Daladala zaenguliwa D'Salaam

Daladala zaenguliwa D'Salaam

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
Ahmad-Kilima.jpg

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Ahmad Kilima

Mpango wa kuziondoa daladala jijini Dar es Salaam ‘umeiva’, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kueleza kuwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu, wasafirishaji wa magari hayo katika barabara za Kilwa na Ali Hassan Mwinyi, hawataruhusiwa kutoa huduma hiyo kama watakuwa hawajajiunga na kuanzisha kampuni au ushirika wa kusimamia usafiri huo.

Sumatra imesema kujiunga na kuanzisha kampuni au ushirika kwa wasafarishaji hao kutawawezesha kupewa leseni za kutoa huduma katika njia husika kuanzia tarehe hiyo.
Hata hivyo, Sumatra imesisitiza kuwa vigezo na masharti ya leseni za usafirishaji vitazingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya; ambavyo ni pamoja na kampuni kuwa na mabasi yasiyopungua 100 na yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 70.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Sumatra kusitisha utoaji wa leseni mpya kwa mmiliki mmoja mmoja wa magari hayo ya abiria yanayopita katika njia hizo, kuanzia Mbagala kwenda maeneo ya jiji kati na maeneo mengine, na kuanzia Mwenge kwenda maeneo ya jiji kati.Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabarani wa Sumatra, Leo Ngowi, alisema jana kuwa mwisho kwa wasafirishaji hao kuanzisha kampuni au ushirika huo, ni Juni 30, mwaka huu.Ngowi alisema hayo wakati akiwasilisha mada ya hatua ya kuboresha huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam kwa kupitia kampuni za usafiri, katika mkutano wa wadau kuhusu uanzishwaji wa utoaji leseni kwa kampuni za usafirishaji abiria, ulioandaliwa na Sumatra jijini humo jana.

Ili kuonyesha kuwa Sumatra iko makini juu ya utaratibu huo mpya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Ahmad Kilima, aliwaeleza wadau kuwa fursa za kutoa huduma ya usafiri wa magari hayo Dar es Salaam, bado zipo, hivyo akawataka wasafirishaji wasioweza kuungana na kuanzisha kampuni waende wakaendelee kutoa huduma hiyo nje ya jiji, ikiwamo Mabwepande.
Ngowi alisema hatua hiyo imechukuliwa na Sumatra kama njia mojawapo ya kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika jiji hilo, ikiwa ni pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri kujiandaa kushiriki katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Darts) na kuwa na kampuni chache zenye uwezo wa kutoa huduma bora na mabasi yenye viwango.Ngowi alisema Sumatra ilisitisha utoaji wa leseni mpya kwa mmiliki mmoja mmoja kwa magari yanayopita katika njia hizo, kuanzia Desemba Mosi, mwaka jana.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuanzia Juni 30, mwaka huu, Sumatra itasitisha uendelezaji wa leseni kwa mmiliki mmoja mmoja anayetoa huduma katika njia hizo.Alisema kwa wale, ambao leseni zao zinaisha kabla ya Juni 30, Sumatra itaziendeleza kwa kuwapa leseni za muda mfupi zitakazoishia tarehe hiyo.“Katika kipindi cha kuanzia tarehe 01/12/2012 hadi tarehe 30/06/2013 wasafirishaji wanaotoa huduma katika njia hizo wanashauriwa kujiunga na kuanzisha kampuni au ushirika ili waweze kupewa leseni za kutoa huduma katika njia husika kuanzia tarehe 01/07/2013,” alisema Ngowi.

Vigezo vya Kampuni ya safirishaji
Alivitaja vigezo vingine vya kampuni ya usafirishaji kuwa ni iliyosajiliwa Tanzania, iwe na ofisi yenye anuani na mahali, muundo wa kampuni, mpango kazi wa kampuni, eneo la mkuhifadhi na kufanyia matengenezo, mmahesabu ya mapato na matumizi, mpango wa ukaguzi na usimamizi wa magari.Vigezo vingine ni mfumo wa kutoa tiketi, mfumo wa udhibiti wa mapato na kuzuia matumizi ya wapigadebe, mpango wa upangaji na ufuatiliaji wa ruti, utaratibu wa ajira kwa madereva na makondakta na kadiri maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na mdhibiti.

