Dalili 10 za Mwanaume asiye na pesa kwa mpenzi wake

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
1. Kila siku appointment zake yeye ni gheto kwake au anang'ang'ania kuja kwako, hakuna hata kwenda beach wala hotelin.

2. Siku ukiwa unaenda kwake, anakwambia njoo kwenye saa tisa au kumi. Ujue amekadiria hiyo mida utakuwa umeshapata lunch.

3. Ukiwa unaenda kwake hasemi ukikaribia nishtue nitoke kukupokea, ujue anaogopa akifika kabla yako itabidi alipie bajaji.

4. Ukiwa unaondoka kwake anasema sijisikii vizuri kwahiyo siwezi kukusindikiza, ujue anaogopa unapopanda bajaji itabidi akulipie.

5. Ukimwambia umefulia, anakwambia "pole mpenzi ndio maisha hayo" ujue hana cha kukupa.

6. Mkiwa mpo mahali inabidi kila mtu aondoke peke yake ukasikia anasema mi ntapanda bajaji pale mbele kuna sehemu napitia, ujue hana hela anaenda kupanda daladala.

7. Kila mkienda kula restaurant jamaa anasema "mi nimetoka kula sio mda njaa haiumi" haagizi hata maji ya kunywa ujue jamaa hana kitu.

8. Kama upo mtandao tofauti na yeye kila siku ye anatuma tu sms, siku akitaka kupiga simu anakwambia "weka line ya tigo tuongee" ujue hana kitu huyo.

9. Ukiona anasisitiza kwamba hapendi wanawake wanaopenda vitu vya gharama kama simu n.k, ujue kaishiwa huyo akaoe ma house girl.

10.Ukiona kila siku ukikaa nae anakupa wosia kwamba mapenzi sio pesa, ujue hana kitu huyo.
 
Back
Top Bottom