Dar es Salaam (Tz) Vs Nairobi (Kny)

DON SINYORI

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
511
417
Habari wana JamiiForums.
Kwa uzoefu mdogo nilio nao ngoja leo niache uvivu na niyaongelee majiji mawili makubwa na pendwa hapa Afrika mashariki yaani DAR ES SALAAM NA NAIROBI. Nitayaongelea majiji haya katika vipengele vichache kwani nimebahatika kuishi katika majiji yote kwa muda Fulani hivi karibuni.

USAFIRI:katika jiji la DSM usafiri ni changamoto kidogo kutokana na kuwa na msongamano wa magari hasa mida ya asubuhi na jioni. Lakini ujio wa mabasi ya mwendokasi umesaidia kwa kiasi kikubwa kero hii katika baadhi ya maeneo.
Katika jiji la Nairobi kwa kiasi Fulani usafiri ni mzuri japo kuna muda wa jioni na asubuhi ‘rush hour’ mambo huwa ni mabaya kidogo.kwa upande wa daladala za Nairobi ‘matatu’ zina ubora zaidi ukilinganisha na za Dsm.ubora huu upo katika minajili ya kwamba unaweza kulipia kwa credit card(sisi tumeanza mwezi ulopita),zina ’flat’screen nzuri katika kila daladala na nyingine katika kila siti, kuna huduma ya internet wi-fi bure kabisa,muziki mkubwa,daladala zote ni level seat yaani hakuna abiria kusimama.ukikutwa umesimama ndani ya daladala traffic hukutoza faini wewe abiria na sio dereva .kwa upande wa utumiaji wa usafiri wa anga siongelei kwani its obvious Jommo Kenyata International Airport ipo juu zaidi ya JNIA

HUDUMA YA MAJI; Kwa jiji la DSM maeneo mengi maji ni tabu japo kuna maeneo maji yapo hadi siku 3,4 za juma. Kwa upande wa Nairobi hali ni mbaya sana kwani maeneo mengi maji yanatoka mara moja au mbili kwa wiki.tena ndoo ya lita 20 ni shilingi zipatazo 50/= za Kenya au tsh 1000.

USWAZI(SLUMS). Kwa upande wa DSM maeneo ya uswazi niliyolenga ni kama manzese na mbagala. Umasikini upo ndio na uhalifu wa kiasi Fulani. Kwa Nairobi slums maarufu ni ghetto zilizopo Kibera na mathare. Huko hali ni mbaya sana.kama ulikuwa hujui Kibera ni ghetto ya pili kwa ukubwa Afrika baada ya SOWETO afrika ya kusini.katika maeneo haya uhalifu ni nje nje,watu wanauana kirahisi rahisi kwa ufupi matukio ni jambo la kawaida sana.huko ndipo kunaongoza kwa NGOs nyingi sana zinazofadhiliwa na wazungu

BIDHAA/MASOKO. Katika jiji la DSM bidhaa za vyakula gharama zake ni za kawaida sana wakati electronics zipo juu.lakini hali ni tofauti Nairobi kwani electronics ni bei nafuu ukilinganisha na Dar wakati vyakula ni ghali. Mf. Nilinunua Samsung GALAXY J1(dukani) kwa shilingi laki moja ya kitanzania.pia niliulizia flat ambayo dar inauzwa kwa laki 7,Nairobi ni about laki 4.5.soko la hisa la Nairobi liko juu na active sana.

UKABILA: ITS OBVIOUS kwamba DSM na TZ kwa ujumla hakuna ukabila. Lakini hali ni tofauti sana kule Nairobi na Kenya kwa ujumla.ukabila ni jambo la kawaida sana.watu wana favor watu wa kwao zaidi.ambapo wakikuyu na wajaluo ndo rivals wakuu

UWEKEZAJI. Katika jiji la DSM uwekezaji wa miradi ya kimaendeleo upo baadhi ya maeneo lakini ni wa kiwango cha kuridhisha kwani kuna majengo makubwa,mahoteli na vitega uchumi mbali mbali.miaka ya hivi karibuni kuna ongezeko la plaza kubwa.pia kwenye usafiri hali si mbaya sana uwekezaji unaridhisha.
Hali pia iko hivyo jijini Nairobi uwekezaji ni wa kasi zaidi. Plaza ziko nyingi zaidi,migahawa classic sana.pia mahoteli ni mengi sana Nairobi.masupermarkets na mabenki ni mengi sana ndio maana unaweza kuona benki na supermarkets kama NAKUMATT NA KCB (just to mention few) zikiwepo hadi baadhi ya maeneo ya TZ. Pia uwekezaji wa kilimo mfano maua na mboga na matunda ni mkubwa kwani wana export hadi ulaya. Pia uwekezaji katika usafiri ni mkubwa sana

MAKAZI(estates);kwa upande wa makazi jiji la DSM bado halijawa active sana kwani msongamano estates zenye apartments sio nyingi kiukweli.tunaona project tu huko kigamboni na kijichi etc. kwa upande wa Nairobi estates zenye apartment za hadhi ya juu kati na kawaida zipo nyingi sana japo ukweli ni kwamba gharama zake zipo juu mno.