Awali, Ngowi alisema hali ya utoaji huduma ya usafirishaji abiria katika jiji la Dar es Salaam haikidhi viwango vya ubora na kwamba, inakabiliwa na changamoto kadhaa; ikiwamo miundombinu isiyotosheleza mahitaji.Changamoto nyingine alizitaja kuwa ni uduni wa vyombo vya uchukuzi; ikiwamo mabasi kuwa chakavu, uwezo mdogo wa mabasi, weledi usiotosha katika kuendesha biashara ya usafirishaji na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji zinazochangiwa na bei ya mafuta na vipuri.

Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni watoa huduma wenye mitaji midogo, matengenezo hafifu na yasiyokidhi viwango vya usalama na ubora, usimamizi duni katika uendeshaji wa biashara ya usafirishaji na kutofanyia matengenezo magari.Changamoto nyingine ni kutokuwa na utamaduni wa kutii sheria kwa baadhi ya wamiliki, madereva na makondakta na malengo makubwa ya fedha kwa siku wanayowwawekea madereva.

Ngowi alisema katika Jiji la Dar es Salaam ni kampuni chache ndizo zinazomiliki vyombo vya usafiri; kama vile Uda na Cordial Transport, ambazo kila moja umiliki wake uko kwa mtu binafsi, wakati leseni hutolewa kwa chombo cha usafiri. Hata hivyo, alisema muundo wa kampuni una manufaa makubwa kwa kuwa mmiliki wake anakuwa na wakaguzi, ambao pamoja na kudhibniti matumizi mabaya ya magari yao, hudhibiti pia uvujaji wa mapato ya kampuni, pia kampuni zitakuwa na uwezo wa kutoa huduma bora na mabasi yenye viwango.Alisema pia wamiliki wa kampuni kufanya biashara ya usafirishaji kwa weledi na ufanisi zaidi, uwezekano wa kupata menejimenti ya kisasa na yenye taaluma katika mambo ya usafirishaji na pia kuweza kuandaa taarifa za kihasibu na kuwa na utaratibu wa kuweka pesa benki.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk, aliwataka wamiliki wa magari kutokuwa waoga kuupokea mfumo huo mpya wa kutoa huduma ya usafiri wa magari hayo jijini humo.Kutokana na hali hiyo, aliwaeleza wamiliki wenzake wa magari hayo kuwa hawana budi zaidi ya kuungana na kuanzisha kampuni zao ili kuingia kama wanataka kuendelea kutoa huduma jijini humo.Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Kilima alisema sekta ya usafirishaji abiria nchini inazidi kukua kwa kiwango cha kuridhisha na kwamba, sasa Watanzania wanashuhudia wamiliki hususan wa mabasi ya masafa marefu wakiwekeza katika mabasi mapya na yenye viwango vya juu.Baadhi ya wadau katika kuchangia utaratibu huo mpya, walionyesha wasiwasi wao kuhusu kuungana wakisema ni vigumu katika kipindi kifupi cha miezi minne na wengine kushauri ufanyike utafiti kubaini mambo yaliyosababisha baadhi ya mashirika ya zamani kufeli katika suala hilo.Hata hivyo, wengi walikubaliana na utaratibu huo mpya baada ya kuanza kujiorodhesha kwenye daftari maalum lililowekwa na uongozi wa Sumatra katika mkutano huo.

