A
Anonymous
Guest
Barabara ya Bonde la Mchicha ambayo inatumiwa mara nyingi na Wakazi wa Tabata Kimanga, Mawenzi, Segerea, Kinyerezi, Bonyokwa hata Ukonga na Gongo la Mboto ni mbaya na imekuwa kero kubwa kwa Watumiaji.
Hii barabara ni kero kubwa kuwe na mvua au kusiwe na mvua. Kipindi cha mvua hata wapita kwa miguu hawawezi kupita inajaa mashimo makubwa matano.
Kipindi cha jua ina mashimo hasa hapo kwenye mpando darajani kiasi kwamba Umoja wa Bajaj ilibid wafukie mashimo.
Shida iko wap kwa TARURA kurekebisha barabara hii yenye kuunganisha maeneo yote haya? Hii iende sambamba na barabara mbovu ya Kimanga na kukosekana kwa Stand ya Mabus Kimanga.