Dar-es-salaam chafu sana

Dar inahitaji mkuu wa mkoa mwenye akili mtaalamu wa ujenzi na mipango miji sio mpenda sifa na madharau anayetoa misaada yakuzuga kuwa mtu mwema! Atueleze ishu ya eya hosteji intapretenyuaa dewji imeishia wapi?
Raiz sio mjinga sana anauwezo wa kupambanua mambo japo kingreza ndo shida kwakweli
 
Dar mji mchafu sana kila mahali ni uchafu. Mji unanuka vibaya sana. Sijui wanadamu wanaishi vp kwenye huo mji.
 
Ile Kiki ya awamu hii ya tano waliyoingia nayo ya kufanya usafi iliishia wapi? Au hao watafuta kiki wameridhika na uchafu huu tofauti na ule walioanza nao?
 
πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½Hii ni kweli kabisa

Nipo Tanzania kwa sasa na mkoa wa Dr mchafu hakuna mfano. Hakuna utaratibu wowote wa utupaji uchafu na maeneo ya wazi yanakuwa kama dampo. Mkuu wa mkoa anashidwa kabisa na wengine kama Kilimanjaro!
 
Nimepita pale buguruni siku moja,nikamuona bibi amejichokeaa anafagia pembezoni mwa bara bara,halafu hana hata vitendea kazi,yeye mwenyewe anevaa malapa tu,nikabaki kusikitika !!!
 
Ile Kiki ya awamu hii ya tano waliyoingia nayo ya kufanya usafi iliishia wapi? Au hao watafuta kiki wameridhika na uchafu huu tofauti na ule walioanza nao?

Nikupe falsafa moja rahisi sana maishani. "DOnt trust the first 100 days". Usiamini siku 100 za kwanza, siyo tu kwenye uongozi wa nchi kama urais, ukuu wa mkoa na ngazi nyingine, bali hata kwenye ndoa yako, kazini kwako na popote pale. ANgalia sana mtu anapoanza kitu usimwamini sana ndani ya hizo siku. show off nyingi sana. Kwenye ndoa ndo kipindi cha kubebishana balaa, yaani unajiona uko mbingu ya saba. Kazini kama kaajiriwa bosi mpya utaona speed atakayoanza nayo atatembelea kila idara, ataita wafanyakazi ataongea nao na kusema maneno mengi matamu.

Subiri baada ya hapo ndo utaona uhalisia wa huyo mtu.
 
Nipo Tanzania kwa sasa na mkoa wa Dr mchafu hakuna mfano. Hakuna utaratibu wowote wa utupaji uchafu na maeneo ya wazi yanakuwa kama dampo. Mkuu wa mkoa anashidwa kabisa na wengine kama Kilimanjaro!
Ni muda mrefu toka Rais wetu mpendwa asafishe akiungwa mkono na wateule wake na sasa amechoka na wao wanasubiri aende tena mtaani waunge mkono juhudi. Wateule wake wa miji mingine nao bado wanasubiri huku hali ikiwa mbaya zaidi maana huko hafiki kujionea mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…