Mmoja wa wadau hao, Azim Dewji, licha ya kusaini daftari hilo, pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo, aliitaka Sumatra kueleza wapi mabasi hayo 100, ambayo kampuni imetakiwa kuwa nayo, yatakapokuwa yakilazwa.Naye Mratibu wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Magari ya Abiria nchini Kenya, maarufu kama “Matatu”, Albert Karakacha, aliwaondoa hofu wasafirishaji wa Kitanzania, akisema utaratibu huo hauna tatizo, badala yake una faida nyingi iwapo wataungana na kuwa wa wazi.Alisema kwa kutekeleza utaratibu huo, mwaka 2008 walianza na basi moja, lakini hivi sasa wameweza kumiliki mabasi 150 na kwamba, unawasaidia kutoa ajira kwa watoto wao pindi wanapomaliza shule.
 
Hivi huu mradi wa magari yaendayo kasi wanategemea hizohizo daladala zilizopo hapo Dar? Kama ni hivyo basi hakukuwa na sababu ya vunjavunja
 
Kama inawezekana, ningeshauri SUMATRA wangewapatia ka-training hawa wamiliki wa mabasi ili kuwajengea uwezo kabla ya kujiunga. Kwa mtu ambaye amekuwa anapokea mahesabu kila jioni, na ana maamuzi katika kila jambo, lazima aingiwe na hofu juu ya hatma yake kwenye huu mfumo mpya wa kuwa na makampuni. Ni vema kukawa na msaada wa kimafunzo kipindi hiki cha mpito ili watu wavuke salama.
 



Wednesday, February 6, 2013



Ahmad-Kilima.jpg


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Ahmad Kilima


Mpango wa kuziondoa daladala jijini Dar es Salaam ‘umeiva', baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kueleza kuwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu, wasafirishaji wa magari hayo katika barabara za Kilwa na Ali Hassan Mwinyi, hawataruhusiwa kutoa huduma hiyo kama watakuwa hawajajiunga na kuanzisha kampuni au ushirika wa kusimamia usafiri huo.


Sumatra imesema kujiunga na kuanzisha kampuni au ushirika kwa wasafarishaji hao kutawawezesha kupewa leseni za kutoa huduma katika njia husika kuanzia tarehe hiyo.

Hata hivyo, Sumatra imesisitiza kuwa vigezo na masharti ya leseni za usafirishaji vitazingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya; ambavyo ni pamoja na kampuni kuwa na mabasi yasiyopungua 100 na yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 70.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Sumatra kusitisha utoaji wa leseni mpya kwa mmiliki mmoja mmoja wa magari hayo ya abiria yanayopita katika njia hizo, kuanzia Mbagala kwenda maeneo ya jiji kati na maeneo mengine, na kuanzia Mwenge kwenda maeneo ya jiji kati.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabarani wa Sumatra, Leo Ngowi, alisema jana kuwa mwisho kwa wasafirishaji hao kuanzisha kampuni au ushirika huo, ni Juni 30, mwaka huu.

Ngowi alisema hayo wakati akiwasilisha mada ya hatua ya kuboresha huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam kwa kupitia kampuni za usafiri, katika mkutano wa wadau kuhusu uanzishwaji wa utoaji leseni kwa kampuni za usafirishaji abiria, ulioandaliwa na Sumatra jijini humo jana.

Ili kuonyesha kuwa Sumatra iko makini juu ya utaratibu huo mpya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Ahmad Kilima, aliwaeleza wadau kuwa fursa za kutoa huduma ya usafiri wa magari hayo Dar es Salaam, bado zipo, hivyo akawataka wasafirishaji wasioweza kuungana na kuanzisha kampuni waende wakaendelee kutoa huduma hiyo nje ya jiji, ikiwamo Mabwepande.

Ngowi alisema hatua hiyo imechukuliwa na Sumatra kama njia mojawapo ya kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika jiji hilo, ikiwa ni pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri kujiandaa kushiriki katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Darts) na kuwa na kampuni chache zenye uwezo wa kutoa huduma bora na mabasi yenye viwango.

Ngowi alisema Sumatra ilisitisha utoaji wa leseni mpya kwa mmiliki mmoja mmoja kwa magari yanayopita katika njia hizo, kuanzia Desemba Mosi, mwaka jana.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuanzia Juni 30, mwaka huu, Sumatra itasitisha uendelezaji wa leseni kwa mmiliki mmoja mmoja anayetoa huduma katika njia hizo.

