Damu yamwagika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Damu yamwagika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Jun 7, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  MASJID HIJRA: ndiyo msikiti damu ilimomwagika Mtoni Mtongani Dar..kisa?
  [​IMG]Majeruhi akiwa hoi kwenye benchi la wagonjwa hospitali ya Temeke

  [​IMG]Mjahidina au ?
  Mapigano makali baina ya waumini wa dini ya Kiislam yaliyosababisha kumwagika kwa damu yametokea katika Msikiti wa Masjid Hijra, uliopo Mtongani jijini Dar es Salaam baada ya pande mbili za waumini hao kurushiana silaha kali na kuumizana.


  Kwa mujibu wa mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, mapigano hayo yaliyotokea saa 8.30 mwishoni mwa wiki iliyopita na kudumu kwa takriban dakika 30, yalifanya waumini kumi wajeruhiwe na kukimbizwa Hopitali ya Wilaya, Temeke kupata matibabu.


  Mtoa habari huyo alisema kuwa kama si polisi wa doria na wale wa Kituo kidogo cha Mtongani kufika eneo hilo mapema na kutuliza ghasia hiyo hali ingekuwa mbaya kwani waumini hao walikuwa wakirushiana mawe, nondo na silaha nyingine kali.


  Vurugu hizo zilisababisha Barabara ya Kilwa kutopitika kwa muda kutokana na waumini kujazana huku wakirusha mawe kuelekea msikiti huo mpya.


  Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, chanzo cha mapambano hayo ni baadhi ya waumini hao kutaka uitishwe uchaguzi wa viongozi na jina la msikiti huo ubadilishwe kutoka Masjid Hjira na kuwa Masjid Badri.

  Habari zinasema kuwa msikiti huo awali ulikuwa ukiitwa Masjid Badri kabla kuhamishwa ili kupitisha ujenzi wa barabara mpya ya Kilwa inayoendelea kujengwa hivi sasa ambapo kwa sasa viongozi wanaosimamia wameupa jina jipya la Masjid Hijra.


  Waandishi wetu ambao walifika katika eneo la tukio walishuhudia mawe na vipande vya nondo vilivyotumika katika mapambano hayo vikiwa karibu na msikiti huo huku baadhi ya watu wakiwa katika makundi kutafakari tukio hilo.


  Aidha, waandishi hao walikwenda katika Hopitali ya Wilaya ya Temeke na kuwakuta baadhi ya waumini waliojeruhiwa wakiwa wanapatiwa matibabu.


  Akiongea na mwandishi wetu mmoja kati ya viongozi wa msikiti huo aliyejitambulisha kwa jina la Shehe Mnondwa ambaye naye alipata kipigo kikali, alisema kuwa chanzo cha ugomvi huo ni tofauti ya msimamo kwani wakati wengine wanataka msikiti huo uandikwe jina jipya la Masjid Hijra, huku baadhi wanataka liandikwe jina la zamani la Masjid Badri.


  Aidha, Shehe Mnondwa alisema kuwa baadhi ya waumini wanataka kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wapya kutokana na waliopo kumaliza muda wake.


  Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kuwa kilichosababaisha kushindwa kufanyika kwa uchaguzi huo ni kuchelewa kukamilika ujenzi wa msikiti huo mpya. "Tusingeweza kufanya uchaguzi wakati tuko katika harakati za kumalizia ujenzi msikiti mpya baada ya kuhamisha ule wa zamani," alisema Shehe Mnondwa.


  Naye mmoja wa majeruhi hao aliyejitambulisha kwa jina la Issa Hussen alisema kuwa hii ni mara ya nne kutokea kwa vurugu katika msikiti huo, ambapo moja ya tukio kama hilo alisharipoti kwa Kituo cha Polisi Kilwa Road kwa jalada KLR/RB/5591/07 shambulio.


  Baadhi wa wananchi walishuhudia tukio hilo walishangazwa na waumini hao kufikia hatua hiyo ya kutoana damu katika kipindi hiki cha mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani, badala ya kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo.

   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duuu, kaaaazi kweli kweli. Hizi njaa jamani zinauwa kumbe. Leo zimejeruhi tu naona.
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Doedoe, nifafanulie tena. Hili tukio ni la lini?, ramadhani ipi?
   
 4. M

  MPG JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njaa mbaya sana
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli!
   
 6. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Ivi kweli kwa tukio kama hilo na sehemu yenyewe ni mtongani ni lakuja kuripotiwa leo? Una msukumo mwingine.wewe kama mwandishi baada ya kusikia kwa mtu umechukua jukum gani? Nadhani kwa mwandishi mzuri akisikia taarifa hakurupuki kuiandika bali anatakiwa kuifatilia ajue chanzo chake na sikuandika kwa hisia zako na kuweka maneno hata usiyoyajua maana yake.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  inawezekana wewe ndiyo huyu jamaa aliyeumia .... teh teh teh
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  kama watakatifu wanauana je sisi makafiri tufanye nini sasa?
   
 9. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TEH,TEEEEEEEH,Mkuu umenivunja mbavu kweli asbh hii!!
   
 10. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahahahahaa!!! we nouma chalii!!!! hahahahhaa!!!
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  aiseeee...:A S-coffee:
   
 12. M

  Maga JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mh sio kitu kizuri
   
 13. T

  Twasila JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Wanagombea jina au kuna kitu cha ziada!! Polisi wamechukua hatua gani? Tujuze. Hili si la kufumbia macho hasa kutokana na mwandishi kusema hili ni tukio la 4. Sheria ichukue mkondo wake. Tusisubiri kubeba maiti na kufanya post-mortem.
  Nya
   
 14. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Astakafulah, astakafulah, hivi allah huwa anasafiri na kusahau viumbe na ummah wake? Yaani hawa wanatoana damu kwenye nyumba ya allah? Na allah anaangalia tu,
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!dini sasa ni biashara!!
   
Loading...