Toka niko std 1 mpaka namaliza chuo na leo nna mke na watoto ni mwendo wa dana dana tu.Napenda kutoa malalamiko yangu makali na kero kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya fidia kwa ardhi tuliyotoa KIPUNGUNI kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa serikali. Taarifa ya tathmini ya ardhi ilifanywa tangu jana, na hata miaka ya nyuma (1997), lakini hadi leo hatujaona malipo yoyote.
Yalishatolewa matamko kutoka kwa mawaziri wawili tena wakiwa bungeni, waliotoa ahadi hewa pamoja na mbunge wa segerea kuwa malipo yatafanyika mwaka huu, wakihakikisha yatafanyika mwezi huu wa nane ambao bado siku sita tu uishe.
Naomba malipo yafanyike mara moja ili tuweze kuhama kwenda maeneo bora zaidi, kwani haturuhusiwi kuendeleza chochote kattika maeneo haya ambayo sasa yamekuwa vichaka.
Aidha, tunasisitiza kwamba malipo haya yawe na riba kama ilivyoainishwa katika sheria za upatikanaji wa ardhi.
Tunahitaji hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha tunapata haki yetu.
Pia soma:Mbunge Bonna Kamoli atishia bungeni sakata la wananchi Kipunguni kupisha Airport, hawajalipwa fidia miaka 27 sasa
DaaahNadhani last month rais alisema malipo ya fidia yasubiri kwanza maendeleo yapatikane ndio wadai fidia waweze kulipwa.. Kama hiyo kauli haitatenguliwa danadana zitaendelea
Shangazii nikipotea wajukuu zako watalia sanaa acha tu tuone movie inaisha wapiiAunt, umekua sasa.
Ni vema kuwasimamia watu.
Sanaaa yaan wanapigwa kalenda kama watoto wa la sabadah inasikitisha
Alienda Mwigulu naye akapiga porojo zake weeee akajiondokeaDuuh hii fidia mpaka leo haijalipwa? Wawalipe bana Kipunguni imenikuza
BadoooDuuh hii fidia mpaka leo haijalipwa? Wawalipe bana Kipunguni imenikuza
Tapeli Mwigulu Nchemba ndio mnategemea awalipe?Kipunguni
Kipunguni
Kipunguni
Machozi yananitoka
Kama kijana nmesimama ujenzi miaka inasonga nguvu zinaisha hakuna kuendelea
Wapangaji wameondoka
Wazee wamekosa Kodi wanaishi maisha magumu
Ni wakati serikali iseme jambo moja inalipa ilipe watu wahame
Kama hakuna bomoa bomoa waseme tuendelee na mambo mengine
Ishu hii ina zaidi ya miaka 27
Kila kukicha ahadi zisizo fika ukomo.