Alisema kwa wale, ambao leseni zao zinaisha kabla ya Juni 30, Sumatra itaziendeleza kwa kuwapa leseni za muda mfupi zitakazoishia tarehe hiyo.

"Katika kipindi cha kuanzia tarehe 01/12/2012 hadi tarehe 30/06/2013 wasafirishaji wanaotoa huduma katika njia hizo wanashauriwa kujiunga na kuanzisha kampuni au ushirika ili waweze kupewa leseni za kutoa huduma katika njia husika kuanzia tarehe 01/07/2013," alisema Ngowi.

Alivitaja vigezo vingine vya kampuni ya usafirishaji kuwa ni iliyosajiliwa Tanzania, iwe na ofisi yenye anuani na mahali, muundo wa kampuni, mpango kazi wa kampuni, eneo la mkuhifadhi na kufanyia matengenezo, mmahesabu ya mapato na matumizi, mpango wa ukaguzi na usimamizi wa magari.

Vigezo vingine ni mfumo wa kutoa tiketi, mfumo wa udhibiti wa mapato na kuzuia matumizi ya wapigadebe, mpango wa upangaji na ufuatiliaji wa ruti, utaratibu wa ajira kwa madereva na makondakta na kadiri maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na mdhibiti.

Awali, Ngowi alisema hali ya utoaji huduma ya usafirishaji abiria katika jiji la Dar es Salaam haikidhi viwango vya ubora na kwamba, inakabiliwa na changamoto kadhaa; ikiwamo miundombinu isiyotosheleza mahitaji.

Changamoto nyingine alizitaja kuwa ni uduni wa vyombo vya uchukuzi; ikiwamo mabasi kuwa chakavu, uwezo mdogo wa mabasi, weledi usiotosha katika kuendesha biashara ya usafirishaji na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji zinazochangiwa na bei ya mafuta na vipuri.

Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni watoa huduma wenye mitaji midogo, matengenezo hafifu na yasiyokidhi viwango vya usalama na ubora, usimamizi duni katika uendeshaji wa biashara ya usafirishaji na kutofanyia matengenezo magari.

Changamoto nyingine ni kutokuwa na utamaduni wa kutii sheria kwa baadhi ya wamiliki, madereva na makondakta na malengo makubwa ya fedha kwa siku wanayowwawekea madereva.

Ngowi alisema katika Jiji la Dar es Salaam ni kampuni chache ndizo zinazomiliki vyombo vya usafiri; kama vile Uda na Cordial Transport, ambazo kila moja umiliki wake uko kwa mtu binafsi, wakati leseni hutolewa kwa chombo cha usafiri.

Hata hivyo, alisema muundo wa kampuni una manufaa makubwa kwa kuwa mmiliki wake anakuwa na wakaguzi, ambao pamoja na kudhibniti matumizi mabaya ya magari yao, hudhibiti pia uvujaji wa mapato ya kampuni, pia kampuni zitakuwa na uwezo wa kutoa huduma bora na mabasi yenye viwango.

Alisema pia wamiliki wa kampuni kufanya biashara ya usafirishaji kwa weledi na ufanisi zaidi, uwezekano wa kupata menejimenti ya kisasa na yenye taaluma katika mambo ya usafirishaji na pia kuweza kuandaa taarifa za kihasibu na kuwa na utaratibu wa kuweka pesa benki.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk, aliwataka wamiliki wa magari kutokuwa waoga kuupokea mfumo huo mpya wa kutoa huduma ya usafiri wa magari hayo jijini humo.

Kutokana na hali hiyo, aliwaeleza wamiliki wenzake wa magari hayo kuwa hawana budi zaidi ya kuungana na kuanzisha kampuni zao ili kuingia kama wanataka kuendelea kutoa huduma jijini humo.


Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Kilima alisema sekta ya usafirishaji abiria nchini inazidi kukua kwa kiwango cha kuridhisha na kwamba, sasa Watanzania wanashuhudia wamiliki hususan wa mabasi ya masafa marefu wakiwekeza katika mabasi mapya na yenye viwango vya juu.


Baadhi ya wadau katika kuchangia utaratibu huo mpya, walionyesha wasiwasi wao kuhusu kuungana wakisema ni vigumu katika kipindi kifupi cha miezi minne na wengine kushauri ufanyike utafiti kubaini mambo yaliyosababisha baadhi ya mashirika ya zamani kufeli katika suala hilo.

Hata hivyo, wengi walikubaliana na utaratibu huo mpya baada ya kuanza kujiorodhesha kwenye daftari maalum lililowekwa na uongozi wa Sumatra katika mkutano huo.

Mmoja wa wadau hao, Azim Dewji, licha ya kusaini daftari hilo, pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo, aliitaka Sumatra kueleza wapi mabasi hayo 100, ambayo kampuni imetakiwa kuwa nayo, yatakapokuwa yakilazwa.

Naye Mratibu wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Magari ya Abiria nchini Kenya, maarufu kama "Matatu", Albert Karakacha, aliwaondoa hofu wasafirishaji wa Kitanzania, akisema utaratibu huo hauna tatizo, badala yake una faida nyingi iwapo wataungana na kuwa wa wazi.

Alisema kwa kutekeleza utaratibu huo, mwaka 2008 walianza na basi moja, lakini hivi sasa wameweza kumiliki mabasi 150 na kwamba, unawasaidia kutoa ajira kwa watoto wao pindi wanapomaliza shule.




CHANZO: NIPASHE





 
usafiri dar umeshikiliwa na wahuni sana,bila kufikiria kama kuna ufisadi ndani yake kwenye huu mradi,naunga mkono hoja
 
Mpango mzuri. Utapunguza msongamano na foleni za magari City centre
 
acha tuone maana hivi mmoja mmoja na usafiri bado ni tete je kwa mfano tukapata kampuni mbili huo usafiri utatosha?
 
ni hatua inayo faa, lakini bus route hakuna, hivyo ratiba ya basi kufika kituo a au be itakuwaje kwa wakati unaofaa itakuwaje.
 
kwa portion niliyosoma, it sounds good. Huwa najiuliza hivi hizi DCM za Mbagala , Segerea, na baadhi ya costa chakavu , chafu, kweli zina hadhi ya kuwa city bus kweli? No we need to be serious . Usafiri wa heshima na uhakika, utapunguza sana mindset za watu kukimbilia kuchukua mikopo ya magari badala yake watafikiria kuwekeza kwingine.
 
Tutegemee Mabadiliko ya aina gani ? Isije ikawa longo longo zao kama siku zote .
 
tusubiri tuone hayo makampuni yatakayoundwa kwa shindikizo! wengi wataacha na watawekeza kwenye biashara zingine.
 
Mpango mzuri. Utapunguza msongamano na foleni za magari City centre

Binafsi nimefurahishwa na mpango huu, haya madaladala yana usumbufu, no control, hawana muda, zaidi kuvuruga traffic. Basi moja kubwa litakuwa na uwezo wa kumeza abiria wa daladala mbili hadi tatu, hapa msongamano haujapungua licha ya roughness za madereva wa daladala.

Tuache kupondo kila kitu, mpango huu nawafagilia.
 
mi mpaka ukianza ndo nitawaamini maana viongozi wa bongo kwa kutujengea maghorofa vichwani mwetu imekua tofi sasa.
 
Tz kwa miradi hatujambo!
Huu utaanza,na punde utafifia wakishapata chao.
 
Hii ni kutusumbua tu na Biashara Zetu yaani navyopata Presha we acha tu kama ndio huu ujinga niliokuwa nautegemea wanataka kuufanya nimeamini si bora wangeweka treni tu
 
Back
Top Bottom