamkia kigamboni. kuna joto balaa na nyumba niliyolala imejengwa na kuezekwa kwa zege, walikuwa wanajenga ghorofa wakaishia floor house. Sikilizia hilo tanuri style wakati zege linapumua usiku...
Nikamuuliza mwenyeji inakuwaje hii maana ni karibu na beach akanambia upepo unapita juu na wao wapo chini ya usawa wa bahari, hii ni habari mbaya kabisa.

Inabidi nifungue biashara ya kutengeneza vipepeo lakini wabongo noma wanajipepea na magazeti ya udaku
 
hivi na wale polisi kule kwenye nyumba zao za nanihii inakuwaje
 
yaani bado hujazoea tu joto la dar au unasafiri mara kwa mara. pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…