Dalili za kiongozi dhaifu.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
1.Muda wote ni kulalamika-kiongozi dhaifu hukaa kulalamika juu ya tatizo na kulalamika ni dalili za kushindwa.
2. Hana maamuzi,hutegemea wengi wanasema nini juu ya jambo fulani,hususani raia wake.
3. Hushughulikia matokeo ya tatizo na sio vyanzo vya tatizo.
4.Huangalia nani kakosea/kamsababishia tatizo na sio kuangalia wapi amekosea.
5.Mara zote hupenda kujisifia hata kwa kitu kidogo/ anapotimiza wajibu wake- wakati wajibu ni sehemu ya kazi yake anapokea malipo kutokana na wajibu huo.
6. Hupenda kuweka ndugu/marafiki katika uongozi wake- hapo hushindwa kuwachukulia hatua wanapokosea.
7.Huwa hana vision- hajui vyanzo vya matatizo na namna ya kuyatatua. Kwa mfano umaskini katika nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania.
8.Huwa hapendi kukosolewa na yoyote anapofanya hivyo ajiandae kupoteza kucha na macho.
9.Huwa na matumizi makubwa ya vyombo vya dola kama vile polisi na jeshi dhidi ya raia wake wanaodai haki za msingi.
10.Hutoa majibu mepesi katika mambo magumu- kwa mfano udini Tanzania.
Ongeza na wewe........maoni tu jamani.
 
Back
Top Bottom