Dangote kununua kiwanda cha magari cha Peugeot

Dangote kununua kiwanda cha magari cha Peugeot

Majs

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
232
Reaction score
520
pic+dangote.jpg

Kwa ufupi
Kampuni ya Usimamizi wa Mali ya Nigeria (AMCON), iliyoundwa wakati wa kuyumba kwa benki, inakaribia kuuza Kiwanda cha Magari cha Peugeot cha Nigeria (PAN).

Mfanyabiashara tajiri Afrika, Aliko Dangote anasubiri idhini ya Benki Kuu ya Nigeria ili anunue kiwanda cha kuunda magari aina ya Peugeot akishirikiana na majimbo mawili.

Kampuni ya Usimamizi wa Mali ya Nigeria (AMCON), iliyoundwa wakati wa kuyumba kwa benki, inakaribia kuuza Kiwanda cha Magari cha Peugeot cha Nigeria (PAN).

“Tumeshakamilisha mchakato wote wa zabuni miezi miwili iliyopita na sasa tunasubiri idhini ya Benki Kuu,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa AMCON, Ahmed Kuru alipoongea na Reuters.

PAN, kiwanda cha kuunda magari kilichopo jimbo la Kaduna, kina ubia wa kiufundi na PSA Peugeot Citroen na kikiwa na uwezo wa kuunganisha magari 90,000 kwa mwaka.

Dangote, kwa kushirikiana na majimbo ya Kaduna na Kebbi na Benki ya Viwanda (BOI) waliomba zabuni ya kuwa wamiliki wakubwa wa hisa za PAN mwaka jana kutokana na AMCON kutaka kuuza baadhi ya mali zake ilizozichukua wakati wa matatizo ya taasisi za kifedha.

CHANZO: Mwananchi
 
Natamani kuwa kama huyu jamaa wani dei lazima iwe its matter of time tu .

Nakusanya nguvu.

Lazima nitusue kama dangote.
 
Nigeria ya viwanda, sie tunajisifu na cherehani, Dangote ukinunua njoo uwekeze kwenye General tyre angalau ukifufue kizalishe matairi ya peugeout
 
Nigeria ya viwanda, sie tunajisifu na cherehani, Dangote ukinunua njoo uwekeze kwenye General tyre angalau ukifufue kizalishe matairi ya peugeout

General tyre si ndo yana ya Kenya mafisadi walshaiuza
 
General tyre si ndo yana ya Kenya mafisadi walshaiuza
Aje achukue general tyre bado kipo hakifanyi uzalishaji, YANA wanazalisha Kenya huko..atengeneze matairi ya viwango bei nafuu biashara ianze.
 
Go go go Platnamz😀😀😀😀
kuna msemo unasema ukipta jina la babu kama alikua mganga na ww lazima ushike usinge na pembe za kondoo😀😀
 
Back
Top Bottom