Daladala zimekuwa kero

Daladala zimekuwa kero

Rexwinton

Member
Joined
Mar 26, 2021
Posts
74
Reaction score
137
Daladala siku hizi zimekuwa kero nyingi hazipo in good condition. Siti mbovu zimebanduka banduka. Nyingine hazina siti kabisa bio baadhi ya vioo vimebanduka, bado uvaaji wa makondakta ni wa ovyo lakini pia kauli zao chafu hazifai naomba uongozi ufuatlie hili suala kwa kweli
 
Bajaji ni nyingi zinapunguza abiria wa daladala, hivyo hesabu ya bosi hailipiki , na bosi anapokosa pesa inamaana ukarabati haufanyiki!

Usafi wa kondakta unachagiwa na uhaba wa sare za kubadilisha hivyo zinachakaa mapema! Pesa hakuna kumiliki sare nyingi!

Tiba yake!
1. Bajaji zizuiliwe au ziondelewe
2. Trafiki wapunguze mabao!
3. Madereva na konda wawe na mkataba na sare ilipwe na bosi kila baada ya miezi sita
4. Magari yabebe levo siti ili viti vidumu kuepusha kusukumana!

Mwisho kabisa! Ni ngumu hayo kuwezekana kutokana na rushwa na siasa iliyopo
 
Ila kati ya usafiri wa ilimradi ufike basi ni wa daladala,

Yaani upo ndani chini unaona lami,
Viti mobile, unatoka tabata upo nyuma unafika mjini upo mbele,

gari ikiingia kwenye shimo na wewe lazima uwende kwenye roof, ukishuka kiti kishaenda na mwenzako,

ukinunua maji hunywi mpaka ufike, au labda uinue shingo kama kuku, ukinunua karanga pact unafika umekula 2, nyingine zote zinapishana na mdomo,

Ikinyesha mvua unavujiwa,
Hapo hujapigwa Ndole, Wazee wa dunga dunga, huajamwagikiwa na Shombo ya Samaki..

Teja asipopewa 100 na konda, gari iking'oa anakulaba kibao.

Dar mtu akianza kununua gari kabla ya kujenga binafsi namuelewa.
 
Hizi daladala zitazoweka zenyewe mjini baada ya mji kuwa na usafiri wa kistaarabu pamoja miundombinu ya Mwendokasi ikifika kila mahali,ni suala la muda tu,wala hawatafukuzwa bali watajiondoa wenyewe maana bajaji wanafanya kazi nzuri mno
 
kuna TATA mpya zimeingia, BY/Sokoni - M/Complex,
aisee, uikute imechanganya kule kwa Mbiki aah mbona utaipenda
 
Hizi daladala zitazoweka zenyewe mjini baada ya mji kuwa na usafiri wa kistaarabu pamoja miundombinu ya Mwendokasi ikifika kila mahali,ni suala la muda tu,wala hawatafukuzwa bali watajiondoa wenyewe maana bajaji wanafanya kazi nzuri mno
Kuruhusu BAJAJ kufanya biashara ya kubeba abiria tena Katikati ya JIJI ni ukichaa/uendawazimu maaana tulizuia HIACE kwamba ni VIPANYA vinaleta foleni then leo tumeruhusu BAJAJ ambazo zimekuwa UTITIRI MJINI inafikirisha sana sisi Watanzania zama hizi kuwa na takataka za aina hii katikati ya JIJI.
Kwa kifupi Bajaj ziondolewe tuache siasa.
 
Inategemea ni dala dala za wapi

Njiro- town, ziko poa..
 
Kuna Daladala za Makumbusho-Stesheshi, mvua ikinyesha ndani inavuja unakuwa sawa na aliye nje.
 
nunua gariyako uache lawama.kama huna pambana nahaliyako.
 
Back
Top Bottom