Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Prof Ally Marzui alipofika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kulikuwa na vuguvugu kubwa sana la Ujamaa na kujitegemea. Ikaanzishwa Shule ya Mawazo ya Dar (Dar es Salaam School of Thoughts) hasa nyakati za UMAJUMUI wa akina Prof Mlawa, Prof Shivji, Jeneral Ulimwengu, Hirji, Mama Meghji na wale waliokuwa wanafunzi hapo.
Kulikuwa na mijadala ama niseme debate za maana sana wakichambua Sera na mipango ya mataifa mbali mbali duniani. Sasa Prof Mazrui akaja. Akashangaa kumuona Rais wa Nchi Mwalimu Nyerere akishiriki mijadala hiyo pasipo kuwa na chembe ya woga. Wasomi wakimpiga vijembe vya kisomi na yeye akikubali na wakati mwingine akikubaliana kutokukubaliana.
Ndipo alipotunga kitabu kiitwacho "Tanzaphilia" kuonesha hali isiyoeleweka ya Wasomi na watawala wa Tanzania kulinganisha na kwingine, hasa akisema ijapokuwa Afrika hutawaliwa kwa sauti ya mmoja, lakini hufikiriwa kwa sauti na mawazo ya wengi.
Moja ya sifa makini ambazo najutia sikuzaliwa kipindi cha TANU, ilikuwa kutosheka kwa kujiringanisha hali ya kiongozi wa umma na mtu wa kawaida na kuwa na imani kuwa wote ni sawa. Lakini TANU ilijenga misingi bora kuanzia chini mpaka juu, ndio maana ilikuwa rahisi kukubaliana na kuridhiana katika fikra zao.
Sivyo kwa kizazi hiki kilicho na vyeti vya taaluma bila Maarifa vichwani mwao. Kizazi ambacho kinaona sifa makutank ya wanachama wengi bila kuwapo funzo la Itikadi za vyama vyao cha ajabu watu huanza kutafsiri itikadi za vyama kupitia hamasa za kishabiki.
Kupitia matendo ya waliojuu yao na hata vitendo vya wawakilishi wao, Jamii iliyosahau misingi ya utu wao haiwezi kutosheka, kwani matendo ya kibinadamu upandikizwa kwa mafunzo mema toka kwa watu wanaheshimu utu, kukumbatia vitendo vichafu vinavyoendelea ni kuruhusu hata kizazi toka katika viuno vyako kuishi bila imani na maono, jamii inaposahau ama kukosa mafunzo ya maadili na kufunzwa miiko ya utu kengeufu wa kimapokeo hasi, ni jamii ambayo haitakuwa salama abadani.!
Sifa ya kutosheka iliyoheshimika enzi za TANU ilianza kuumwa 1981 ikazikwa 1991 kaka yangu na dada yangu, Makunyansi ya taifa hili yataondolewa kwa mgongano wa mawazo na sio mmoja afiriki yeye na kutenda yeye kwaniaba ya wajinga walio wengi ijapokuwa taifa ni la wajinga.
Na Yericko Nyerere