MICHEZO: katika upande wa michezo DSM iko juu katika michezo michache sana sana soka.nadhani ni mfumo wa nchi nzima unafanya hali iwe hivi.kuna michezo bado tupo nyuma sana wengi ni mashahidi. Nairobi hali ni tofauti sana kwani michezo ni kipaumbele kweli kweli. Katika michezo kama Rugby,riadha,swimming,rally za magari na pikipiki na volleyball Kenya iko juu. Pia hata ligi kuu yao ya soka iko juu in terms of matangazo kwani inaonekana hadi katika televisheni za SuperSports tangu miaka ya nyuma

MAHUSIANO. Katika eneo hili DSM hali ni ya kawaida watu wanaoa katika umri wa kawaida average 29 yrs wanaume.maadili yanazingatiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa Nairobi nimeshuhudia wengi wanaoooa ni wenye umri mkubwa kidogo ukilinganisha na Dsm au Tz(kama unataka ushahidi zaidi fuatilia kipindi cha Samantha bridal star tv). Nadhani sababu pia ni gharama za harusi kwani Kenya harusi ya kimjini ni expensive mno average ni hadi 50-70 Milioni za kitanzania. Pia mapenzi au romance kwa wapendanao(especially youths) ni nje nje. Unaeza kuta wapo hata kituo cha basi au eneo la public na wanapigana mate au kuonyeshana affection waziwazi

KAZI: kwa upande wa kazi hali hairidhishi sana DSM kwani watu bado wako slow,wavivu, movement slow sana. Nairobi watu wanapiga kazi bana. Na hawataki utani. Mjini kila mtu yupo bize anatembea haraka na hataki hata kuwaste hiyo time ako nayo.kwenye kazi kila mtu yuko serious na smart kweli kweli kiutendaji

Unique features. DSM na Tz kwa ujumla kuna ukarimu sana na watu ni friendly. DSM iko balanced ktk ujamaa na ubepari.

Nairobi na Kenya kwa ujumla kuna bidhaa inaitwa mirungi au miraa asee inaheshimiwa sana.traffic barabarani hata haisimamishi ile gari imebeba hiyo.kampuni ya Toyota wamewatengenezea magari maalumu yenye kasi ili kuwahisha miraa from Meru to Nairobi. Vijana wengi huko wanakula sana mirungi.pia Huduma ya internet na wi-fi ipo almost kila sehemu.kuanzia kwenye nyumba za kuishi watu,karibu kila mgahawa na daladala’’matatu’’. Pia mabasi ya mikoani almost yote yana huduma hii bure kabisa. Nairobi imekaa kibepari zaidi na pengo ni kubwa kati ya maskini na tajiri. Pia uhalifu na uchokoraa ni vitu vya kawaida sana huko. Usije ukaenda sehemu unahitaji huduma hata kama unalipia ukasema naomba kitu Fulani.utaambiwa hatutoi msaada hapa. Nilienda kukata tiketi nikamwambia mtoa huduma nina shida ya tiketi akaniambia hatutoi msaada nenda unicef.nikamwambia si ninatoa hela,akaniambia we ni mtizedi eeh,nikaitika ndio akasema sema nataka na sio naomba au nina shida

HITIMISHO: kwa mtazamo wangu ukijumuisha aspect zote hasa ya kimaendeleo NAIROBI iko juu sana.tena mbali mno japokuwa mfumo ni wa kibepari zaidi. Hivyo WANA DSM(Watanzania) we have a lot to learn from our neighbours nashangaa viongozo wetu eti wanaiga sera na mfumo wa uchumi mara sijui wa Malaysia mara Japan eeeh.waende kwanza Kenya na Ethiopia.

Big up our neighbours Kenya. Personally I have and will learn a lot from you so as I can develop my self and my country

Kufikiria hakuhitaji hasira wala kutokwa na mapovu
rrr.jpg
indexj.jpg
indexhh.jpg
index.jpg
A_matatu.jpg
rrr.jpg
indexgg.jpg
index.jpg
A_matatu.jpg
 
Asante kwa mchanganuo mzuri, nakubaliana na wewe tu na pia umekuwa very objective bila kuandika kwa upendeleo. Maendeleo ni kweli ni makubwa zaidi Nairobi, lakini ni vizuri tukaelewa kuwa Dar maisha ni marahisi au hata niseme mazuri na hata watu maskini wanayamudu tofauti na Nai ambapo maskini hawana nafasi isipokuwa kwenye slums
 
Haha uko nairobi hayo ndio mabus yao ,izo paintings are kinda boring old sana they have to change
 
You are a real Kenya lover. Nothing but it all. That beating around the bushes won't help you for real. Say it, again and again, you love it!
 
Wakati mwingine kubalans inakuwa vigumu kidogo Dareslam ni kubwa hata mara mbili kwa Nairobi.
 
Kwa upande wa starehe Nairobi inatisha kumbi nzuri za kisasa za Nairobi balaa...
 
Subiri niwaite akina MK254 Iconoclastes IAfrika .....changamkieni tender hiyo!

Hehehe!! Hapo sitakawia kuchangamkia hiyo fursa....

Mleta mada amejaribu kuwa balanced na kuanika ukweli kwenye mambo mengi. Japo hilo la matatizo ya maji sina uhakika nalo maana maeneno ninayoishi maji ni ya uhakika muda wote. Labda maeneo mengine.
 
Back
Top Bottom