DAR ES SALAAM: Ahukumiwa kwenda Jela maisha kwa kosa la kuiba simu

Wanne kati ya watuhumiwa 10 kesi ya mauaji ya Dk. Sengodo Mvungi wameachiwa huru baada ya DPP kuondoa mashtaka dhidi yao- HT @ Nipashe
 
Sio mtaalam wa sheria ila sheria za bongo huwa pasua kichwa , kuna washkaji 4 singida walihukumiwa miaka 30 kwa kufanya biashara ya ndege wa porin bila kuwa na vibali wakati huo huo walimuuza faru John hawashtakiwa na waliokamatwa na pembe za ndovu walilipa fedha wakaachiwa huru. Kwel hii nchi ya wachache
 
Acha kupotosha kwa lengo la kuichafua mahakama au sab zako binafsi. Hilo ni kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha (armed robbery) kwa kawaida mahakama haiangalii thamani ya kitu kilichonyang'anywa bali inaangalia kama kweli tendo la unyang'anyi na kujeruhi limefanyika. Kwahiyo mtuhumiwa amefungwa kwa unyang'anyi wa kutumia nguvu sio kwa wizi wa simu.

Vipi kuhusu wanyang'anyi wanaotumia akili?
 
We vipi mafisadi wamehukumiwa kwan? Mahakama ya mafisadi haina kesi ..mafisadi wanadunda mtaani dagaaa wanahukumiwaa
Ukishamuita mtu fisadi maana yake ameshahukumiwa vinginevyo huyo ni mtuhumiwa wa ufisadi.
 
Kuna haja ya kuwa tunawapima "stress levels" mahakimu wetu kia baada ya miezi mitatu. Usikute hakimu wa watu wakati anatema cheche alikuwa anawaza ataishije (na kulipa karo za watoto) mpaka tarehe 28 Jan 2017 wakati mshahara alipewa tarehe 21 Dec 2016 na keshautumbua wote
 
Acha kupotosha kwa lengo la kuichafua mahakama au sab zako binafsi. Hilo ni kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha (armed robbery) kwa kawaida mahakama haiangalii thamani ya kitu kilichonyang'anywa bali inaangalia kama kweli tendo la unyang'anyi na kujeruhi limefanyika. Kwahiyo mtuhumiwa amefungwa kwa unyang'anyi wa kutumia nguvu sio kwa wizi wa simu.

Aliyeibiwa alipigwa ngumi,akasukumwa bahati mbaya akadondokea mafuta ya kuchomea chips akaungua mgongoni, hapo vipi adhabu ni sawa?
 
Aliyeibiwa alipigwa ngumi,akasukumwa bahati mbaya akadondokea mafuta ya kuchomea chips akaungua mgongoni, hapo vipi adhabu ni sawa?
Hapo siwezi kusema lkn kuna nafasi ya kukata rufaa kama anaamini ameonewa
 
[HASHTAG]#Habari24UPDATES[/HASHTAG], Kassim Salum (18) mkazi wa Dar Es Salaam, amehukumiwa kwenda Jela Maisha kwa kosa la kuiba simu aina ya Tecno (TZS 110,000) na kujeruhi.
khaaa! hiv ni laki na kumi au billion mia na kumi?? siamini kama kuna watu wanamuabudu Mungu huyu wetu sisi naamini wana wa kwao..
 
Wanasheria wetu hao Napata wasiwasi wakati muingine juu ya maamuzi yao muda mwingi wanafanya kazi kwa mashinikizo ya kutaka waonwe wanafanya kazi hawa angalii upande wa pili angekuwa ndugu yake angetoa hukumu ile? kuna maisha baada ya uanasheria wao huo
 
Back
Top Bottom