JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 703
- 1,225
Matatizo ya miguu au mikono kuhisi ganzi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa Neva za pembezoni mwa mwili (peripheral neuropathy), hivyo kusababisha kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika eneo husika (miguuni au mikononi).
Zifuatazo ni dalili za mguu au mkono kufa ganzi,
Maumivu au kuhisi kama vile moto unawaka miguuni au mikononi
Kuhisi kama vile umevaa soksi au gloves wakati hujavaa
Kuhisi kama vile kuna kitu chenye ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole
Sababu zinazopelekea neva kudhoofika na kupelekea ganzi ni kama zifuatazo:-
Kupungua kwa virutubisho mwilini. Hapa tunamaanisha mwili kutokuwa na Vitamin za kutosha hasa mkusanyiko wa Vitamini B Complex
Matumizi ya dawa fulani kwa muda mrefu mfano ARV
Uzito mkubwa wa mwili. Hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo huonekana tofauti na ilivyo kawaida.
Kubadilika huku husababisha baadhi ya Neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli au uzito wa mwili na hivyo kusababisha Neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake unaanza kuhisi maumivu au miguu au mikono kufa ganzi.
Ugonjwa wa kisukari.
Shinikizo la damu.