Daladala inayoitwa Babylon T 932 BHE kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daladala inayoitwa Babylon T 932 BHE kulikoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Apr 26, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF na wapenda maendeleo, jana (April 25, 2011) nilikuwa Kimanzichana (Wilaya ya Mukuranga) na nilipanda Hiace moja inayoitwa BABYLON T 932 BHE (mali ya Othman M Hassan PO Box 273, Zanzibar) kwenda Dar es Salaam.

  Tulipokaribia Mbagala Rangi Tatu (kwenye saa mbili hivi usiku) kulikuwa na foleni ya magari lakini ilikuwa inaenda taratibu. Ilikuwa kama nusu kilomita hivi kufika kituoni Mbagala Rangi 3. Kilichofanyika dereva alisimamisha gari na kutuambia tuteremke huku akisema anataka kwenda kupaki gari na haendi sehemu yoyote zaidi ya pale aliposimamisha gari. Alisema dereva ndiye anayeamua wapi awateremshe abiria na kama tunataka kwenda kushtaki polisi twende hana wasiwasi kwani hata akienda ndani hatakaa muda mrefu na amezoea hali hiyo.

  Baadhi ya abiria (hasa wale ambao walikuwa wamefika na pengine hawakuwa na mizigo mizito waliamua kushuka) na abiria watano hivi tuliamua kubaki na kuendelea kudai atufikishe kituoni kuliko kutuacha mbali vile maana wengine walikuwa na mizigo mizito. Hata kama wasingekuwa na mizigo mizito utaratibu ni kufika kituoni na si sehemu dereva anayoamua awateremshe abiria. Tulijaribu kumwelemisha kuwa tulipopanda gari na kulipa nauli 2,000/- tuliingia mkataba kutoka ituo cha Kimanzichana hadi cha Mbagala Rangi 3 tu.

  Kulikuwa na mabishano sana kati ya dereva + konda wake upande mmoja na sisi abiria tuliokuwa tumebakia ndani ya lile gari. Kisha kwa shingo upande akaamua kutusogeza mbele kidogo na kusimama katikatika ya maji machafu akidai atatupeleka hadi kituo cha Mbagala Rangi 3 pale foleni itakapopungua.

  Tulibaki pale kwa muda wakati magari mengine yalikuwa yakipita. Alifanya hivyo makusudi kutukomesha kwa vile aliona tunadai atende haki na siyo kutumia lugha mbaya na mabavu kwa vile tumeishalipa nauli. Baadaye alilitoa gari kwenye yale matope na kupaki sehemu kavu na akasema kama tunataka kubaki ndani tubaki na yeye haendeshi gari tena. Muda huo foleni ilikuwa imeshaanza kupungua.

  Kwa kweli mimi niliumia sana hasa kuona kuwa abiria tunanyanyasika kwa namna ile, Kisha lisema hatuna hela kama tungekuwa na hela tusingepanda daladala.

  Nilitaka kupiga simu kwa mwenye gari kulalamika lakini tiketi tulizopewa hazikuwa na namba ya simu ila jina na anwani yake tu. Kwa vile sisi wanaJF tunapenda maendeleo katika nchi yetu na pia tunapenda wanaofanya biashara wafanye kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa, naomba kama kuna mwanaJF anamfahamu mwenye daladala hii ya BABYLON amjulishe kuwa dereva na konda wake ni wahuni watamharibia biashara. Ni afadhali aweke watu wastaarabu na siyo wahuni kwa vile wanalipwa kidogo.

  Naomba wanaJF tuisusie Hiace hii kwa sababu ya dereva na konda wake kutumia lugha chafu na ya kudhalisha dhidi ya abiria badala ya kutumia lugha ya kistaarabu na inayowafanya abiria wapende huduma za gari hili. Naomba maoni yenu.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu je unauhakika hiyo gari haijauzwa kwa mmiliki mwingine??Anwani si tija kwani wengi wananua magari lakini hawabadili anwani lamsingi kuna namba za kova mwenye nayo aweke unamtwangia biashara anamaliza anamchezo na makonda,driver wahuni!!Bottomline!
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hahahahaha! Nmecheka alivyowaambia hamna hela, kwa hiyo kupanda daladala ni kutokuwa na hela?? Kweli amekosa ustaarabu kabisa!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  ungemwendea kova hewani
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  shukrani za punda hizi, tusipopanda haya mabasi yao atapata wapi ajira?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Pole sana kiongozi wangu!
  Shida ya hawa vijana madereva wanakuwa wamevuta bangi zao wanajiona ndo wamiliki!
  Dawa ilikuwa ni kumpigia Kova kama alivyoshauri KKKZ, na kisha mwenye gari angejua cha kufanya na huyu mla mirungi!
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Nadhani hawana akili madereva wa Daladala pamoja na makonda wao!
   
 8. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mkuu, naomba namba ya simu ya Kova maana hawa watu wanatudhalilisha sana!
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  ndo mana nikacheka sana, majibu ya hawa madereva wa daladala wakat mwngine ni kichefuchefu, watu wanataka awafikishe mwisho wa gari yeye anawaambia hawana hela, ina mana walipanda bure kutoka huko kimanzichana??
  Wasingepanda je angefanya kazi gani? Ajira yake mwenyewe anashindwa kuithamini, naungana na PJ kuwa hawa wenzetu wengi ni bange ndo zinawasumbua! Kazi kweli.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  tena ni vizuri sab=na unaikumbuka namba yao ya gari
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ebwanaee, pole sana Muungwana kwa kudhalilishwa.... Ndo dunia hii, pigania haki yako, usiombe!!
   
Loading...