Daladala zetu

Zerock

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
214
Reaction score
359
Kila mwaka,wamiliki wa magari ya daladala hupeleka vyombo vyao ili kupasishwa kuendelea kufanya route zao (kubeba abiria)

Ajabu zile gari sijui huwa zinakaguliwa na vipofu au watu wa aina gani, unakuta gari yote ni mbovu ila ni nzima tu kwa sababu bado inakimbia.
Ukiiangalia kuanzia kwa dreva (mbele) steering ni ngumu kuizungusha kupiga kona (turn),viti vya abiria vibovu,bodi ya juu inavuja kama mvua ikinyesha.
Lakin ajabu hiyo gari itapasishwa inafaa kubeba abiria.
Hii hali ni sehemu zote (Zanzibar na Tanganyika)
Sijui mamlaka husika zinakagua vipi hizi gari,au wamiliki wa magari ndo wanajikagua.
Hii ndio Tanzania yetu kwa ujumla
 
Reactions: Lax
sio tu daladala , emu fikiria huo driving school kwenyewe gari mbovu, na zenyewe zinakaguliwa na kuthibitishwa.

sheria zianze kufuatwa
 
Huwa wananunua tu stika ya usalama barabarani wanabandika bila kukaguliwa
Tena walivyo wajinga bora gari mbovu ila iwe tu na stika kuliko gari nzima halafu Haina stika mambo ya kisenge sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…