Mwana wa Nuru
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 590
- 415
Uislaam ni "global", Qur'an imeandikwa kiarabu, lugha kubwa kuliko zote uzijuazo.
Jee, unajuwa kuwa hata Kiswahili unachotumia asilimia kubwa ya maneno yake yametokana na Kiarabu? jiulize kwa nini?
Umaskini tulioingizwa wakati wa Nyerere nna uhakika hujaona, wala foleni za wakati huo nna uhakaika hujaziona, umeshakaa foleni ya vibiriti wewe? Leo una foleni za neema na maendeleo za magari, unahaha.
Kuna ufisadi zaidi ya kupoteza watu wasijulikane walipo? Unayajuwa ya Kassim Hanga?
Chukuwa idadi ya wanafunzi woooooooote waliofaulu wakati wa Nyerere, nachukuwa idadi wanafunzi waliofaulu wakati wa Kiwete kwa muhula mmoja, tuwekee hapa, kama hujajiaibisha. Huwezi.
Kwa mara ya kwanza tunaiona Tanzania ikijitegemea yenyewe kwa asilimia zaidi ya 65. Jee, uliwahi kuiona ikijitegemea zaidi ya hivyo? weka ushahidi. Huwezi.
Jina lipi linalokupa shida> Barack Hussein Obama? au Jakaya Mrisho Kikwete? au Zomba? weka wazi. Huwezi!
Kwa kukupa darsa tu, tuko katika masiku ya "Mrisho" huu ndio msimu wake, kabla ya Ramadhan. Jee, unajuwa maana ya Mrisho?
Tatizo naona mtoa mada ni Almaamuma! hawezi kutofautisha kiarabu na uislamu.Hajui kuwa kiarabu ni lugha na kilikuwapo hata kabla ya uislamu kufikiriwa kuwepo.Hajui kuwa hata hicho kitabu anachokisemea kiliandikwa lini na kwa jinsi gani.Yamkini hajui hata kilichizisibu nakala zake halisi za kale zimefikwa na madhira gani. Sijui kama anajua hata ile hadithi inayoonesha uchina kuwa ni kitovu cha elimu wakati wa mtume na si arabuni au ulaya. Labda pia ana usubi hata kwa mambo ya kisiasa na kijamii ya Tanzania kwani utofautishaji wake wa awamu za uongozi wa nchiunatia shaka. Nyerere na Kikwete kamwe hawatalingana hata kwa namna ya kuwaza kwao tu. Namshauri mtoa mada asisumbuke na suala la udini kwani si issue kwa sasa,burning issue ni uchumi wetu unavyokua kwa wageni(wawekezaji) na kushuka kwetu kila mara chini ya uongozi thabiti wa chama cha mapinduzi. Mgeni wetu anaitwa Barack Hussein Obama hivyo labda ni mwislamu au wazazi wake, lakini haituhusu.
Uislaam ni "global", Qur'an imeandikwa kiarabu, lugha kubwa kuliko zote uzijuazo.
Jee, unajuwa kuwa hata Kiswahili unachotumia asilimia kubwa ya maneno yake yametokana na Kiarabu? jiulize kwa nini?
Huu ujumbe si umemwandikia Obama???? Atakuelewa? Sasa si ungeandika kiingereza? Au hakipandi?!!!
Imeandikwa Kijaluo.
Mod aifungue ile "Dar es Salaam" au aiunganishe na hii ktk ban?Kama ulikuwa na hizo 2,000 na unakaa foleni kwa kupanga matofali kuanzia saa kumi za usiku, na ikifika saa 5 kabla ya adhuhuri unaambiwa sukari hakuna hapa kuna "betri" za "National" ndio zimeletwa, piga hesabu ya hayo masaa uliyopoteza halafu uniambie hiyo bajeti ya 10,000 na unakipata ukitakacho bila kupoteza wakati, bila kutafuta jiwe wala btri bovu la kupangia foleni na bila "risk" ya kukabwa usiku na kina "Joni" Mgogo ukiiwahi foleni mtaa wa sita. Ipi bora?
Huujuwi uchumi, usiuongelee, utaaibika, hapa nna ongelea Obama kutotenda haki kwa tafsiri mbovu ya jina la jiji letu adhyim. Dar Es Salaam.
Moderator ifungulie id yangu ya Dar Es Salaam, roho mbaya tu.
Zoba bwana ana vituko kama nini
Zanzibar, ndio maana vikaitwa visiwa vya viungo, umeshakunywa chai ya karafuu?
Hata Adam na Hawa walianzia upuuzi wao peponi au huijui maana ya "dhambi ya asili"?