Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 15, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,505
  Likes Received: 5,737
  Trophy Points: 280
  Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi Send to a friend Monday, 14 March 2011 21:40 0diggsdigg

  [​IMG]Mussa Juma, Loliondo na Deusdedit Moshi, Dodoma
  DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la 'Babu', huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi.
  Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Sonjo iliyoshirikisha mamia ya watu. Akizungumza katika ibada hiyo, Mchungaji Mwasapile alisema Lengume ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza kumtibu.

  Akizungumza na Mwananchi kanisani hapo, Lengume alisema baada ya mumewe, John Meneyi Lengume kufariki dunia mwaka 2002, aliamua kwenda kupima na kuonekana kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) lakini baada ya kutumia dawa hiyo alisema sasa hana tena virusi vya Ukimwi. Alisema kwa muda mrefu mama huyo alikuwa akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARV) katika Kituo cha Afya Didodigo wilayani Ngorongoro.
  Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kupona kwa mama huyo, Dk Mbosha alisema: “Hiki kitu kilituchanganya sana, nakumbuka mimi ndiye nilimpima mwaka jana... ikabidi niwaeleze watu wa maabara Hospitali ya Wasso ili wafuatilie aliyempima awali huyu mama na nilimweleza aache kutumia dawa kwani hana HIV,” alisema Dk Mbosha.
  Dk Mbosha alisema alihamishiwa katika kituo hicho cha Afya cha Digodigo zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alimkuta mama huyo akiendelea kuhudhuria kliniki na kupata ARV pamoja na ushauri wa kulinda afya yake lakini alianza kuona mabadiliko makubwa ya afya yake na ndipo alipoamua kumpima tena.

  Aliamua kumpima mwaka jana baada ya kuona 'CD4' (kinga za mwili) zake zinaimarika kiasi cha kutohitaji kuendelea kutumia dawa hizo za kupunguza makali.Aliamua kumhoji kujua siri iliyokuwa imejificha katika mabadiliko hayo ambayo alisema yalikuwa ya haraka haraka mno na ndipo alipomweleza kwamba alipata tiba kutoka kwa Mchungaji Mwasapile.
  Lengume alisema licha ya mumewe kufariki, mtoto wao mmoja pia alifariki dunia lakini baada ya kutumia dawa ya Mchungaji Mwasapile, maisha yake ni mazuri na ana mtoto mwingine mchanga anayeitwa Evelyn ... “Namshukuru Mungu na Mchungaji Mwasapile sasa nimepona na ninaishi maisha mazuri tu.”Alisema baada ya kuanza kuugua, mchungaji huyo, ndiye aliyemfuata na kumuomba amtibu akimthibitishia kwamba atapona maradhi yaliyokuwa yakimsibu.Hata hivyo, kitalaamu bado haijathibitika kupatikana kwa tiba wala chanjo ya Ukimwi.

  Ushuhuda wa Mzee Mtaki
  Mwingine aliyejitangaza kupata ahueni kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsibu baada ya kupata tiba ya mchungaji huyo ni aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mzee Ali Said Mtaki.Mzee Mtaki (81) ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mpwapwa katika miaka ya 1980, Mkuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida kwa nyakati tofauti, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mbunge wa Afrika Mashariki na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Usharika Mkoa wa Dodoma, alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kutetemeka kiasi cha kushindwa kutembea na kuzungumza vizuri.

  Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Mtaa wa Nyerere Mjini Dodoma, Mzee Mtaki alisema tangu anywe dawa ya mchungaji huyo Jumanne ya wiki iliyopita huko Loliondo, sasa anaendelea kupata nafuu siku hadi siku.
  Akiongea kwa kujiamini alisema sasa anajiona kama amepona na anaweza kuendelea na shughuli zake ikiwamo ya uwakala wa bima... "Si unaona nilikuwa natembea kwa shida, kuzungumza kwa taabu, sasa hali yangu ni nzuri nafanya kila kitu bila kusaidiwa.”Akielezea safari yake ya siku mbili ambayo ilimfikisha kijijini Samunge, Loliondo anasema alifuatana na mkewe, Amina Mtaki ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na mgongo. Anasema naye pia amepona.

  Anasema safari ya kutoka Dodoma hadi Samunge iliwagharimu Sh60,000 kila mmoja na baada ya kufika huko walikuta umati mkubwa wa watu ukisubiri kupata tiba hiyo. Anasema aliwakuta watu wa mataifa mbalimbali, Waafrika, Wahindi, Wazungu na Waarabu... "Watu walikuwa wengi na kila mtu na matatizo yake lakini Mchungaji alikuwa akiwasisitizia kwamba habagui watu na haangalii dini au uwezo wa mtu."
  “Katika mkusanyiko huo nilibahatika kukutana na Askofu Thomas Laizer wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati akiwa amefuatana na mama wa kizungu. Nilikaa karibu na mama yule wa kizungu ambaye sikumbuki jina lake. Nilimshika Askofu Laizer mkono tukasalimiana na kuongozana naye kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile."

  "Tulipofika kwa Mchungaji, Askofu Laizer akamwambia mchungaji kwamba ana wageni wake, hivyo mama yule wa kizungu akapewa dawa na mimi pia nikapewa na mke wangu akapewa pamoja na kijana wangu japo yeye hakuwa na tatizo lolote la kiafya."

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Last Updated on Tuesday, 15 March 2011 08:54
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wabishi wataendelea kubisha tu!
  Watakwambia ..."sample size ni ndogo...labda wawe watu 20"
  Na wakifika ishirini, watageuka na kutaka 100!
  Upinzani kwa kila huduma upo tu!, cha kufanya ni kuwa wanaoamini waende, na wasioamini wabaki kunywa madawa yasiyoponya na yenye masumu kibao huko mahospitalini, basi!
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Huyu mama ndo alikuwa miongoni wa watu wa kwanza kukiri kuwa wamepona Mungu mkubwa
   
 4. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Watasema kama wasemavyo siku zote kwenye mikutano ya Injili Yesu anapofanya uponyaji, "Wale watu wao, waliwaleta waliwapa hela waseme wamepona kwa kuombewa!" Hata kwenye biblia walikuwepo wabishi. Sitashangaa ila ukweli, Mungu yupo na acheni aitwe Mungu.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,505
  Likes Received: 5,737
  Trophy Points: 280
  Yaani huyu n kumjaza lishe tu ndicho kinachokosekana hapo
  mwezi umuwamini tena
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi sielewi hii serikali iiliyojipachika jina la ari mpya nguvu mpya.

  kwa nini wanachelwa kutoa majiu japo ya awali kwa umma

  • waliotumia dawa wapo
  • watu wa kujitolea kufanyiwa sampling kutumia dawa hata kama ina madhara wapo
  • mabaara zipo
  • Dawa ipo
  Sasa utadhani dawa ndo inaombewa kibali cha kutumika kwa mara ya kwanza ambapo inakuwa kazi kuthibitishwa sababu huwezi kufanya mjaribio kwa watu.

  Serikali itoe jibu mapema liwe la kupendeza au la kuchukiza watu waeedlee na mengineyo.
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  teh teh teh! Nikweli kwani ukumuangalia anaonekana bado u mgonjwa.
   
Loading...