Dar es Salaam yaweza kuwa kijani tukiamua

jmapunda

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
731
2,923
Ndugu zangu ingawa jiji letu la Dar linazidi kujaa maghorofa ya kila aina bado linakosa kitu muhimu sana ili livutie...Linakosa miti.Lipo tupu...hakuna hewa nzuri ya kuvutia.

Linapoteza kwa kasi uoto wa asili. Nashauri mamlaka zinazohusika zihamasishe wananchi wapande angalau mti moja mbele ya nyumba zao. Na kila taasisi zipande miti ya kutosha kwenye maeneo yao.

Ikiwezekana zitungwe sheria ndogo ndogo kusimamia hili.Imefika mahali mtu anaona bora akate miti kwenye eneo lake ajenge fremu!Joto hili linalotesa lingepungua sana.
Nawasilisha.
 
Naona wameanza kuweka fence kwenye bustani za nyasi barabarani ili zisikanyagwe ni hatua nzuri.
 
ukikaa maeneo ya manzese,magomeni,kkoo kama una pua ndogo unaweza kufa, amna hewa kabisa
Utashangaa watu wameinua shingo kama twiga utadhani wanatazama kitu kumbe wanatafuta hewa. Comment yako imenichekesha sana maana inafika mahali unaona matundu ya pua hayatoshi kupata hewa unatamani yaongezeke ukubwa
 
Nikweli kabisa nivyema wahusika wa Mazingira wakaangalia hili na wakaweka mikakati ya kupata miche ya kitu,msimu wakupanda na uhamasishaji wa mtaa kwa mtaa ,kama usafi inawezekana y not green city
 
Nikweli kwa hali ya hewa ya Dar mvua ni nyingi na Joto lipo la kutosha miti aina nyingi itastawi bila shida.
 
Jiji la Dar ni kama hot pot...Mie nadhani zitungwe sheria kali za uhifadhi mazingira .
 
Back
Top Bottom