Dar: Akamatwa kwa kusambaza kuku waliokufa kwa wauza chips

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Kijana mmoja mkazi wa Buguruni amekamatwa baada ya kubainika akiwa na kuku 78 waliokufa kwa ajili ya kusamabaza kwa wauza chips.

Alikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa kutoka kwa raia kuwa kuna mtu alikuwa anasamabaza kuku waliokufa kwa wauza chips na mighahawa.

Afisa Afya Kata ya Buguruni amesema baada ya uchunguzi kuku hao baada ya kuchunguzwa hawafai kwa matumizi ya binadamu kwa kuwa walikuwa wameshakufa.


 
Huyu atakuwa aliwaiba kwa hiyo alikuwa anawanyonga wakati wa kuwaiba ili wasipige kelele, hawa ni kuku wa kisasa
 
Nyamafu watu tunalishwa Sana ila hatujui tu,binadamu Wa sasa hivi Ni heri ya mnyama.
 
Mbona mmewala sana. Nendeni Kitunda halafu uliza kama Kuku wanaokufa huwa wanatupwa!
 
Kawaida sana hapa Shinyanga kuna jamaa anajiita Seifu kuku,anauza kwenye hoteli zote za Shinyanga hapa mikuku iliyochina maana anachinja lakini hana friji za kutunzia.Sasa mtu kama huyu hata akikuletea nyamafu huwezi kujua.kuku nunua mzima uchinje mwenyewe haya mambo ya kula nyama barabarani waachie wachina
 
Sijaelewa au??
Kabla ya kula si tunauwaa kwanzaa
Kibudu kinalika tuu vema km hakijaoza
 
Afu muuzaji Muislamu...anawalisha wenzie vibudu...
Mimi kuku tena basi...ntakula nilofuga mwenyewe
 
Back
Top Bottom