DAR ES SALAAM: Ahukumiwa kwenda Jela maisha kwa kosa la kuiba simu

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
[HASHTAG]#Habari24UPDATES[/HASHTAG], Kassim Salum (18) mkazi wa Dar Es Salaam, amehukumiwa kwenda Jela Maisha kwa kosa la kuiba simu aina ya Tecno (TZS 110,000) na kujeruhi.
 
Wahujumu uchumi waliokamatwa hivi karibuni walifutiwa kesi na mahakama kijana ameiba simu thamani sh.110,000 pamoja kujeruhiwa japokuwa simtetei muhalifu amefungwa kifungo cha maisha.
Mahakama katika hili hajatenda haki kabisa.
 
Sio mahakama ni sheria hata siku moja hakimu hatoi sheria mfukoni anatumia vifungu vya sheria iliyotungwa bungeni. Halafu mahakama huwa haifuti kesi kamwe wanaofuta kesi ni upande wa mashitaka kwa sab mbalimbali za kisheria kazi ya mahakama ni kumuachia mtu huru au kumtia hatiani na si vinginevyo.
 
[HASHTAG]#Habari24UPDATES[/HASHTAG], Kassim Salum (18) mkazi wa Dar Es Salaam, amehukumiwa kwenda Jela Maisha kwa kosa la kuiba simu aina ya Tecno (TZS 110,000) na kujeruhi.
Badilisha title iwe kosa la kujeruhi wakati akiiba simu acha kukuza mambo, kosa la msingi ni kujeruhi
 
nitawaambia wanangu" ni dhambi kubwa kuwa masikini, na mkiwa masikini basi moto wa kuzimu unawahusu"
 
We vipi mafisadi wamehukumiwa kwan? Mahakama ya mafisadi haina kesi ..mafisadi wanadunda mtaani dagaaa wanahukumiwaa
 
[HASHTAG]#Habari24UPDATES[/HASHTAG], Kassim Salum (18) mkazi wa Dar Es Salaam, amehukumiwa kwenda Jela Maisha kwa kosa la kuiba simu aina ya Tecno (TZS 110,000) na kujeruhi.
Acha kupotosha kwa lengo la kuichafua mahakama au sab zako binafsi. Hilo ni kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha (armed robbery) kwa kawaida mahakama haiangalii thamani ya kitu kilichonyang'anywa bali inaangalia kama kweli tendo la unyang'anyi na kujeruhi limefanyika. Kwahiyo mtuhumiwa amefungwa kwa unyang'anyi wa kutumia nguvu sio kwa wizi wa simu.
 
Back
Top Bottom